The Civic United Front

The Civic United Front To be completed

13/04/2015

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF- Chama Cha Wananchi)
Kurugenzi ya Haki za Binadamu Habari na Uenezi
Office of the Secretary General
P.O. BOX 3637, Zanzibar, Tanzania
E-mail: [email protected]
Weblog:http:hakinaumma.worldpress.com

Date: 13/04/2015


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Waheshimiwa Wakurugenzi, Viongozi, Watendaji wa Chama, Wahariri, Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbali mbali, Ndugu Wananchi, Mabibi na Mabwana……Assalaamu Alaykum!

Waheshimiwa!

Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezu Mungu kwa kutujaalia tukakutana wakati huu na katika kikao hiki muhimu.

Waheshimiwa! Hizi ni zama ambazo Nchi yetu ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, inahitaji mafanikio na maendeleo ya kweli katika ngazi zote, kupitia misingi muhimu ya demokrasia na utawala bora, chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo sasa imeanza kuangaza matumaini mema ya ukombozi thabiti wa Wazanzibari wote.

Waheshimiwa! Katika kuendeleza na kufanikisha azma hiyo ni lazima yawepo mashirikiano ya wananchi wote bila kutanguliza utashi binafsi, pamoja na kuzingatia siasa za kistaarabu, demokrasia, utawala bora na umoja wa kitaifa, na pia kuweka mbele maslahi ya Nchi yetu.

Waheshimiwa! Sote ni mashahidi wa namna umma wa Wazanzibari ulivyokwisha kujiunga na wimbi kubwa, zito, la kihistoria la kisiasa katika safari ndefu sasa ya kupigania na kurejesha mamlaka kamili ya Zanzibar, ambapo tunasema hilo halizuiliki, kwani si rahisi kuushinda wakati.

Waheshimiwa! Hiyo ni safari na hayo ni mapambano ambayo k**a ilivyo kawaida hayakosi wasaliti, ingawa pia hatimaye hakuna mapambano ya dhati yasiyokuwa na mafanikio; nataka nikuhakikishieni kwamba na sisi hatutarudi nyuma.

Historia inathibitisha kuwepo wasaliti wa Zanzibar na Wasaliti wa Mamlaka kamili ya Zanzibar, na pia wasaliti wa maendeleo na matumaini ya watu wa visiwa hivi vya Unguja na Pemba; tena usaliti huo ulikuwepo zamani na awamu zilizotangulia, na sasa dhahiri unajionyesha kupitia hata baadhi ya watendaji wa ngazi za juu za Serikali, ambao kimsingi wamedhihirisha kutokuitakia mema Nchi hii na watu wake; tunasema hao ni vibaraka na huko ni kushindwa kwa kiasi kikubwa.

Waheshimiwa! Usaliti na azma mbaya ni mambo yasiyoweza kujificha, ni mithili ya moto ulianzia kufuka moshi na hatimaye ukawaka na kuleta madhara kwa wahusika wenyewe na kisha kwa umma ambao katu sasa umeshaamua kuachana na kila asiyeitakia mema Zanzibar.

Historia inaashiria hivyo Waheshimiwa, tangu pale kabla na baada ya Mapinduzi ya Tarehe 12 Januari 1964; kupitia Awamu zote za Uongozi; Awamu ya Pili ya Mzee wetu Aboud Jumbe; mpaka kufikia katika Awamu ya Sita ya Uongozi chini ya Raisi Mstaafu Mheshimiwa Dr. Amani Abeid Karume, ambapo Umma wa Wazanzibari uliamua kwa Sauti kubwa kuyachagua Maridhiano ya Kisiasa na hatimaye Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Yote hayo Waheshimiwa ni ishara kwamba Wazanzibari walikwishachoshwa na usaliti wa maendeleo na usaliti wa mamlaka kamili; na hivyo basi pia wameelekeza kwa ujasiri kabisa matumaini yao ya maendeleo ya kweli na utaifa wao katika misingi ya umoja wa kitaifa, na asilan hawaonyeshi dalili za kurudi nyuma, na wala hawatakubali kudanganywa tena.

Mnaelewa waheshimiwa Chama cha Wananchi, CUF, kilikotokea, na kinakoenda; namna kilivvyohimili mawimbi mazito ya hila, hujuma, idhilali, vitisho na kila aina ya mateso na udhalilishaji, ambayo matunda yake ya subira na uvumilivu na ya kujivunia yanaonekana sasa ambapo umma umeamua kuwekeza matumaini yao ya dhati kabisa kwa Chama hiki kisichoyumba na kilichothibiti katika kuwajali na kuwatetea wananchi wote kwa hali na mali bila ubaguzi huku kikitanguliza maslahi ya Nchi.

Waheshimiwa! Moja ya matunda ya uvumilivu na hikma za Viongozi wa Chama cha Wananchi, CUF, chini ya Majemedari Maalim Seif Sharif Hamad, Profesa Ibrahim Lipumba na wengine wote ni kuiona Zanzibar ikibaki salama, licha ya fitna na misukosuko, iliyogharimu hata maisha ya watu wasiokuwa na hatia; na Inshaallah itaendelea kubaki salama, hata mbele ya maadui wasioitakia mema Nchi hii.

Mnakumbuka vyema Waheshimiwa namna Wananchi walivyouwawa kikatili na Jeshi la Polisi katika Mauaji ya Tarehe 26 na 27 Januari 2001, Unguja na Pemba; namna Viongozi na Wananchi walivyosulubiwa kila mara kwa vipigo na namna walivyoweza kubambikiziwa kesi na kila aina ya hujuma; namna Nchi hii ilivyotikisika na hatimaye ikazalisha wakimbizi katika Kambi za Shimoni na Dadaab, Nchini Kenya.

Waheshimiwa! Lazima muelewe kwamba si rahisi kuirejesha historia na mambo yaliyokwishapita; lakini pia ni lazima kujifunza kutokana nayo, hivyo mwanadamu si vyema kufumbia macho dhulma iliyokwishatendeka kwa kisingizio tu kwamba watu wamejaribu kusahau; Na huo ndio pia wito wetu k**a wasemavyo wahenga, “mwenye kovu usidhanie kapoa”.

Waheshimiwa! Zama za ubabaishaji, ubadhirifu, ufisadi wa kupindukia, ubaguzi, vitisho na kila aina ya hujuma dhidi ya wananchi, Viongozi wapenzi wa wananchi, watendaji waaminifu na waadilifu, na watetezi wote wa umma na watetezi wa Zanzibar, zimepitwa na wakati, siyo hapa tu bali duniani kote; huu ni wakati wa kuishi kwa kuchunga haki, demokrasia, utawala bora, sheria, umakini, na uwazi usioleta shaka.

Mmeshuhudia Waheshimiwa katika mfululizo wa matukio ya hivi karibuni, na zaidi dhidi ya Chama cha CUF, Viongozi wa CUF, Wapenzi na Wafuasi pamoja na Wananchi wasiokuwa na hatia, na pia dhidi ya Ofisi za CUF; na ndiyo maana tukaamua kuyakumbusha hayo.

Chama cha Wananchi, CUF, umma wote, na kila waungwana, hawakupendezewa hata kidogo na kitendo cha hivi karibuni cha kuteketezwa vibaya na moto, Ofisi ya Jimbo la Dimani, Wilaya ya Magharibi Unguja, Usiku wa kuamkia tarehe 24 Machi, 2015 majira ya saa 8.30, iliyogharimu zaidi ya Shilingi 150 Milioni.

Umma wote umestushwa na kulaani kwa nguvu zote kitendo cha kupigwa na kuhujumiwa wananchi waliokuwa wakirejea katika Mkutano wa Hadhara, uliofanyika Jumapili Tarehe 29 Machi, 2015, Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja, ambapo zaidi ya watu 30 walijeruhiwa vibaya.

Pamoja na yote, ya kushangaza, ya kuudhi na ya kusikitisha sana ni matokeo ya Jana Jumapili, Tarehe 12 April, 2015 katika Jimbo la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja; katika hali isiyotarajiwa kabisa, wakati huu tunaohitaji siasa za kistaarabu kwa maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari wote, kuona vurugu zilizoandaliwa kwa makusudi ili kuparaganya na kutiribua hali ya utengamano wa kisiasa Nchini.

Waheshimiwa! Kilichotokea hiyo jana ni hali iliyoandaliwa kwa makusudi kwani dalili ziliashiria tangu mapema za kushawishi na kulazimisha au pia kuuhujumu Mkutano Halali kabisa wa Chama chetu uliopangwa kufanyika katika Jimbo hilo, katika Shehia ya Kipandoni, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CUF, ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Maalim Seif Sharif Hamad.

Waheshimiwa! Waandaaji, wahamasishaji, wafadhili na watekelezaji wa hujuma zote hizo, wakitumia mamlaka waliyonayo serikalini, na pia kwa kushirikiana na vyombo vya dola, wanajulikana na umma umeshathibitisha kupitia mfululizo wa matukio hayo azma mbaya waliyonayo katika kukihujumu Chama cha CUF, kuwahujumu wananchi wasiokuwa na hatia, kuihujumu Zanzibar, na kuirejesha tena Nchi hii katika zama za siasa chafu za chuki, ubaguzi, mizozo na migogoro.

Chama cha Wananchi, CUF, kinalaani kwa nguvu zote mwenendo huo na kinaitaka Serikali kuwa makini hasa wakati huu ambao wananchi wanashuhudia mwelekeo mwema wa kisiasa na matumaini ya maendeleo chini ya maridhiano na hali ya umoja wa kitaifa.

Aidha, Chama cha Wananchi, CUF, kinatoa wito kwa Jeshi la Polisi kutekeleza wajibu wake kwa misingi ya haki, sheria na uadilifu; na kuepuka kutumiwa kisiasa na kuwacha ukereketwa, huku likielewa kwamba kwa mujibu wa Sheria No.5 ya Mwaka 1992 ya Vyama vya Siasa, halina mamlaka yoyote ya kuzuia Mkutano Halali wa Chama cha Siasa Kilichosajiliwa.

Pongezi za dhati kwa wanachama, wapenzi na wananchi, pamoja na wakaazi wa Kitope, kwa uungwana, hikma na ustahamilivu wao, waliouonyesha ambao uliodhihirisha ukomavu wa hali ya juu kisiasa wa Wana-CUF, licha ya hujuma, uchokozi na usumbufu wa makusudi uliofanywa na Jeshi la Polisi. Jeshi la Pilisi linaonekana wazi kwamba limebeba mbeleko Chama cha CCM kutoka katika kina kirefu cha Maji.

Jeshi la Polisi linatoa vibali na kuvifuta hii inadhihirisha wazi kwamba Jeshi hilo halina uhuru wa kufanya kazi zake bila kuingiliwa na viongozi wa Chama cha CCM.

Wameshindwa kufanya kazi yao ya Ulinzi wa Raia sasa wananyima haki na uhuru wa watu ambao kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar wanaouhuru wa kutembea Zanzibar bila ya vizuizi vyovyote.

Mpango wa Jeshi la Polisi kuzuia Wazanzibari kutembea wanapotaka na siku wanayoitaka ni kukiuka Katiba Halali ya Zanzibar.

Chama cha Wananchi, CUF, kinatoa pole kwa waandishi wa habari, kutokana na usumbufu na udhalilishaji wa Jeshi la Polisi uliolenga kuzuia utekelezaji wa majukumu yao ya kazi hasa pale walipotaka kushiriki ziara ya ndani ya Mhe shimiwa Katibu Mkuu katika Uzinduzi wa Matawi Mapya na Uwekaji wa Mawe ya Msingi wa Matawi na Baraza za CUF katika Jimbo hilo.

Na mwisho kabisa, Chama cha Wananchi, CUF, kinatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu, wasikivu, na wastahamilivu wakizingatia umuhimu wa amani, utulivu na mshik**ano, mambo ambayo hayapatikani pasi na kutenda haki, huku wakielewa kwamba mwisho wa fitna zote ni fedheha.

HAKI SAWA KWA WOTE

…………………………….
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Zanzibar

Headquaters: P.O.Box 3637, Zanzibar, Tanzania. Tel.: 024 22 37446 Fax.: 024 22 37445
Main Office: PO. Box 10979, Dar-es-Salaam, Tanzania. Tel. 022 861009 Fax.: 022 861010

MAKAMO WA KWANZA WA RAISI MAALIM SEIF SHARIFU HAMAD, AKIMBEBA MTOTO ALIPOKUA MAKUNDUCHI KABLA YA MKUTANO ULIOFANYIKA TAR...
31/03/2015

MAKAMO WA KWANZA WA RAISI MAALIM SEIF SHARIFU HAMAD, AKIMBEBA MTOTO ALIPOKUA MAKUNDUCHI KABLA YA MKUTANO ULIOFANYIKA TAREHE 29/3/2015

30/03/2015
30/03/2015
30/03/2015

To be completed

30/03/2015

HUJUMA ILIYOFANYWA NA CCM ZIDI YA FAFUWASI WA CUF-CHAMA KINACHOKUBALIKA ZAIDI

30/03/2015

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama cha Wananchi)
OFFICE OF SECRETARY GENERAL
Office of the Secretary General
P.O. BOX 3637, Zanzibar, Tanzania

30/03/2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Itakumbukwa kwamba jana, tarehe 29/03/2015 The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi) kilifanya ziara na mkutano wa hadhara Wilaya ya Kusini, jimbo la Makunduchi katika uwanja wa Jamhuri.

Wakihutubia Mkutano huo Viongozi wa CUF walizungumzia mwenendo na kuibuka kwa vitendo vya hujuma dhidi ya wafuasi wa CUF na majengo ya Ofisi za Chama hicho katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mfano, wakati akihutubia katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu, Mheshimiwa Nassor Ahmed Mazrui alitahadharisha kuwa kuna taarifa za uhakika zilizoletwa uwanjani hapo kuwa kuna mpango ulioandaliwa wa kuwadhuru kwa kuwashambulia wananchi waliohudhuria mkutano huo na kwa hivyo kulitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha ulinzi katika maeneo yote ili kudhibiti na kuzima mpango huo.

Mbali na tahadhari hizo zilizotolewa mapema, Jeshi la Polisi lilishindwa kutoa mashirikiano kwa kuwapatia wananchi hao ulinzi hali iliyosababisha msafara wa uliokuwa ukitoka katika mkutano huo kuvamiwa, na wafuasi wa CUF kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.

Kufuatia matukio hayo, CUF-Chama Cha wananchi:
• Kinalitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kwa kuanza na wale wote waliotajwa kushiriki na kufadhili hujuma na uhuni dhidi ya wananchi waliokuwa wakitumia haki yao ya Kikatiba ya kushiriki katika shughuli za kisiasa kwa mujibu wa sheria za nchi.

• Kinalitaka Jeshi la Polisi kuwafuatlia na kuwachukulia hatua vijana wote waliohusika kuwavamia, kuwapiga na kuwajeruhi wananchi hao wasio na hatia yoyote.

• Kinalitaka Jeshi la Polisi kutodharau hujuma zinazofanywa dhidi ya CUF na kwa hivyo kufuatilia kwa kina na kubaini njama za upangaji wa mipango ya hujuma kwa kuwachukulia hatua za kisheria bila ya kujali cheo cha yeyote miongoni mwao wale wote wanaochochea na kushabikia dhulma za aina hii kwa wananchi.

• Kinalitaka Jeshi la Polisi kukomesha utaratibu wa CCM wa kukusanya vijana (JANJAWEED) kutoka maeneo mbalimbali ya nchi katika makambi na kuwapa mafunzo ya utumiaji wa silaha na kuwatia mori wa kupiga, kujeruhi na kuuwa kila asiyekubaliana na sera na matakwa ya CCM.

IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO NA UMMA

……………………………………..
SALIM A. BIMANI

MKURUGENZI WA H/U/M/UMMA

HUJUMA ILIYOFANYWA NA CCM ZIDI YA FAFUWASI WA CUF-CHAMA KINACHOKUBALIKA ZAIDI
30/03/2015

HUJUMA ILIYOFANYWA NA CCM ZIDI YA FAFUWASI WA CUF-CHAMA KINACHOKUBALIKA ZAIDI

CUF yanyakua kiti cha Zitto, PACNa Mwandishi Wetu, DodomaWAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, wamemchagua M...
23/03/2015

CUF yanyakua kiti cha Zitto, PAC
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WAJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, wamemchagua Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mwidau (CUF) kuwa mwenyekiti wa k**ati hiyo.
Katika uchaguzi uliofanyika jana mjini hapa, Mwidau alichaguliwa na wajumbe wa PAC kwa kupata kura 15 dhidi ya mpinzani wake, Lucy Owenya (Chadema) aliyeambulia kura mbili.
Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo, Mwidau alisema atafanya kazi iliyoachwa na Zitto Kabwe wakati akiiongoza k**ati hiyo kwa kuzingatia masilahi ya nchi na siyo watu binafsi.
“Moto ni uleule ambao umeachwa na mwenyekiti mtangulizi wangu, Zitto Kabwe, na tutafanya kazi pale alipoishia maana nikiwa mjumbe wa k**ati hii tulifanya kazi k**a ndugu wa familia moja.

“Zitto na Deo Filikunjombe waliweka misingi imara katika PAC na hilo tutaendelea nalo na tutafanya kazi k**a jicho la Bunge kwa Serikali hasa katika kusimamia na kulinda rasilimali za Watanzania ila tunawaomba waendelee kutuamini,” alisema Mwidau.
Alisema ingawa imebaki takribani miezi minne Bunge kuvunjwa, k**ati yake itaendelea na ratiba yake ya mwaka iliyokuwa imepangwa.

“Kama mwenyekiti kazi yangu kubwa ni kuiongoza k**ati kwa mujibu wa taratibu, sisi tunakagua hesabu za serikali kuu na mashrika ya umma.

Tunaangalia namna serikali inavyofanya kazi yake, tuna mpango wa kazi, ratiba ya mwaka mzima tutaendelea nayo,” alisema.
Alisema pia kuwa k**ati itaendelea na msimamo wa uwajibikaji na uwazi ambao ulikuwa ukisimamiwa na Zitto.

Akizungumzia kuchaguliwa kwa Mwidau kuongoza Kamati hiyo, Mwenyekiti wa zamani wa PAC, Zitto Kabwe alimpongeza kwa kushinda nafasi hiyo akisema ana imani ataendelea kusimamia mifumo ya uwajibikaji.

“Nampongeza kwa dhati dada yangu kwa imani aliyopewa na wajumbe wenzake wa PAC. Nimefanya kazi na Amina tangu mwaka 2010 tulipokuwa Kamati ya POAC na nina imani kwa ushirikiano mkubwa wa Makamu Mwenyekiti Deo Filikunjombe wataendeleza kazi tuliyoianza ya kujenga mfumo madhubuti wa uwajibikaji nchini kwetu,” alisema Zitto.

Chanzo MTANZANIA

Address

Mnazi Mmoja

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Civic United Front posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to The Civic United Front:

Share