Ministry of Water

Ministry of  Water Karibu: Maji ni hitaji la msingi na haki kwa binadamu wote. Tafadhali yathamini, kuongeza matumizi y

The Ministry of Water is mandated to formulate and monitor implementation of policies on rural and urban water services; water resources development; water infrastructure development; water sources protection and conservation; sanitation improvement; water laboratories; river basins development and management; water quality and pollution control; drilling and dam construction and rain water harvest; Water Institute Affairs; performance improvement and development of human resources; extra ministerial departments, parastatal organizations, agencies, programmes and projects. VISION

To have reliable and sustainable water resources that adequately meet the social and economic development needs of the country presently and in future. MISSION
To ensure that water resources are developed, managed and utilized sustainably to foster social and economic development in Tanzania.

VISIMA VYA BUNGE VYAKAGULIWA Wizara ya Maji imekagua visima vinavyotoa huduma ya maji katika Bunge la Tanzania, jijini D...
08/06/2026

VISIMA VYA BUNGE VYAKAGULIWA

Wizara ya Maji imekagua visima vinavyotoa huduma ya maji katika Bunge la Tanzania, jijini Dodoma.

Kazi hiyo imehusisha upimaji wa kina cha maji, ubora wa maji pamoja na uwezo wa pampu kuvuta wingi wa maji kubaini uwezo wa kisima katika kuzalisha maji.

Hizo ni hatua muhimu katika kuhakikisha huduma ya maji ni endelevu na inayikidhi mahitaji.

VISIMA BUNGENI VYAKAGULIWAWizara ya Maji imefanya kazi ya kukagua visima vya maji Bungeni jijini Dodoma. Kazi hiyo imehu...
08/06/2026

VISIMA BUNGENI VYAKAGULIWA

Wizara ya Maji imefanya kazi ya kukagua visima vya maji Bungeni jijini Dodoma.


Kazi hiyo imehusu kupima kina cha maji, uchunguzi wa ubora wa maji , pamoja na ukaguzi wa miundombinu ya visima kutathmini ubora wake.

Pia, majaribio ya pampu kusukuma maji yamefanyika kubaini uwezo wa kuzalisha maji.

08/06/2026

VISIMA VYA BUNGE VYAKAGULIWA

Wizara ya Maji imekagua visima vinavyotoa huduma ya maji katika Bunge la Tanzania, jijini Dodoma.

Kazi hiyo imehusisha upimaji wa kina cha maji, ubora wa maji pamoja na uwezo wa pampu kuvuta wingi wa maji kubaini uwezo wa kisima katika kuzalisha maji.

Hizo ni hatua muhimu katika kuhakikisha huduma ya maji ni endelevu na inayikidhi mahitaji.

NMB WATEMBELEA WIZARA YA MAJI Ujumbe wa  Benki ya NMB Makao Makuu Dodoma umetembelea Wizara ya Maji kuonesha benki hiyo ...
05/06/2026

NMB WATEMBELEA WIZARA YA MAJI

Ujumbe wa Benki ya NMB Makao Makuu Dodoma umetembelea Wizara ya Maji kuonesha benki hiyo k**a mshirika wa kuimarisha Sekta ya Maji

Ujumbe huo umeongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Serikali Bi
Vicky Bishubo na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesso (Mb) ambapo umeeleza jitihada zinazochukuliwa na NMB k**a mshirika wa kimkakati katika kuendeleza sekta ya maji hapa nchini.

Wazara wa Maji Mhe. Aweso amesema Sekta ya Maji itaendelea kushirikiana vyema na Benki ya NMB na kuhakikisha mipango na mazungumzo yote ya kimkakati yanafanikiwa na kuahidi kutoa ushirikiano wa dhati.

Wizara ya Maji Yatakiwa Kutekeleza Miradi Kwa Kuzingatia Uhifadhi wa Ardhi OevuMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa ...
05/06/2026

Wizara ya Maji Yatakiwa Kutekeleza Miradi Kwa Kuzingatia Uhifadhi wa Ardhi Oevu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi ameitaka Wizara ya Maji kutekeleza miradi ya maji kwa kulinda ardhi oevu nchini.

Ametoa agizo hilo katika Siku ya Mazingira iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Mhe. Dkt. Nchimbi amemwakilisha Rais katika maadhimisho hayo.

Amesema hadi kufika mwaka 2050 Tanzania inakadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 100 hivyo, utunzwaji wa ardhi oevu utasaidia kuendeleza vyanzo vya maji na kupunguza upungufu wa maji.

Pia, ametoa agizo pia kwa Wakala wa Misitu Nchini (TFS) kuhakikisha miti ya kutosha inaoteshwa katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kutunza mazingira na vyanzo vya maji.

Dira ya mwaka 2050 imejumuisha maendeleo ya mazingira na uhifadhi wa ardhi oevu Nchini.

Katika maagizo mengine makamu wa Rais ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuanzisha bustani za kijani na kuzitunza kikamilifu.

Maadhimishi ya Siku ya Mazingira yamehusisha uzinduaji wa program endelevu ya Usimamizi wa Mazingira kuelekea Dira ya mwaka (2050) ambayo itatekelezwa kuanzia mwaka 2026 mpaka mwaka 2030.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika viwanja vya ukumbi w...
05/06/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete tayari kwa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani 2026.

Siku hiyo ilitanguliwa na wiki ya maonesho yaliyoanza tarehe 1 Juni yakiwa na kauli mbiu isemayo Dira 2050 Tuwajibike kukijanisha Tanzania

Pichani ni Banda la maonesho la Wizara ya Maji.

05/06/2026
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akizungumza na Maafisa Rasilimaliwatu  wa Sekta ya Maji  katika ofisi za Wizara zil...
04/06/2026

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akizungumza na Maafisa Rasilimaliwatu wa Sekta ya Maji katika ofisi za Wizara zilizoko mji wa Serikali jijini Dodoma.

Mhe. Aweso amesisitiza ushirikiano kwa watumishi na wadau wa sekta, matumizi ya Teknolojia katika kutatua changamoto mbalimbali pia ubunifu unaolenga kufikia malengo ya Wizara ya Maji.

Amewahakikishia kuwa yeye pamoja na viongozi wa wizara wanatambua mchango wao katika mafanikio yaliyofikiwa na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo ili kuwezesha huduma ya majisafi na salama ambalo ni moja ya malengo ya msingi kwa wizara yanafikiwa kwa haraka zaidi kwa ushirikiano wao wa dhati.

Teknolojia ya Kurejesha  Majitaka kwa  Matumizi Mengine Yajadiliwa na  Wadau Wa Sekta Ya MajiWadau wa Sekta ya Maji wame...
04/06/2026

Teknolojia ya Kurejesha Majitaka kwa Matumizi Mengine Yajadiliwa na Wadau Wa Sekta Ya Maji

Wadau wa Sekta ya Maji wamejadili teknolojia na mbinu za kurejesha majitaka kwa matumizi mengine kwa faida zaidi.

Wadau hao wa maji wamegusia eneo hilo katika kikao jumuishi na Wizara ya Maji Jijini Dodoma.

Wamesema kipo kiasi kikubwa cha maji yanayopotea majitaka, yanayotakana na shughuli mbalimbali nchini, ikiwemo viwandani na makazi. Pia, mashuleni kutokana na shughuli mbalimbali.

Mahitaji makubwa ya maji yanayoongezeka upo ulazima wa kubuni teknolojia itakayorahisisha matumizi kwa kuyageuza majitaka kwa matumizi mengine siku za usoni.


Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Bw. Robert Sunday akiongea na wadau amesema kuwa majitaka majitaka yakigeuzwa kwa matumizi mengine yataleta ahueni na mageuzi makubwa katika nyanja mbalimbali za maisha ya kila siku.

Ameainisha kuwa usimamizi na utunzaji wa mazingira unapaswa kupewa kipaumbele Ili wananchi waendeleee kutumia maji yaliyo salama.

Address

456
Dodoma

Telephone

+255262324634

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ministry of Water posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ministry of Water:

Shortcuts

Share