Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia This is an official FACEBOOK PAGE for Ministry of Education, Science and Technology in Tanzania

KisomoKwaManufaaYaWatu     Simiyu2026
19/09/2026

KisomoKwaManufaaYaWatu





Simiyu2026

PROF. MUSHI: IPOSA IWE DARAJA LA KUUNGANISHA VIJANA NA ELIMU, AJIRA Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tek...
19/09/2026

PROF. MUSHI: IPOSA IWE DARAJA LA KUUNGANISHA VIJANA NA ELIMU, AJIRA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, amezitaka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Halmashauri na wadau mbalimbali kuendelea kuimarisha utekelezaji wa Programu ya Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu (IPOSA) ili iwe daraja la kuwaunganisha vijana na elimu zaidi, ajira na maisha bora.

Prof. Mushi ametoa kauli hiyo, Septemba 18, 2026, mkoani Tanga, akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Programu ya IPOSA awamu ya Pili (IPOSA II).

Amesema IPOSA II ni utekelezaji dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya elimu bila kujali umri, mahali alipo au changamoto alizokutana nazo.

Ameelekeza TEWW kuimarisha ushirikiano na VETA, SIDO, FDC na sekta binafsi kwa kuunganisha mafunzo ya IPOSA na mafunzo kwa vitendo, ushauri wa kitaalamu, ziara za kujifunza pamoja na fursa za ajira.

Prof. Mushi amesema mafanikio yaliyopatikana katika mikoa sita inayotekeleza IPOSA II kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini kupitia KOICA yanapaswa kuwa msingi wa kuimarisha utekelezaji wa programu hiyo katika mikoa mingine kwa kuzingatia ubora wa mafunzo, upatikanaji wa wawezeshaji wenye sifa na usimamizi madhubuti.

Amesema Serikali inatambua mchango wa Serikali ya Korea Kusini kupitia KOICA katika kuimarisha utekelezaji wa IPOSA na amepongeza wadau mbalimbali walioshiriki katika programu hiyo,

Naye Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Balozi Eunje Ahn amesema Serikali ya Korea Kusini kupitia KOICA imetoa takribani dola za Marekani milioni sita kwa ajili ya utekelezaji wa programu hiyo katika mikoa sita ya Pwani, Shinyanga, Simiyu, Lindi, Tanga na Manyara.

Amesema kupitia mradi huo, jumla ya vituo 31 vimejengwa, vikiwemo vituo vitatu vya mfano vilivyopo Shinyanga, Manyara na Tanga, pamoja na kituo kimoja maalumu kilichopo Tanga pamoja na kutoa vifaa na kujengea uwezo wawezeshaji.


     Kisomo2026Simiyu2026
18/09/2026






Kisomo2026
Simiyu2026

Safari ya kujifunza huanza kwa msingi imara. Tushiriki kikamilifu kuwawezesha watoto kukuza umahiri wa Kusoma, Kuandika ...
18/09/2026

Safari ya kujifunza huanza kwa msingi imara. Tushiriki kikamilifu kuwawezesha watoto kukuza umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu na kufikia uwezo wao.

Jukumu letu ni kushiriki kikamilifu katika safari ya ujifunzaji wa watoto, tukiwasaidia kujenga umahiri wa Kusoma, Kuand...
17/09/2026

Jukumu letu ni kushiriki kikamilifu katika safari ya ujifunzaji wa watoto, tukiwasaidia kujenga umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.


17/09/2026

Tanzania inaendele kujipambanua katika kuhakikisha inakuwa na rasilimali watu yenye maarifa na ujuzi katika maeneo ya Sayansi na Teknolojia. Moja ya eneo muhimu ni kuimarisha na kuwezesha tafiti zinazofanywa na Watanzania kwa maendeleo ya Taifa letu.

Usikose Fuatilia episode ya kwanza, ya Sauti ya Sayansi, Teknolojia na Elimu Podcast kupitia YuoTube ya Wizara Elimu TZ TV kufahamu zaidi kuhusu utafiti uliofanywa na Prof. Ndakidemi na kumpa ushindi mnono.



✨ COMING SOON! ✨
16/09/2026

✨ COMING SOON! ✨

Kila mtoto ana uwezo wa kujifunza, kung’ara na kufikia mafanikio.
16/09/2026

Kila mtoto ana uwezo wa kujifunza, kung’ara na kufikia mafanikio.


16/09/2026

MAFUNZO YA AKILI UNDE YAONGEZA TIJA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU



Kila mwalimu ana nafasi ya kujenga msingi wa mafanikio ya mtoto katika ujifunzaji.
15/09/2026

Kila mwalimu ana nafasi ya kujenga msingi wa mafanikio ya mtoto katika ujifunzaji.


Address

Mji Wa Serikali Mtumba/Mtaa Wa Afya S. L. P 10
Dodoma
40479DODOMA

Opening Hours

Monday 02:00 - 15:30
Tuesday 02:00 - 21:30
Wednesday 02:00 - 21:30
Thursday 02:00 - 21:30
Friday 02:00 - 09:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia:

Shortcuts

Share