Tume ya Maadili Zanzibar

Tume ya Maadili Zanzibar Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tume ya Maadili Zanzibar, Government Organization, Wete.

18/06/2020
WATENDAJI wa Tume wametakiwa kuendelea kudhibiti na kuhifadhi siri za Viongozi wa Umma ili kuendelea kuijengea sifa na h...
17/03/2020

WATENDAJI wa Tume wametakiwa kuendelea kudhibiti na kuhifadhi siri za Viongozi wa Umma ili kuendelea kuijengea sifa na heshima Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi, Sheria, Utawala Bora na Idara Maalum za SMZ ambae pia ni Makamo Mwenyekiti wa k**ati hiyo wakati walipokutana na Viongozi na Wafanya kazi wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika kuangalia utendaji na changamoto zinazoikabili Tume hiyo.
Amesema kua siri za Viongozi wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zipo Ofisi ya Tume hivyo endapo wafanyakazi hawatakuwa waadilifu katika majukumu yao wanaweza kuivunjia heshima Tume pamoja na wao wenyewe.
Aidha wajumbe hao wameitaka Tume ya Maadili kuendelea na kazi ya utoaji elimu kwa njia tofauti kwani bado kuna baadhi ya viongozi hadi sasa wameshindwa kutekeleza wajibu wao wa kujaza Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni.
Wamesema kuwa baadhi ya viongozi k**a wahasibu wapo baadhi yao katika taasisi wanajaza wote lakini kuna baadhi ya ofisi nyengine bado hawajazi.
Vile vile wameutaka uongozi wa Tume kuharakisha suala la kuongeza wafanyakazi wa Tume katika ofisi ya Pemba ili kurahisisha utoaji huduma kwa Viongozi walioko Pemba.
Mapema akiwasilisha ripoti ya utekelezaji Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, Ndugu Asma Jidawy amesema kuwa katika utekelezaji wa robo ya tatu 2019/20 Tume ya Maadili imepokea Fomu za Viongozi wa Umma thelathini (30) kati ya hizo Fomu tatu (3) za Viongozi wapya na ishirini na saba (27) ni viongozi waliochelewa kurejesha Fomu.
Hata hivyo amesema kuwa tayari utaratibu wa kuwachambua Viongozi na kubaini Kiongozi ambae hajarejesha Fomu na aliyeleta nje ya muda umeshakamilika na hatua zitaanza kuchukuliwa karibuni kwa mujibu wa Sheria ya Maadili nambari 4 ya Mwaka 2015 inavyoelekeza.
Vile vile alieleza kuwa kwa mujibu wa matakwa ya Sheria tayari Tume imeshachapisha majina ya Viongozi waliorejesha Fomu katika Gazeti Rasmi la Serikali kupitia Tangazo nambari 6 la mwaka 2020.
Katibu, Jidawy aliongezea kuwa mbali na changamoto za upatikanaji wa fedha Tume imeendelea kutekeleza kazi zake ikiwemo utoaji elimu kupitia njia mbali mbali licha ya upatikanaji wa fedha kuwa wa asilimia chache. Miongoni mwa kazi hizo za utoaji elimu ni utayarishaji vipindi kupitia kupitia ZBC, ushiriki wa maadhimisho ya siku ya Sheria yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Zanzibar na utoaji elimu kwa watumishi mbali mbali wa Serikali vikiwemo vikosi.
Kikao hicho ni muendelezo wa ziara za Kamati za Baraza la Wawakilishi katika kukutana na taasisi mbali mbali na kujadili changamoto zinazozikumba taasisi hizo ili kuziwasilisha Barazani.

21/12/2019
18/10/2019

Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma yawapa darsa ya maadili watumishi Pemba October 18, 2019 Editor-in-Chief Kitaifa, Kona ya Sheria 0   IMEANDIKWA NA AMINA KHAMIS MAELEZO, PEMBA WAFANYAKAZI wa Wizara ya Ardhi, maji, nyumba na nishati Pemba, wametakiwa kujiepusha kutumia miavuli ya viongozi na bada...

18/10/2019

Picha: Tume ya Maadili yakutana na wananchi wa Vitongoji Chakechake October 18, 2019 Editor-in-Chief Kitaifa, Kona ya Sheria 0 AFISA Mdhamini wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Pemba, Hanuna Ibrahim Massoud, akizungumza na wananchi wa shehia ya Vitongoji wilaya ya Chakechake, wakati maafisa wa t...

Mwenyekiti Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, Nd. Assaa Ahmad Rashid akisoma hotuba kwa wajumbe wa Mabaraza y...
21/03/2019

Mwenyekiti Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar, Nd. Assaa Ahmad Rashid akisoma hotuba kwa wajumbe wa Mabaraza ya Vijana Mkoa Kaskazini Pemba juu ya Nafasi ya Vijana katika Kudumisha Maadili kwenye ukumbi wa Jamhuri, Wete.

Ni siku ya pili leo Tume ya maadili ya Viongozi wa Umma bado inaendelea kutoa elimu katika banda lake kwenye viwanja vya...
01/02/2019

Ni siku ya pili leo Tume ya maadili ya Viongozi wa Umma bado inaendelea kutoa elimu katika banda lake kwenye viwanja vya maonesho Gombani Mpya. Tunapongeza wanachi wameweza kufika kwa wingi katika banda la Tume k**a inavyoonekana hapo.

Ikiwa ni miongoni mwa jukumu ililopewa la kutoa elimu ya maadili kwa umma, bado Tume inaendelea na kazi yake ya kutoa el...
01/02/2019

Ikiwa ni miongoni mwa jukumu ililopewa la kutoa elimu ya maadili kwa umma, bado Tume inaendelea na kazi yake ya kutoa elimu katika mabanda ya maonesho ya siku ya sheria yanayoendelea hapo viwanja vya nje ya Gombani Mpya. Wananchi wote wanakaribishwa ili kuelewa wajibu wao.

14/08/2018

USIKOSE KUTUFUATILIA KILA SIKU ZA JUMANNE KUANZIA SAA 11:00 ZA JIONI KUPITIA ZBC NA SIKU ZA JUMATATU KUANZIA SAA 3:30 KUPITIA SPICE FM REDIO ILI KUPATA ELIMU JUU YA UMUHIMU WA MAADILI YA VIONGOZI.

Jamii imetakiwa kiwafichua viongozi wanaokiuka maadili..............VIJANA wameaswa kushiriki kikamilifu katika kujenga ...
30/07/2018

Jamii imetakiwa kiwafichua viongozi wanaokiuka maadili
..............
VIJANA wameaswa kushiriki kikamilifu katika kujenga nchi kwa kuibua matendo ya uvunjwaji wa maadili yanayofanywa na baadhi ya Viongozi wa Umma nchini.
Mwenyekiti wa Tume ya Maadili, Mhe: Asaa Ahmad Rashid amewaeleza Vijana wa Mabaraza ya Vijana Wilaya za Magharibi na Mjini wakati akifungua mkutano wa siku moja uliojadili nafasi ya Vijana katika kuimarisha maadili kwenye ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul Wakil Kikwajuni mjini Unguja.
Mhe: Rashid aliitaja nafasi ya vijana kuwa ni kutoa elimu ya umuhimu wa maadili katika jamii, kuripoti taarifa za ukiukwaji wa maadili na kushirikiana na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika kutekeleza majukumu yake.
“Maendeleo ya nchi yanategemea uimara wa vijana na ndio maana tunasema kijana ni nguvu kazi ya taifa. Jamii ikiwa na vijana dhaifu wasioweza kusimamia rasilimali za nchi yao, wasioweza kuwa na uchungu na nchi yao ni wazi kuwa taifa litakuwa katika hatari”. Alifahamisha.
Amewataka vijana kuzitumia nafasi zao vizuri kwa kuhakikisha maadili yanalindwa na kutekelezwa kila mahali ikiwemo katika ngazi ya familia, jamii, taasisi za elimu, taasisi za dini, sehemu za kazi na kila sehemu ambazo wanakutana.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa viongozi pamoja na watumishi wa umma wanatekeleza majukumu ambayo jamii ina uhitaji kwao hivyo ni lazima wazingatie maslahi ya umma na si vyenginezo katika kutekeleza majukumu yao.
Amefahamisha kuwa jamii yoyote ile haiwezi kupiga hatua za kimaendeleo bila ya kuwa na maadili mazuri ambayo huhitaji watu wa kuyaendeleza ili kizazi na kizazi kiweze kurithi.
Akizitaja baadhi ya faida zitakazoweza kupatikana endapo vijana hao na jamii watasimamia maadili ipasavyo kuwa ni kuimarika kwa maendeleo ya nchi, kuzidisha amani, upendo na utulivu, kuondoka kwa dhulma nchini, kuzidisha hali ya umoja na mshik**ano, kujenga uaminifu na uadilifu, kuondoka kwa rushwa na uhujumu uchumi katika jamii.
Kwa upande mwengine, akiyazungumzia matendo ya udhalilishaji nchini, watumishi kutoa siri za wanaowahudumia k**a vile madaktari kutoa siri za wagonjwa, kuongezeka kwa vitendo vya rushwa na kuongezeka kwa madawa ya kulevya ni athari kubwa zilizopo nchini kutokana na kuacha kufuata maadili.
Aidha, Mwenyekiti wa Tume hiyo akiyazungumzia baadhi ya mafanikio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar alisema kuwa kuanzishwa kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar ni jitihada kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya saba inayoongozwa na Rais Dkt. Ali Mohamed Shein katika jitihada za kuimarisha utawala bora nchini.
Naye Katibu wa Tume hiyo Ndugu Kubingwa Mashaka Simba alisema kuwa Tume hiyo itaendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia makundi tofauti kwani ni moja katika majukumu ya Tume hiyo kisheria.
Amefahamisha kuwa Tume hiyo itachukua hatua kwa kiongozi yeyeto yule endapo itabainika kuwa kiongozi huyo amekiuka miiko na taratibu za uongozi.
Katika mkutano huo mada mbili ziliwasilishwa ikiwemo Sheria ya Maadili na Umuhimu Wake na Jukumu la Mabaraza ya Vijana Katika Kukuza Maadili ambapo vijana waliweza kupata nafasi ya kuchangia mada hizo.
Wakitoa michango yao mbele ya Tume, vijana hao wameitaka Tume hiyo izidi kuendelea kutoa elimu hiyo hususan kwa viongozi wa umma kwani wamesema kuwa kumekuwepo kwa matumizi mabaya ya vyombo vya Serikali vinavyotumika kwa maslahi binafsi.
Aidha, wameishauri Tume kushughulikia viongozi ambao hawawajali wananchi wao kwa kuwatolea lugha zisizofaa wananchi wao.
Mkutano huo uliwashirikisha wajumbe wa mabaraza ya vijana wa Wilaya za Magharibi, Mjini na wajumbe wa Baraza la Vijana Taifa ambapo elimu hiyo itaendelea kutolewa kwa mabaraza yote ya Vijana wa Wilaya za Unguja na Pemba.

Address

Wete

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tume ya Maadili Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share