30/10/2024
MCHONGO NI AFYA YAKO, ZINGATIA UNACHOKULA.
Mkuu wa Wilaya Ya Urambo Dkt.Khamis Athumani Mkanachi amesema Watu wa Urambo kubadilisha mfumo wa Chakula ili kuimarisha afya zao.
Dkt.Khamis Mkanachi amesema hayo wakati akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Lishe iliyofanyika katika viwanja vya Kata ya Ussoke Tarafa ya Ussoke leo tarehe 30.10.2024.
DC. Mkanachi amesema vyakula vinavyohitajika kwa afya zetu vinalimwa katika maeneo yetuz hivyo tutumie vyakul hivyo kuimarisha afya zetu.
Hata hivyo Mhe. Mkuu wa Wilaya amesisitiza kwa kusema ulaji unaohitajika unatufanya tufanye kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo.
Aidha ameendelea kuwaelekeza wadau wa Lishe kuongeza nguvu kwani Takwimu zinaonyesha bado hali siyo nzuri kwa watu wengi ambao wamepimwa hawana lishe bora.
Baada ya kuhitimisha pamoja na maelekezo aliyoyatoa Mhe.Dkt Mkanachi aliongoza zoezi la kuchangia Damu Salama akiwa pamoja na Diwani wa Kata ya Ussoke Wakifuatiwa na baadhi ya Watumishi na Wanannchi.
Zoezi la uchangiaji limekuja baada ya Mhe. Dkt Khamis kutembelea banda la uchangiaji Damu Salama nakuelezwa kuwa hali ya uchangiaji hairidhishi na uhitaji wa Damu salama ni mkubwa sana.
Amesisitiza kwamba liwe zoezi endelevu kwani kumekuwa na uhitaji kwenye maeneo ya huduma za afya hasa kwa Wanawake wanaojifungua, watu wanaopata ajali na wengine kupungukiwa damu hivyo basi Watu wajitokeze kwa wingi kuchangia Damu Salama.
"Mchongo ni Afya , Zingatia unachokula"