Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar, Government Organization, Kilimani, Zanzibar, Stone Town.

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar inawakaribisha wananchi wote, watafiti, wanafunzi na wadau mbalimbali katika k...
08/06/2026

Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar inawakaribisha wananchi wote, watafiti, wanafunzi na wadau mbalimbali katika kilele cha siku ya nyaraka duniani pamoja na kutembelea Maonesho ya Nyaraka za Kiislamu na Kiarabu kwa Jamii ya Zanzibar, yatakayofanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Nyaraka Duniani 2026.

Maonesho haya yanalenga kuonesha mchango wa nyaraka za kihistoria katika kuhifadhi utamaduni, urithi, maarifa na historia ya Zanzibar kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

πŸŽ–οΈ Mgeni Rasmi:
Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

πŸ“… Tarehe: 09 Juni 2026
⏰ Muda: Saa 2:00 Asubuhi
πŸ“ Mahali: Makumbusho ya Amani, Mnazi Mmoja

Karibu ujifunze, ujionee na kuthamini hazina ya nyaraka zinazobeba historia na utambulisho wa Zanzibar.

Katika kuadhimisha Juma la Nyaraka , Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imeandaamaonesho madogo ya nyaraka za kis...
08/06/2026

Katika kuadhimisha Juma la Nyaraka , Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar imeandaa
maonesho madogo ya nyaraka za kisheria ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuadhimisha Juma la Nyaraka Duniani 2026,

Akizungumza katika maonesho hayo, Mgeni Rasmi, Prof. Mohammed Hafidh, amesema kuwa Taasisi imefanya jambo muhimu kwa kuandaa maonesho hayo yenye lengo la kuitangaza Taasisi kwa jamii na kutoa uelewa kuhusu nyaraka na kumbukumbu muhimu zinazohifadhiwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aidha, Prof. Mohammed aliwahimiza watumishi wa Taasisi kutumia fursa za masomo na mafunzo mbalimbali ili kujiendeleza kitaaluma na kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika usimamizi na uhifadhi wa nyaraka kwa njia za kisasa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi Ndg Khatib Suleiman Khatib alisema kuwa maonesho hayo yameandaliwa kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza nyaraka muhimu kwa matumizi ya sasa na ya baadaye, sambamba na kuhamasisha utamaduni wa kuhifadhi kumbukumbu kwa usahihi na usalama.

Maonesho hayo yamewapa fursa wageni na wadau mbalimbali kujionea baadhi ya nyaraka za kisheria zenye thamani ya kihistoria




πŸ“šβš–οΈ MAONESHO YA NYARAKA ZA SHERIA Katika kuadhimisha Juma la Nyaraka 2026, Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar ina...
07/06/2026

πŸ“šβš–οΈ MAONESHO YA NYARAKA ZA SHERIA

Katika kuadhimisha Juma la Nyaraka 2026, Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar inawakaribisha wote kutembelea Maonesho ya Nyaraka za Sheria.

Maonesho haya yatafunguliwa rasmi na Prof. Mohamed Hafidh Khalfan, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya PDB, ambaye atakuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

πŸ—“οΈ 08 Juni 2026
⏰ 02:00 Asubuhi – 08:30 Mchana
πŸ“ Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar

07/06/2026
πŸ† FAINALI YA NYARAKA DAY CUP 2026 πŸ†Timu ya PBZ Bank   imeibuka bingwa wa Nyaraka Day Cup 2026 baada ya kuifunga Tawakal ...
07/06/2026

πŸ† FAINALI YA NYARAKA DAY CUP 2026 πŸ†

Timu ya PBZ Bank imeibuka bingwa wa Nyaraka Day Cup 2026 baada ya kuifunga Tawakal Hospital mabao 3–1 katika mchezo wa fainali uliochezwa katika Viwanja vya Mao Zedong.

Washindi walikabidhiwa kombe na fedha taslimu, huku washiriki wote wakipatiwa zawadi za ushiriki. Aidha, mbio za watoto zilifanyika na washindi wake walizawadiwa zawadi mbalimbali.

Mgeni rasmi alikuwa Mhe. Ali Abdulghulam Hussen, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

07/06/2026

Nani ataibuka mshindi ....

Baada ya michezo miwili ya kusisimua iliyochezwa leo katika Viwanja vya Maisara:⚽ Tawakal 3 - 1 IPA ⚽ PBZ 2 - 0 NyarakaπŸ†...
06/06/2026

Baada ya michezo miwili ya kusisimua iliyochezwa leo katika Viwanja vya Maisara:

⚽ Tawakal 3 - 1 IPA

⚽ PBZ 2 - 0 Nyaraka

πŸ† Tawakal na PBZ sasa zitamenyana kesho katika mchezo wa fainali kuwania kombe la Nyaraka Day Cup 2026.

Nani ataibuka bingwa? Karibuni tushuhudie pambano hili la mwisho la kusaka ubingwa.

Karibuni woteeeeeee........
06/06/2026

Karibuni woteeeeeee........

Nani ataibuka mshindi ...kesho katika viwanja vya maozedongKaribuni woteeeee
06/06/2026

Nani ataibuka mshindi ...kesho katika viwanja vya maozedong

Karibuni woteeeee

Address

Kilimani, Zanzibar
Stone Town

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share