Jumuiya ya Wazazi Iringa Vijijini

Jumuiya ya Wazazi Iringa Vijijini Elimu,Malezi na Mazingira

HEKARI 100 ZATENGWA KATA YA MGAMA, IRINGA VIJIJINI KUWEZESHA UJENZI WA HOSPITALI KUPITIA UMOJA WA WAZAZI, JUMUIYA YA CHA...
04/06/2023

HEKARI 100 ZATENGWA KATA YA MGAMA, IRINGA VIJIJINI KUWEZESHA UJENZI WA HOSPITALI KUPITIA UMOJA WA WAZAZI, JUMUIYA YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Uchungu wa MWANA?
Jana Umoja wa Wazazi Iringa Vijijini tumefanikiwa kutembelewa na Katibu Mkuu wa Wazazi Ndugu Gilbert Kalima akiwa amefika kwa dhumuni la kutembelea eneo la HEKARI Mia Moja lililotengwa Ili KUWEZESHA UJENZI WA HOSPITALI katika eneo hilo

Mwenyekiti wa Halmashauri Iringa Vijijini akiwa ameongozana na Diwani na Viongozi wengine wa Kijiji alisema kuwa litakua jambo jema Sana k**a Mradi huo utafanikiwa na kuishukuru Jumuiya ya Wazazi kwa kuwa tayari kujenga Hospital katika Eneo hilo

Katibu mkuu aliwashukuru Viongozi wote wa Kata ya MGAMA na Viongozi wote wa Halmashauri ya Iringa Vijijini kwa kuwa tayari kulitoa Eneo hilo.

Katibu Mkuu wa Wazazi aliwahakikishia Viongozi na Wananchi kuwa Suala la Afya ni Moja ya Eneo Muhimu ambalo Jumuiya ya Wazazi inajihusisha nalo

Na itakua ni Heshima kubwa Kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa

Uongozi wa Wazazi Iringa Vijijini unawashukuru Viongozi wote kwa kuja na kuungana pamoja nasi katika Kumpokea Katibu mkuu na Kwenda kuliona eneo hilo

Mungu Ibariki Jumuiya ya Wazazi Iringa Vijijini

Mungu Kibariki Chama Cha Mapinduzi

By
Maryline Mamuya
Katibu Elimu, Malezi na Mazingira Iringa Vijijini.

Address

Iringa

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jumuiya ya Wazazi Iringa Vijijini posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Jumuiya ya Wazazi Iringa Vijijini:

Share