20/11/2025
*SIRI YA USHINDI* by Niceman Jay
Leo imedhihiri, tumeonesha ufundi
Pamoja na Umahiri, tumeibuka washindi,
Ubingwa kwetu desturi, washindani Hawapendi,
*Umoja nguvu yetu,Ndiyo Siri ya ushindi.*
Ngoja niwataje, majemedari wa Ufundi,
Urassa namwachaje, alongoza kundi
Jovini ashindwaje, kwaya ilo maridadi
*Umoja nguvu yetu, ndiyo siri ya Ushindi.*
Chambiri kakomoa, Jesika hakuwa nyuma
Zana wamechukua, usafi na kujituma,
Netiboli twachechemea, tumejifunza na ngoma,
*Umoja nguvu yetu, ndiyo siri ya ushindi.*
Kulwa kwenye ngoma, Baguma netiboli,
Mwakani hamtokwama, mturudishe kwenye reli,
Malambo kajipima, kaicheza futiboli,
*Umoja nguvu yetu, ndiyo siri ya ushindi.*
Sijamtaja Zakaria, alowajaza mawazo
Hakika wamejua, Tarime wanauwezo,
Kikosi kiliamua, kujua wanamichezo,
*Umoja nguvu yetu, ndiyo siri ya ushindi.*
Siwasahau wachezaji, hakika wamejitoa,
Wameonesha weledi, mioyoni waliridhia,
Ya*okuwa na IDADI, makombe wakayazoa,
*Umoja nguvu yetu, ndiyo siri ya ushindi.*
Hongereni wababe wao, mekomesha hakika,
Mepiga hadi kwao, Kanda ziwa tushaishika,
Tunawafuata wa mwambao, uwezo utadhihirika.
*Umoja nguvu yetu, ndiyo siri ya ushindi.*
Bila Laki wala Paundi,
Tutawapa uchungu,
Si figisu wala bundi, ni vipaji vya Mungu,
Ushindi huu si wa Kipindi, tutayakata mawingu.
*Umoja nguvu yetu, ndiyo Siri ya ushindi.*
Tamati naweka hapa,Juu zaidi Sipandi,
Nasema huku Naapa,Ajae kwetu Hashindi,
Siri yetu tushawapa, jiandaeni kwa Ndondi,
*Umoja nguvu yetu, ndiyo siri ya ushindi.*