05/18/2026
KANISA TUNAPASWA KUJIANDAA NA KUWA TAYARI KATIKA SIKU HIZI ZA MWISHO
Kanisa k**a Bibi-Arusi tunapaswa kujiandaa ili kukutana na Bwana-Arusi Yesu Kristo katika siku hizi za mwisho. Kanisa tunapaswa kujitayarisha katika Utakatifu (usafi wa kiroho), Maombi, Kukesha, Uaminifu, Uvumilivu, Upendo, Utayari wa kiroho, Kweli ya Neno, Kujitenga na ulimwengu, Maisha katika Roho, na Umoja katika Kristo.
1. Bibi-Arusi kujiweka tayari kwa ajili ya kukutana na Bwana-Arusi
Kanisa ni Bibi-arusi wa Kristo anayepaswa kujiweka tayari kwa ajili ya kukutana na Bwana arusi wake.
“Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu” (Ufunuo 19:7–8).
“Kristo naye alilipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote k**a hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.” (Waefeso 5:25–27).
“Kwa maana nimewaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi” (2 Wakorintho 11:2).
2. Kukesha na Kuwa Tayari
Yesu alilionya Kanisa mara nyingi kukesha kiroho na kuwa tayari wakati wote.
“Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu…Kwa hiyo ninyi nanyi iweni tayari…” (Mathayo 24:42–44).
Mathayo 25:1–13 inatufundisha juu ya kujiandaa kiroho na kuwa na mafuta katika taa zetu.
“Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.
Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.
Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa” (Mathayo 25:1-13).
“Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, k**a mtego unasavyo; kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu” (Luka 21:34–36).
“Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. Mfano wake ni k**a mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni” (Marko 13:33–37).
3. Utakatifu na Kujisafisha
Kanisa linajitayarisha kupitia utakatifu na kujitenga kwa ajili ya Mungu.
“Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu…..atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona k**a alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, k**a yeye alivyo mtakatifu. Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.
Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, k**a yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu” (1 Yohana 3:2–3).
“Fuataeni amani na watu wote, na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao” (Waebrania 12:14).
“Na tujisafishe na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukikamilisha utakatifu katika kumcha Mungu” (2 Wakorintho 7:1).
“K**a watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali k**a yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu” (1 Petro 1:14–16).
4. Kuvumilia na Kudumu Katika Imani katika Siku za Mwisho
Kanisa limeitwa kuvumilia majaribu na kubaki waaminifu katika Imani.
“Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. Kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka” (Mathayo 24:9-10,12–13).
“Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu” (Waebrania 10:35–39).
“Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia” (Yakobo 5:7–8).
“Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu” (Ufunuo 14:12).
5. Maombi na Maisha Katika Roho
Maandalizi katika siku za mwisho yanajumuisha maombi, kukesha kiroho, na kuishi katika Roho.
“Akaja akawakuta wamelala usingizi, akamwambia Petro, Je! Simoni, umelala? Hukuweza kukesha saa moja? Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu” (Marko 14:37-38).
“Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote” (Waefeso 6:18).
“Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu, jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele” (Yuda 1:20–21).
“Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. K**a ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake” (Warumi 13:11–14).
“Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho” (Wagalatia 5:16-17,25).
6. Kushik**ana na Kweli ya Neno la Mungu
Kanisa lazima libaki katika kweli ya Neno na kujiepusha na udanganyifu.
“Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, k**a yamkini, hata walio wateule. Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki” (Mathayo 24:11,23-26).
“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani” (1 Timotheo 4:1).
“Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao” (2 Timotheo 3:1–5,13-14).
“Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema” (Tito 2:11–14).
7. Kanisa Kujengwa Kuwa Makao Matakatifu ya Mungu
Maandalizi si ya mtu mmoja tu — mwili wote wa Kristo unajengwa pamoja kiroho.
“Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho” (Waefeso 2:19–22).
“Ninyi nanyi, k**a mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo” (1 Petro 2:5).
8. Kushinda na Kubaki Waaminifu na Wasafi hata mwisho
Yesu analiita Kanisa lake kushinda hadi mwisho.
“Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, k**a mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi” (Ufunuo 3:21).
“Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya” (Ufunuo 3:10–11).
“Tazama, naja k**a mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake” (Ufunuo 16:15).
Kanisa ni Bibi-arusi anayetakiwa kuwa tayari wakati wote, aliyejazwa Roho, aliyevikwa haki, anayekesha kwa ajili ya kuonekana kwa Bwana Yesu Kristo.
“Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu k**a kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake” (Ufunuo 22:11-14).
“Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo!” (Ufunuo 22:17).