Tanzania Agricultural and Environmental Conservation Association-TAECA

  • Home
  • Tanzania
  • Mwanza
  • Tanzania Agricultural and Environmental Conservation Association-TAECA

Tanzania Agricultural and Environmental Conservation Association-TAECA TAECA ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyoundwa na vijana wenye maono ya kubadilisha maisha yao na ya jamii ya Kitanzania kupitia kilimo na Ufugaji

22/11/2023

BONYEZA LINK HAPA CHINI KUJIUNGA NA CHANNEL

17/04/2022

TUNAKUTAKIA KHERI YA SIKUKUU YA PASAKA

08/10/2020

UHAMILISHAJI WA NGURUWE (PIG ARTIFICIAL INSEMINATION) ni njia ya kisasa ya kuboresha wanyama wako (nguruwe) kwa kuwapandisha na mbegu za kisasa zaidi kwa kutumia teknolojia ya mirija.

Hii ni njia mbadala na rahisi kwa wewe (mfugaji) kupandisha wanyama wako bila kuhitaji kumiliki madume (BOARS) shambani kwako. Unaweza kutumia njia hii kupandisha wanyama wengi kwa wakati mmoja bila uwepo wa dume la kupanda.

Zaidi ya hapo, inakupa wewe mfugaji uwezo wa kuchagua mbegu za dume unayetaka kulingana na mahitaji ya mradi wako.

Njia hii imekuwa inatumika kwa wanyama k**a “NGOMBE, MBUZI, KONDOO NA MBWA” na imeleta mafanikio makubwa sana hapa nchini na hata nchi zilizoendelea.

*FAIDA ZA UHAMILISHAJI*

1. URAHISI
Uhamilishaji unakurahisishia wewe mfugaji kupandisha wanyama wengi kwa mara moja bila kuhitaji madume wengi. Mchakato huu hutumia muda mfupi na nguvu chache ukilingianisha na matumizi ya dume la mbegu amabayo huhitaji matumizi ya muda na nguvu nyingi.

2. UPATIKANAJI WA MBEGU BORA.
Mfugaji anaweza kupata mbegu bora muda wowote pale atakapohitaji.

3. UWEZO WA KUCHAGUA MBEGU
Matumizi ya uhamilishaji unakupa nafasi wewe mfugaji kuchagua mbegu bora na ambayo unahitaji kwa malengo husika. Mara kwa mara, mfugaji huhitaji kujaribu mbegu tofauti tofauti na hii huwa ngumu au ya gharama k**a utakuwa unamiliki madume yote. Mbegu za mirija zinakupa uwezo wewe mfugaji kuwa na uchaguzi wa mbegu za aina mbalimbali.

4. GHARAMA NAFUU
Uhamilishaji ni njia nafuu sana kifedha kwa wafugaji wadogo wadogo wanaotaka kuanza kufuga kisasa na kukuza mradi wao wa nguruwe.
Mchakato huu unapunguza uhitaji wa kununua na kumiliki dume la mbegu la kisasa ambao huuzwa kwa bei kubwa, ukizingatia kwamba dume huyo hutumika mara chache sana.

5. MAGONJWA
Pale unapoingiza nguruwe mgeni (iwe dume au jike) kwenye shamba lako, unahatarisha sana wanyama wako kwani mnyama huyo huweza kuja na magonjwa ambayo yanaweza kuambukiza shamba lako zima. Matumizi ya uhamilishaji huepusha uwezekano wa kupatwa na magonjwa hayo yanayotoka shamba moja kwenda lingine.

K**a una maswali ya ziada, unaweza wasiliana basi kupitia:
[email protected]
+255-755-361-904

12/09/2020
27/08/2020
04/08/2020

UFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA:
1. ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa hautegemei mvua, uzalishaji hufanyika wakati wote ; kiangazi na mvua
2. Bei ya maziwa , mara nyingi haishuki hata k**a kutakuwa na maziwa mengi kuliko mahitaji
3. Mahitaji ya maziwa yanazidi kuongezeka kila siku. Ulaji wa bidhaa za maziwa pia unazidi kuongezeka
4. Kulinganisha bidhaa zingine, soko la maziwa ni rahisi kupatikana. Kwa kifupi gharama za kuuza maziwa ni ndogo kulinganisha na bidhaa zingine
5. Ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ndiyo biashara pekee, kuna uhakika wa kupata kipato kila mwezi

Kwa mipango ya Biashara ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa Whatsapp : +255621106923

Address

MWANZA
Mwanza
4001

Telephone

+255629209000

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Agricultural and Environmental Conservation Association-TAECA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanzania Agricultural and Environmental Conservation Association-TAECA:

Share