06/24/2025
Kim YoungHoon, raia wa Korea Kusini na mbeba rekodi ya IQ (kipimo cha akili) cha juu zaidi duniani, amevunja ukimya na kugonga vichwa vya habari kwa ujumbe mzito wa kiimani. Kupitia ukurasa wake wa X, alitweet: "As the world's highest IQ record holder, I believe that Jesus Christ is God, the way and the truth and the life." (Nikiwa k**a mtu mwenye IQ kubwa zaidi duniani, naamini kwamba Yesu Kristo ni Mungu, njia, kweli na uzima). Kauli hii imezua mijadala mitandaoni, ikizingatiwa imetoka kwa mtu anayehesabiwa kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kiakili duniani.
IQ (Intelligence Quotient) ni kipimo kinachotathmini uwezo wa mtu kufikiri kimantiki (logic), kutatua matatizo, na kuelewa dhana tata kwa haraka. Young-Hoon alijulikana kimataifa baada ya kushinda mashindano ya World Memory Championships, akipata alama ya IQ ya 276 kiwango kisichowahi kufikiwa na binadamu mwingine katika historia.
Mafanikio yake yamekuwa yakihusishwa na uwezo wa kukumbuka, kuunganisha taarifa kwa kasi, na uwezo mpana wa mantiki (logic).
Japo wengi hufikiri kuwa maarifa ya kisayansi yanapingana na imani ya kiroho, Young-Hoon anaonesha tofauti. Kauli yake inaonesha kuwa hata kilele cha akili kinaweza kuungama mamlaka ya Yesu Kristo k**a Mungu.
Kwa kusema haya, si tu amehamasisha Wakristo duniani, bali pia amewachanganya wale waliowahi kufikiri kwamba imani ni ya watu "wanaoshindwa kufikiri sana".