03/06/2026
WILAYA YA BAHI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MIRADI YA MAENDELEO
Viongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 wakiongozwa na Ndugu Wazo Michael Mwang'onda wameipongeza Wilaya ya Bahi kwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kutekeleza maelekezo mbalimbali ya Serikali kwa ufanisi
Akizungumza wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru wilayani humo , kiongozi wa mbio hizo amesema kuwa Wilaya ya Bahi imekuwa ya kwanza miongoni mwa Wilaya zote walizozitembelea kwa kufanikiwa kusajili vikundi vingi vya wananchi, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan hatua ambayo imeonesha dhamira ya halmashauri katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo
Viongozi hao pia wamepongeza usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo, wakisema miradi hiyo imekamilishwa kwa ubora na kuwahimiza wananchi kuendelea kushiriki katika miradi ya maendeleo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Sambamba na hayo, viongozi wa Mwenge wa Uhuru wamesisitiza umuhimu wa kulinda amani na utulivu wa nchi, wakieleza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo endelevu na ustawi wa wananchi
Katika hatua nyingine, wameipongeza Wilaya ya Bahi kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama kwa vitendo na wamewataka wananchi kuacha ukataji holela wa miti unaochangia uharibifu wa mazingira na badala yake kutumia nishati safi na kuacha matumizi ya mifuko ya lambo ili kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo
Vilevile, viongozi hao wamepongeza jitihada za halmashauri katika kusajili vikundi vingi vya wananchi na kufikia na kuvuka malengo yaliyowekwa na serikali Wamesema mafanikio hayo yameufurahisha Mwenge wa Uhuru na Serikali kwa ujumla, kwani yanaonesha utekelezaji mzuri wa maelekezo ya Serikali na dhamira ya kuwainua wananchi kiuchumi
Mwenge wa uhuru umetembelea, na kukagua Miradi 7 katika wilaya ya Bahi na kukabidhiwa na Kaimu mkuu wa wilaya ya Bahi Dkt. Sophia Kizigo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Tarehe 3 Juni 2026 katika wilaya ya Kondoa dc.