Zanzibar Investment Promotion Authority

Zanzibar Investment Promotion Authority ZIPA is responsible for promotion and facilitation of investment in Zanzibar

Zanzibar Investment Promotion Authority is a semi autonomous government institution operating under the Zanzibar Investment Promotion and Protection Authority Act No. 10 of 2023.

Bodi ya Wakurugenzi, Mkurugenzi Mtendaji na Wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), wanampongez...
18/09/2026

Bodi ya Wakurugenzi, Mkurugenzi Mtendaji na Wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), wanampongeza Ndugu Hafsa Hassan Mbamba kwa kuteuliwa kuwa Naibu Mkurugeni Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA)

Tunamuombea mafanikio na hekima katika kutekeleza majukumu yake mapya, akiwa sehemu ya kuendelea kuimarisha utendaji katika Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).

Sometimes, the decision to invest begins with a sense of belonging.For this Mauritian investor, Zanzibar offered more th...
18/09/2026

Sometimes, the decision to invest begins with a sense of belonging.

For this Mauritian investor, Zanzibar offered more than an investment opportunity. The shared cultural connection, peaceful environment and warm welcome made Zanzibar feel like home from the very beginning.

This is the kind of connection that continues to shape Zanzibar as a destination for investors looking for opportunity, stability and a place they can call home.

16/09/2026

Zanzibar offers a range of investment incentives designed to reduce investment costs, improve the business environment and support sustainable growth across priority sectors.

Explore the opportunities and invest in Zanzibar.

TANZANIA NA JAPAN  KUIMARISHA USHIRIKIANO WA UWEKEZAJIUjumbe wa maafisa kutoka taasisi zinazosimamia uwekezaji nchini, i...
15/09/2026

TANZANIA NA JAPAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA UWEKEZAJI

Ujumbe wa maafisa kutoka taasisi zinazosimamia uwekezaji nchini, ikiwemo Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, umeendelea na ziara yake katika Mji wa Okinawa, Japan, kwa lengo la kujifunza uzoefu na kutambua fursa za ushirikiano wa uwekezaji kati ya Tanzania na Japan, hususan Zanzibar.

Ziara hiyo imeandaliwa kwa pamoja na ZIPA, TISEZA na Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, ikiwa na lengo la kuimarisha uhusiano kati ya taasisi za umma na sekta binafsi, pamoja na kuchunguza maeneo ya ushirikiano yanayoweza kuchangia maendeleo endelevu ya uchumi wa visiwa.

Katika ziara hiyo, ujumbe wa Tanzania umefanya mazungumzo na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) Okinawa, ambapo walijadili fursa za kujenga uwezo, uhamishaji wa maarifa na teknolojia, kuimarisha taasisi na kubadilishana uzoefu katika maendeleo ya uchumi wa visiwa.

Aidha, ujumbe huo ulitembelea Ryukyu Mura, eneo linaloonesha utamaduni na urithi wa jadi wa Okinawa, na kujifunza namna utamaduni, usanifu wa majengo, sanaa za mikono na urithi wa jamii vinavyoweza kutumika katika kukuza utalii na uchumi wa ndani.

Ziara hiyo imetoa maarifa muhimu kwa Tanzania, hususan Zanzibar, kuhusu namna ya kuunganisha utamaduni, urithi, ushiriki wa jamii na biashara za ndani katika uwekezaji wa utalii, huku ukihifadhi utambulisho wa maeneo husika.

Mbali na utalii, ziara hiyo inahusisha maeneo mengine ya kimkakati, yakiwemo uchumi wa buluu, uvuvi na ufugaji wa viumbe vya majini, elimu na utafiti, teknolojia na maendeleo endelevu ya uchumi wa visiwa.

Kupitia ziara hiyo, ZIPA, TISEZA na Ubalozi wa Tanzania nchini Japan wanaendelea kuwezesha ushirikiano wa Tanzania na Japan katika uwekezaji, uhamishaji wa teknolojia na maarifa, pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya wafanyabiashara na taasisi za nchi hizo mbili.

ZANZIBAR NA OKINAWA KUFUNGUA FURSA MPYA ZA USHIRIKIANO WA UWEKEZAJIZANZIBAR imeendelea kuimarisha fursa za ushirikiano w...
14/09/2026

ZANZIBAR NA OKINAWA KUFUNGUA FURSA MPYA ZA USHIRIKIANO WA UWEKEZAJI

ZANZIBAR imeendelea kuimarisha fursa za ushirikiano wa uwekezaji na Japan, kupitia ziara ya Ujumbe wa Uwekezaji wa Tanzania katika eneo la Okinawa, unaolenga kujifunza uzoefu wa maendeleo ya uchumi wa visiwa na kuangalia maeneo ya ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati.

Ushirikiano huo unalenga kufungua fursa katika maeneo ya utalii, uchumi wa buluu, uvuvi na ufugaji wa viumbe vya majini, elimu na utafiti, teknolojia pamoja na maendeleo endelevu ya visiwa.

Hayo yamezungumzwa katika ziara na mikutano iliyofanywa na Ujumbe wa Uwekezaji wa Tanzania nchini Japan katika siku ya kwanza ya programu ya Okinawa, ikiwemo ziara ya heshima katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan (MOFA) Okinawa, Chuo Kikuu cha Ryukyus na Ofisi Kuu ya Okinawa chini ya Ofisi ya Baraza la Mawaziri la Japan.

Katika mazungumzo na Chuo Kikuu cha Ryukyus, ujumbe huo ulipata fursa ya kujadili maeneo ya utafiti na teknolojia katika ufugaji wa viumbe vya majini, nishati jadidifu na mifumo jumuishi ya ufugaji wa viumbe vya majini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA amesema uzoefu wa Okinawa unatoa fursa muhimu kwa Zanzibar kujifunza mifumo inayoweza kutumika katika kuimarisha uwekezaji na maendeleo ya sekta za uchumi wa buluu, uvuvi, utalii na teknolojia.

Amesema ziara hiyo pia inalenga kuweka msingi wa ushirikiano wa vitendo katika kubadilishana maarifa, teknolojia na uzoefu, pamoja na kufungua fursa za ushirikiano kati ya taasisi za Zanzibar na Okinawa.

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kutembelea Kokusai Street, eneo la biashara na utalii katika Jiji la Naha, ambapo ujumbe ulipata fursa ya kuona namna shughuli za utalii, biashara za ndani na uchumi wa kisiwa zinavyounganishwa.

Ushirikiano unaoendelea kati ya Zanzibar na Okinawa unatarajiwa kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya pande hizo na kutoa fursa mpya za uwekezaji, ubadilishanaji wa teknolojia na maarifa, pamoja na maendeleo endelevu ya uchumi wa Zanzibar.

A strong investment environment is built on confidence, predictability and effective partnership between Government and ...
14/09/2026

A strong investment environment is built on confidence, predictability and effective partnership between Government and the private sector.

Creating the right conditions for investors means addressing challenges, improving the ease of doing business and ensuring that investment opportunities can translate into real projects and sustainable growth.

For Zanzibar, this remains an important part of strengthening the economy, creating jobs, supporting local businesses and expanding opportunities for communities.

ZANZIBAR, UAE KUIMARISHA USHIRIKIANO WA UWEKEZAJI KUPITIA MRADI WA NYUMBA ZA MAKAAZISERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar im...
11/09/2026

ZANZIBAR, UAE KUIMARISHA USHIRIKIANO WA UWEKEZAJI KUPITIA MRADI WA NYUMBA ZA MAKAAZI

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji, huku Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ukionesha nia ya kushiriki katika utekelezaji wa mradi wa Nyumba za Makaazi uliopo Kiboje Unguja.

Mradi huo ni miongoni mwa fursa za ushirikiano kati ya Zanzibar na UAE, unaotarajiwa kuchangia maendeleo ya kiuchumi, kuongeza shughuli za uwekezaji na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya pande hizo.

Hayo yameelezwa katika mazungumzo kati ya Konseli mkuu wa umoja wa falme za kiarabu Zanzibar Mhe. Saleh Al-Theeb Alhemeiri na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Ndg. Saleh Saad Mohamed, yaliyolenga kujadili maandalizi ya mradi huo na hatua zinazohitajika ili kuanza utekelezaji wake.

Katika mazungumzo hayo, pande hizo zimejadili upatikanaji wa huduma muhimu katika eneo la mradi, ikiwemo umeme, maji, mawasiliano na miundombinu mingine ya msingi.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Saleh Saad Mohamed amesema Serikali, kupitia taasisi zake, inaendelea kuhakikisha maeneo ya uwekezaji yanapata huduma muhimu ili kuwawezesha wawekezaji kutekeleza miradi yao kwa ufanisi.

Amesema hatua zinaendelea kutafuta suluhisho la nishati litakalokidhi mahitaji ya mradi huo, huku Serikali ikiendelea kuratibu upatikanaji wa huduma nyingine muhimu kwa ajili ya utekelezaji wake.

Kwa upande wake, Konseli mkuu wa umoja wa falme za kiarabu Zanzibar mhe. Saleh Al-Theeb Alhemeiri amesema mradi huo ni sehemu ya ushirikiano kati ya Zanzibar na UAE, akieleza kuwa nchi hiyo inaendelea kuangalia fursa za kushiriki katika miradi ya utalii, ukarimu na sekta nyingine za uwekezaji.

Amesema maandalizi ya mradi yanaendelea, huku hatua zinazofuata zikilenga kuhakikisha mahitaji muhimu yanapatikana ili mradi huo uweze kuanza kutekelezwa.

ZANZIBAR YAWEKA MAZINGIRA BORA KWA WAWEKEZAJISERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kuweka mazingira bora na ...
10/09/2026

ZANZIBAR YAWEKA MAZINGIRA BORA KWA WAWEKEZAJI

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itaendelea kuweka mazingira bora na rafiki kwa wawekezaji ili kuchochea ukuaji wa uchumi, kuongeza fursa za ajira na kuimarisha maendeleo ya Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Kaimu Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mudrick Ramadhan Soraga, aliyemwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Joud Hotel Zanzibar (Joud by Sea) Jambiani Mkoa Kusini Zanzibar.

Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi na wawekezaji katika kuendeleza uchumi wa Zanzibar, hususan kupitia uanzishaji wa miradi inayozalisha ajira, kuongeza mapato na kufungua fursa mbalimbali kwa wananchi.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji pamoja na taasisi zinazohusika na uwekezaji kuhakikisha changamoto zinazoweza kujitokeza zinafanyiwa kazi, huku akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mazingira salama na rafiki kwa mitaji ya ndani na nje.

Mapema, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Saleh Saad Mohamed, amesema hali ya uwekezaji Zanzibar inaendelea kuwa nzuri, ambapo hadi sasa mamlaka hiyo imesajili jumla ya miradi 654, ambayo imezalisha zaidi ya ajira 30,000 kwa wananchi.

Amesema ongezeko hilo la miradi linaonesha namna Zanzibar inavyoendelea kuwa kivutio kwa wawekezaji, huku ZIPA ikiendelea kurahisisha taratibu za uwekezaji na kutoa huduma zinazolenga kuwafanya wawekezaji kutekeleza miradi yao kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Waziri wa Kazi na Uwekezaji Zanzibar, Shariff Ali Shariff, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano, akieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na jitihada za Serikali katika kuweka mazingira yanayochochea uwekezaji na shughuli za kiuchumi.

10/09/2026

UFUNGUZI WA HOTELI YA JOUD BY THE SEA ZANZIBAR

SERIKALI YAAHIDI KUWALINDA WAWEKEZAJI WA NDANI ZANZIBARSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema itaendelea kuweka...
09/09/2026

SERIKALI YAAHIDI KUWALINDA WAWEKEZAJI WA NDANI ZANZIBAR

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuhakikisha wawekezaji wa ndani pamoja na mitaji yao wanalindwa, ili waweze kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wa Zanzibar.

Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa Wawekezaji wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Madinat Al Bahr, Mbweni Zanzibar, Waziri wa Kazi na Uwekezaji Zanzibar Mhe. Shariff Ali Shariff amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wawekezaji wa ndani katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi.

Amesema Serikali inatambua pia changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji hao na ipo tayari kushirikiana nao katika kuzitatua, kwa lengo la kuhakikisha shughuli zao za uwekezaji zinaendelea kukua na kutoa matokeo chanya kwa uchumi wa Zanzibar.

Waziri huyo amesisitiza kuwa Serikali ipo tayari kuwapa ulinzi wawekezaji wa ndani na mitaji yao, huku ikiendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Ndug. Saleh Saad Mohamed, amesema wawekezaji wa ndani wanalindwa kwa mujibu wa Sheria ya Uwekezaji Zanzibar Namba 10 ya mwaka 2023.

Amesema mkutano huo umeandaliwa na ZIPA kwa lengo la kuwakutanisha wawekezaji wa ndani na Serikali, ili kusikiliza changamoto zinazowakabili na kutafuta njia za pamoja za kuzitatua.

Saleh amesema kuanzia sasa, ZIPA itaendelea kukutana na wawekezaji wa ndani kila baada ya miezi mitatu, hatua ambayo itasaidia kufuatilia changamoto zao na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar, Hamad Hamad, amepongeza hatua ya ZIPA kuandaa mkutano huo huku akisema ni muhimu kwa Serikali na taasisi zake kuwa na utaratibu wa mara kwa mara wa kuwasikiliza wawekezaji na wafanyabiashara ili kuelewa changamoto zinazowakabili.

Amesema ushirikiano kati ya Serikali, ZIPA na wawekezaji wa ndani ni muhimu katika kujenga mazingira bora ya biashara, kuongeza uwekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Zanzibar.

Address

V656+XV Zanzibar
Zanzibar

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zanzibar Investment Promotion Authority posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share