14/07/2017
Anaandika Julius Mabula,
Alifukunyua na kulifafanusha bunge la Afrika lisilofahamika kwa raia wengi wa wa bara la afrika.
Bunge la Afrika (PAN AFRICAN PARLIAMENT/AFRICA PARLIAMENT)
Bunge hili lilianzishwa Tar 18/3/2004
Ni sehemu ya umoja wa nchi huru za kiafrika( AU) na chimbuko Lake ni kwenye huu umoja wa AU.
Linaendeshea vikao vyake katika mji wa Midland nchini afrika kusini.
Lengo la bunge hili ni kuibua na kujadili kero, changamoto, matatizo na masuala mbalimbali ya kiuchumi,kijamii na kisiasa ya bara zima la afrika kwa maslahi Ya waafrika wote ikiwa ni pamoja na kuyatatua na kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayolikumba bara la afrika.
Rais wa Bunge hili na ndiye kiongozi mkuu ni Mh Roger Nkodo Dang,aliingia madarakani mwaka 2015 ni raia wa nchi Ya
Cameroon.
Muundo wa utawala wa bunge hili ni:
1,Rais
2,Kamati 10 za sekta mbalimbali za shughuli za kiuchumj, kisiasa na kijamii barani afrika.
3,Mabaraza 3 ya bunge la afrika.
Baraza la kwanza linaitwa(bureau of pan African parliament)
Hili ni baraza la viongozi tu wa bunge hili na lina uongozi pia k**a ifuatavyo:
1,Rais wa bureau of Pan African parliament ni Mh Bethel Ninaemeka Amadi Raia wa Nigeria na anawakilisha kwenye bunge hili ukanda wote wa afrika ya Magharibi.
2,Makamu wa kwanza wa Rais wa Bureau of pan African parliament ni mh Roger Nkodo Dang ambaye pia ndiye Rais wa bunge zima, ni raia wa nchi Ya Cameroon na kwenye bunge hili anawakilisha ukanda wote wa afrika Ya kati
3,Makamu wa pili wa Rais wa bureau of Pan African parliament ni Mh Moustafa El-Gendy Raia wa nchi Ya misri(Egypt) katika bunge hili anawakilisha ukanda wote wa afrika Ya kaskazini.
4,Makamu wa tatu wa Rais wa bureau of pan African parliament ni mh Loide L. Kasingo ni raia wa nchi Ya Namibia,katika bunge hili anawakilisha ukanda wote ulioko kusini mwa bara la afrika.
5.Makamu wa nne wa Rais wa bureau of Pan African parliament ni mh Safia Elmi Diibril ni raia wa nchi ya Djibouti, katika bunge hili anawakilisha ukanda wote wa afrika Ya mashariki.
Baraza la pili linaitwa, prenary of pan African parliament.
Hiki Ndiyo chombo cha maamuzi katika bunge hili,
Humu ndimo walimo wabunge wa bunge hili,
Bunge hili lina wabunge 235 na wanachaguliwa na mabunge 47 ya nchi huru za afrika wanachama wa AU kati ya nchi 54 za bara la afrika.
Mabunge 47 ya nchi huru za kiafrika kila bunge huchagua wabunge 5 na kati Ya hawa 5 mmoja sharti awe mwanamke,mabunge haya huwachagua hawa wabunge kwa kufuata misingi ya kisiasa Ya kila bunge kulingana na wingi wa wabunge wa chama kipi ama pinzani au tawala katika nchi husika.
Baraza la tatu linaitwa, Secretariat of Pan African parliament
Hiki ni chombo kinachoratibu shughuli za kila siku za bunge hili,huratibu agenda za vikao,chaguzi na ratiba zote za bunge hili.
Kiongozi mkuu wa sekretarieti hii huitwa karani na anaitwa mh Zwelethu lukhangiso Mighty Madasa ni raia wa Taifa la afrika kusini.
Naibu karani wa kwanza ni mh Helen Bwange Dingani ni raia wa Zimbabwe, anahusika na shughuli zote za utawala za kila siku za bunge hili.
Naibu karani wa pili wa sekretarieti hii ni mh Morad Boularad ni raia wa Algeria,anahusika na masuala yote Ya utawala wa kimataifa na fedha katika bunge hili.
Ni bunge zuri lenye historia ndefu hapa barani afrika kwa ustawi wa nchi za kiafrika na jamii zote za kiafrika.
Na Julius Nkwabi Mabula.
[email protected]
Mwandishi na mchambuzi wa makala hii.
Chambo Ushetu Kahama shinyanga Tanzania.
Jamii ya wafugaji na wakulima.