Ikulu habari Zanzibar

Ikulu habari Zanzibar Karibu kwenye ukurasa rasmi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Jummah Mubarak
29/05/2026

Jummah Mubarak

27/05/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akizungumza leo, tarehe 27 Mei 2026, wakati alipohutubia Baraza la Eid lililofanyika katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi, Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

27/05/2026
RAIS DKT. MWINYI: SMZ INAENDELEA KUCHUKUA HATUA KUKABILIANA NA GHARAMA ZA MAISHARais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza...
27/05/2026

RAIS DKT. MWINYI: SMZ INAENDELEA KUCHUKUA HATUA KUKABILIANA NA GHARAMA ZA MAISHA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali zote mbili za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) zitaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na athari za kiuchumi zinazosababishwa na mgogoro wa vita vya Mashariki ya Kati, hususan kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo leo, tarehe 27 Mei 2026, alipohutubia Baraza la Eid lililofanyika katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi, Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema hali inayoendelea Mashariki ya Kati inaleta changamoto kubwa za kiuchumi duniani na kusababisha ugumu wa maisha kwa wananchi, hivyo Serikali itaendelea kuchukua hatua mahsusi za kupunguza athari hizo kwa wananchi.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewaomba wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika juhudi zake za kukabiliana na hali hiyo pamoja na kuhimiza kuombewa amani na maridhiano duniani kwa ajili ya ustawi wa watu wote.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza Wizara ya Nchi, Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora kupitia Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana pamoja na Umoja wa Taasisi Zinazosafirisha Mahujaji Zanzibar (UTAHIZA) kwa ushirikiano wao mzuri katika kufanikisha huduma za usafirishaji wa mahujaji wa Zanzibar.

Amesema ibada ya Hijja inafundisha umuhimu wa umoja, mshik**ano na usawa wa wanadamu wote mbele ya Mwenyezi Mungu bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

Sambamba na hayo, Rais Dkt. Mwinyi ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuzifanyia kazi changamoto zinazowasilishwa na taasisi zinazoshughulikia safari za Hijja ili kuweka mazingira bora yatakayowezesha waumini wengi zaidi kutimiza Nguzo ya Tano ya Uislamu.

Vilevile, ameishukuru Serikali ya Saudi Arabia pamoja na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa katika kuhakikisha mahujaji wa Tanzania wanapata huduma na mazingira mazuri wakati wa utekelezaji wa ibada ya Hijja.

Mapema baada ya kuwasili katika Baraza hilo, Rais Dkt. Mwinyi alipokea salamu na kukagua gwaride la heshima lililoand

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
27/05/2026

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

RAIS DKT. MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU PEMBA KATIKA SALA YA EID EL-HAJJRais wa Zanzibar na Mwenyekiti ...
27/05/2026

RAIS DKT. MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU PEMBA KATIKA SALA YA EID EL-HAJJ

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu, Pemba katika Sala ya Eid El-Hajj iliyosaliwa leo, tarehe 27 Mei 2026, katika Msikiti wa Ole Kianga, Mkoa wa Kusini Pemba.

Mapema baada ya sala hiyo, Alhaj Dkt. Mwinyi alifika Ikulu Ndogo ya Pagali katika eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya kuchinja mnyama wa (Udh-hiya), ikiwa ni sehemu ya ibada ya Eid, pamoja na kutoa mkono wa Eid kwa Masheikh wa Mkoa huo, k**a ilivyo Sunna katika kusherehekea Sikukuu ya Eid El-Hajj.

Waumini wa dini ya Kiislamu duniani kote wanasherehekea Sikukuu ya Eid El-Adha kufuatia kukamilika kwa Ibada ya Hijja, ambayo ni Nguzo ya Tano ya Uislamu.

Address

Zanzibar
Stone Town

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ikulu habari Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share