Ofisi Ya Mkuu Wa Mkoa Morogoro

Ofisi Ya Mkuu Wa Mkoa Morogoro Ukurasa wetu unaelezea taarifa mbalimbali zinazohusu Mkoa wa Morogoro Mkoa wa Morogoro ni Mkoa wa pili kwa ukubwa nchini ukitanguliwa na Mkoa wa Tabora.

Mkoa una eneo la kilometa za mraba 73,039. Eneo hili ni sawa na asilimia 7.7 ya eneo lote la Tanzania Bara, kati ya eneo hili Km2 2,240 ni eneo la maji. Mkoa umepakana na Mikoa ya Pwani na Lindi kwa upande wa Mashariki, Manyara na Tanga upande wa Kaskazini na kwa upande wa Magharibi umepakana na Mikoa ya Dodoma na Iringa. Upande wa Kusini unapakana na Mkoa wa Ruvuma. Hali ya Hewa

Mkoa hupata mvua

mara mbili kwa mwaka. Mvua za vuli hunyesha kuanzia mwezi Oktoba hadi katikati ya mwezi Januari, na mvua za masika hunyesha katikati ya mwezi Februari na kuishia mwezi Mei mwishoni. Kiwango cha mvua ni kati ya milimita 600 katika sehemu za tambarare na milimita 1,200 katika miinuko. Hata hivyo, zipo sehemu zilizo na ukame ambazo hupata mvua chini ya milimita 600 kwa mwaka. Sehemu hizo ni pamoja na Tarafa za Gairo katika wilaya ya Gairo, Mamboya katika Wilaya ya Kilosa na Tarafa ya Ngerengere katika Wilaya ya Morogoro. Utawala

Mkoa wa Morogoro kiutawala umegawanyika katika Wilaya sita ambazo ni Wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilosa, Kilombero, Ulanga na Gairo. Kufuatana na Muundo wa Serikali za Mitaa Mkoa una Halmashauri sita za Wilaya na Halmashauri ya Manispaa moja. Halmashauri za Wilaya ni pamoja na Kilosa, Gairo, Kilombero, Morogoro, Ulanga, Mvomero na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. Mkoa unayo majimbo ya Uchaguzi 10, Kata 212, Vijiji 673, Mitaa 295, vitongoji 3,451

Idadi ya watu

Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 idadi ya kaya za Mkoa wa Morogoro ni 489,688 zenye watu 2,218,492 ambapo kati yao wanawake ni 1, 125,190 na wanaume ni 1,093,302. Wastani wa idadi ya watu katika Kaya ni 4.5.
- See more at: http://morogoro.go.tz

Address

P. O BOX 650
Morogoro

Opening Hours

Monday 07:45 - 15:30
Tuesday 07:45 - 15:30
Wednesday 07:45 - 15:30
Thursday 07:45 - 15:30
Friday 07:45 - 15:30

Telephone

+255232604237

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi Ya Mkuu Wa Mkoa Morogoro posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ofisi Ya Mkuu Wa Mkoa Morogoro:

Share