Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar - Mowem

Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar - Mowem Ministry of Water, Energy and Minerals is responsible for Managing and Developing Water, Energy and Minerals issues in Zanzibar.

18/09/2026
16/09/2026
Mkurugenzi Idara ya Nishati na Madini Afanya Ziara ya Ghafla Kukagua Eneo la Uchimbaji wa KifusiMha. Said H. Mdungi Afua...
16/09/2026

Mkurugenzi Idara ya Nishati na Madini Afanya Ziara ya Ghafla Kukagua Eneo la Uchimbaji wa Kifusi

Mha. Said H. Mdungi Afuatilia Malalamiko ya Wananchi Kuhusu Athari za Uchimbaji wa Kifusi kwa Njia ya Miripuko

Mha. Said H. Mdungi, amefanya ziara ya ghafla ya kukagua eneo la uchimbaji wa kifusi lililolalamikiwa na wananchi wa maeneo ya vitongoji, kufuatia kikao cha wadau wa viwanda vinavyozalisha bidhaa za ujenzi, ikiwemo matofali, kokoto, vumbi na bidhaa nyingine zinazohusiana na ujenzi.

Ziara hiyo imefanyika baada ya wadau hao kuwasilisha malalamiko ya wananchi kuhusu shughuli za uchimbaji wa kifusi zinazofanyika kwa kutumia njia mbalimbali, ikiwemo miripuko, ambazo zimeelezwa kusababisha athari kwa afya na ustawi wa wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo.

Aidha, eneo hilo lipo karibu na bahari, jambo linaloongeza umuhimu wa kufanyika kwa tathmini ya kina kuhusu athari zinazoweza kujitokeza kwa mazingira ya bahari na maeneo yanayolizunguka eneo la uchimbaji.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi amepata fursa ya kujionea hali halisi ya eneo linalofanyiwa uchimbaji na kufuatilia changamoto zilizowasilishwa na wananchi kupitia wadau wa viwanda. Ziara hiyo inalenga kuwezesha Idara kupata uelewa wa kina kuhusu shughuli zinazoendelea na kuangalia hatua zinazofaa za kushughulikia malalamiko hayo.

Mha. Said H. Mdungi amesisitiza umuhimu wa shughuli za uchimbaji wa kifusi kufanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazohusika, huku afya na usalama wa wananchi pamoja na uhifadhi wa mazingira vikipewa kipaumbele.

Idara ya Nishati na Madini itaendelea kufuatilia masuala yanayohusu shughuli za uchimbaji na kusimamia utekelezaji wa taratibu zinazolenga kuhakikisha shughuli hizo zinafanyika kwa uwajibikaji na kwa kuzingatia maslahi ya jamii na mazingira.

WIZARA YAKUTANA NA WADAU WA VIWANDA VYA KUSAGIA KOKOTO (CRUSHERS) PEMBAWizara ya Maji, Nishati na Madini imeendelea kuch...
16/09/2026

WIZARA YAKUTANA NA WADAU WA VIWANDA VYA KUSAGIA KOKOTO (CRUSHERS) PEMBA

Wizara ya Maji, Nishati na Madini imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha usimamizi wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa za ujenzi, ikiwemo kokoto, vumbi.

Kufuatia agizo la Mhe. Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mkurugenzi wa Idara ya Nishati na Madini, Mha. Said H. Mdungi, amefanya kikao na wadau wa viwanda vya kusaga kokoto (crushers) pamoja na wazalishaji wa bidhaa za ujenzi kisiwani Pemba.

Kikao hicho kililenga kutoa maelekezo, kujadiliana changamoto na kuelekezana kuhusu utendaji kazi, hususan katika uzalishaji na matumizi ya malighafi kwa ajili ya bidhaa za ujenzi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mjumbe Ahmed K. Ahmed ameomba Serikali kuweka maeneo maalum kwa ajili ya uchukuaji wa kifusi katika Unguja na Pemba, hatua ambayo amesema inaweza kusaidia kurahisisha shughuli za uzalishaji na kuweka utaratibu mzuri wa matumizi ya malighafi hiyo.

Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za Wizara katika kuhakikisha shughuli za uzalishaji wa vifaa vya ujenzi zinafanyika kwa utaratibu, usalama na kuzingatia taratibu zilizowekwa na Serikali.

Address

Maisara
Zanzibar City
255

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar - Mowem posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar - Mowem:

Shortcuts

Share