17/09/2026
WANANCHI WAPATA ELIMU NA TAARIFA KUHUSU UCHUMI WA BULUU
Wananchi wanaotembelea banda la Sekta ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi katika Mkutano wa Kitaifa wa Uchumi wa Kijani (Green Summit) unaofanyika Mlimani City, Dar es Salaam, wamepata elimu na maelezo kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na rasilimali za bahari.
Elimu hiyo inaeleza namna Uchumi wa Buluu na Uvuvi endelevu unavyoweza kuchangia ajira, uwekezaji, kuongeza kipato na kukuza maendeleo endelevu.
Lengo kuu la Mkutano ni kujadili na kutafuta fursa za kiuchumi zinazotokana na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuimarisha mwelekeo wa Tanzania kuelekea uchumi wa kijani endelevu.
Katika muktadha huo, Sekta ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ina nafasi muhimu katika kuibua fursa na kuhakikisha rasilimali za bahari zinatumika kwa tija na kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.