Ofisi ya Rais-UTUMISHI

Ofisi ya Rais-UTUMISHI Jukumu kubwa la OR-MUUUB ni kuimarisha Utawala Bora katika uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa kubuni Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu

NAIBU WAZIRI QWARAY ASISITIZA UTUNZAJI WA MIRADI YA TASAFNa. Antonia Mbwambo na Helela Lusungu – GeitaNaibu Waziri, Ofis...
18/09/2026

NAIBU WAZIRI QWARAY ASISITIZA UTUNZAJI WA MIRADI YA TASAF

Na. Antonia Mbwambo na Helela Lusungu – Geita

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, amesisitiza umuhimu wa kutunzwa na kutumiwa ipasavyo miradi inayotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili iweze kutoa huduma endelevu na kunufaisha wananchi.

Mhe. Qwaray ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia TASAF katika Mkoa wa Geita, ikiwemo Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Utawala katika Shule ya Sekondari Fazilibucha, iliyopo Kata ya Bombambili, Manispaa ya Geita.

Aidha, Mhe. Qwaray ametembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Huduma za Wagonjwa wa Nje (OPD) pamoja na jengo la Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCH) katika Zahanati ya Kakora, iliyopo Kijiji cha Kakora, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Qwaray amesema kuwa uwekezaji unaofanywa na Serikali kupitia TASAF ni kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii na kuinua ustawi wa wananchi, hivyo ni wajibu wa viongozi na Wananchi kuhakikisha miradi hiyo inatunzwa na kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

“Miradi hii ni mali ya wananchi na imejengwa kwa lengo la kuwapatia huduma bora na endelevu. Ni muhimu kuhakikisha inatunzwa vizuri, inatumika ipasavyo na kila mmoja anawajibika kulinda uwekezaji huu ili uweze kunufaisha jamii.” – Mhe. Qwaray amesema.

Ameongeza kuwa utunzaji wa miundombinu hiyo utasaidia kuongeza muda wa matumizi ya majengo na kuhakikisha Wananchi wanaendelea kupata huduma muhimu za kijamii bila kulazimika kutumia rasilimali nyingi katika ukarabati wa mara kwa mara.
Amesema Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati, inazingatia viwango vinavyohitajika na inatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa.

NAIBU WAZIRI QWARAY ATOA MAELEKEZO KUZINGATIA ANUAI ZA JAMII KATIKA UTUMISHI WA UMMANa. Antonia Mbwambo na Helela Lusung...
17/09/2026

NAIBU WAZIRI QWARAY ATOA MAELEKEZO KUZINGATIA ANUAI ZA JAMII KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Na. Antonia Mbwambo na Helela Lusungu- Nyang’hwale -Geita
Tarehe 17 Septemba, 2026.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, amewataka Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kuhakikisha kuwa utekelezaji wa majukumu ya kiutumishi unazingatia anuai za jamii na mahitaji ya makundi mbalimbali bila ubaguzi, ili kujenga Utumishi wa Umma jumuishi na wenye usawa.

Mhe. Qwaray ametoa kauli hiyo leo, Septemba 17, 2026, wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoani Geita, katika ziara yenye lengo la kutembelea miradi ya maendeleo, kusikiliza changamoto za Watumishi na kujadili namna ya kuboresha utendaji na utoaji wa huduma.
Amesisitiza kuwa uzingatiaji wa anuai za jamii unapaswa kuonekana katika utoaji wa huduma, usimamizi wa watumishi, upangaji wa ajira, mazingira ya kazi na utekelezaji wa stahiki za watumishi.

“Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu wahakikishe kuwa utoaji wa huduma, usimamizi wa Watumishi, upangaji wa ajira, mazingira ya kazi na utekelezaji wa stahiki unazingatia mahitaji na tofauti za makundi mbalimbali ya jamii, bila ubaguzi, ili kujenga Utumishi wa Umma jumuishi na wenye usawa,” amesema Mhe. Qwaray.

Aidha, Mhe. Qwaray amesema Tume ya Utumishi wa Umma inaendelea na ukaguzi wa utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi katika Taasisi za Umma, na kuwataka Waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kushirikiana kikamilifu, kurekebisha mapungufu yatakayobainika na kutekeleza maelekezo ya Tume kwa wakati.

“Kwa ujumla, tunahitaji Utumishi wa Umma unaowajibika, unaozingatia sheria, unaoheshimu haki na kuzingatia anuai za jamii, na unaotoa huduma kwa ufanisi, usawa na kwa wakati,” amesema Mhe. Qwaray.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyang’hwale, Bi. Kaunga Amani, amemshukuru Mhe. Qwaray kwa kutembelea miradi ya maendeleo na kukutana na watumishi ili kusikiliza changamoto zao. Amesema Halmashauri imepokea maelekezo yaliyotolewa na itaendelea kuyatekeleza ili kuboresha utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.

KM MKOMI AFUNGA MAFUNZO YA MFUMO WA e-WATUMISHINa Eric Amani, Jijini DodomaKatibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya...
16/09/2026

KM MKOMI AFUNGA MAFUNZO YA MFUMO WA e-WATUMISHI
Na Eric Amani, Jijini Dodoma

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Juma Mkomi, Leo Septemba 16, 2026 katika Ukumbi wa St Gaspar uliyopo Jijini Dodoma amefunga mafunzo ya Mfumo wa e-Watumishi kwa Maafisa Rasilimaliwatu na Utawala kutoka taasisi mbalimbali za Serikali hapa nchini.

Bw. Mkomi amewataka washiriki kutumia maarifa waliyoyapata kuongeza ufanisi katika usimamizi wa taarifa za watumishi na utoaji wa huduma za kiutumishi kwa kutumia mifumo ya kidijitali.

Amesisitiza umuhimu wa maafisa hao kuhakikisha taarifa za watumishi zinaingizwa na kusasishwa kwa usahihi katika Mfumo wa e-Watumishi, kwa kuzingatia taratibu, miongozo na viwango vya usalama wa taarifa.

Aidha, amewataka washiriki kuwa mabalozi wa matumizi sahihi ya Mfumo wa e-Watumishi katika taasisi zao kwa kuwasaidia watumishi wengine kuelewa na kutumia huduma zinazopatikana kupitia mfumo huo.

MHE.QWARAY AWATAKA WATUMISHI KUKUMBATIA MIFUMO YA KIDIJITINa. Antonia Mbwambo na  Lusungu Helela Naibu Waziri, Ofisi ya ...
16/09/2026

MHE.QWARAY AWATAKA WATUMISHI KUKUMBATIA MIFUMO YA KIDIJITI

Na. Antonia Mbwambo na Lusungu Helela

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray, amewataka watumishi wa umma nchini kuongeza matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kupunguza urasimu na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Qwaray ametoa agizo hilo leo Septemba 16, 2026 wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya ya Geita mkoani Geita kwa lengo la kusikiliza changamoto za watumishi na kujadili namna ya kuboresha utendaji katika Utumishi wa Umma

Amesema matumizi sahihi ya teknolojia ya TEHAMA ni muhimu katika kuongeza kasi ya utendaji na uwajibikaji katika utumishi wa umma na itasaidia kuchagiza jitihada za utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Wajibu wetu wa kwanza chini ya Dira hii mpya ni kuongeza kasi ya utendaji, kukumbatia kikamilifu mifumo ya kidijiti ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma kwa wakati na bila usumbufu,” alisema.

Aidha, alibainisha kuwa mfumo wa e-Watumishi na Watumishi Portal inawezesha watumishi kupata huduma mbalimbali za kiutumishi kwa njia ya mtandao ikiwa ni pamoja na taarifa za mishahara, likizo na uhamisho. Hivyo, amewataka kuitumia kwa makini.

Aliongeza kwa kuwataka watumishi kuhimiza wananchi kutumia mfumo wa e-Mrejesho ambao unatoa fursa kwa wananchi na watumishi kuwasilisha maoni, pongezi, malalamiko na mapendekezo kuhusu huduma zinazotolewa na Serikali.

“Matumizi ya mifumo hii yanapaswa kwenda sambamba na uwajibikaji, weledi na uadilifu kwa kuwa teknolojia ni nyenzo ya kurahisisha utendaji, lakini mafanikio yake yanategemea namna viongozi na watumishi wanavyoitumia,” amesema.

Vile vile, alisisitiza matumizi ya mfumo wa GSD ambao unaweka taarifa za huduma za Serikali katika sehemu moja ya kidijitali na kuwawezesha wananchi, wafanyabiashara na wageni kupata taarifa kuhusu huduma, gharama, masharti na namna ya kuzipata huduma hizo kwa haraka.

Ziara ya Qwaray katika mikoa ya Mwanza na Geita inalenga kusikiliza changamoto za watumishi wa umma na kujadili namna ya kuboresha utendaji na utoaji wa huduma.

KATIBU MKUU MKOMI AWASISITIZIA MAADILI, NIDHAMU, MSHIKAMANO UTUMISHI SCNa Eric Amani, DodomaKatibu Mkuu wa Ofisi ya Rais...
16/09/2026

KATIBU MKUU MKOMI AWASISITIZIA MAADILI, NIDHAMU, MSHIKAMANO UTUMISHI SC

Na Eric Amani, Dodoma

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi, amewaaga na kuwatakia kila la kheri wanamichezo wa Utumishi Sports Club (UTUMISHI SC) wanaokwenda kuiwakilisha Ofisi katika Mashindano ya Michezo ya Wizara, Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI 2026) yanayotarajiwa kufanyika mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza wakati wa kuwaaga wanamichezo hao katika Ukumbi wa Ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali, Mtumba Bw. Mkomi amewataka kwenda kushindana kwa kuzingatia nidhamu, mshikamano, heshima, na uadilifu, huku wakitambua kuwa wanapokuwa uwanjani wanawakilisha siyo tu UTUMISHI SC, bali pia Ofisi ya Rais – Utumishi.

“Nawatakia kila la kheri katika mashindano haya. Nendeni mkaiwakilishe Ofisi yetu kwa vizuri. Ushindi ni muhimu, lakini zaidi ya yote tunataka kuona mnakuwa mabalozi wazuri wa Utumishi wa Umma,” amesema Bw. Mkomi.

Aidha, amewapongeza wanamichezo na viongozi wa UTUMISHI SC kwa juhudi na maandalizi waliyofanya kuelekea mashindano hayo. UTUMISHI SC imeendelea kufanya maandalizi kupitia michezo ya kirafiki, ikiwemo ushindi wa mabao 4–0 dhidi ya Mkonze Veterans katika mchezo uliofanyika Septemba 5, 2026 jijini Dodoma.

UTUMISHI SC inaingia katika mashindano hayo ikiwa na dhamira ya kufanya vizuri, baada ya kutwaa ubingwa wa SHIMIWI mwaka 2025 yaliyofanyika jijini Mwanza.

MRADI WA TANZANIA YA KIDIJITALI (DTP) UMELETA MAPINDUZI MAKUBWA YA MAWASILIANO YA KIMTANDAO YALIYORAHISISHA UTOAJI WA HU...
16/09/2026

MRADI WA TANZANIA YA KIDIJITALI (DTP) UMELETA MAPINDUZI MAKUBWA YA MAWASILIANO YA KIMTANDAO YALIYORAHISISHA UTOAJI WA HUDUMA KWA UMMA

NUKUU ZA LEO ZA NAIBU WAZIRI MHE.REGINA QWARAY
15/09/2026

NUKUU ZA LEO ZA NAIBU WAZIRI MHE.REGINA QWARAY

NAIBU WAZIRI MHE.QWARAYAWAAGIZA WAAJIRI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAAJIRI KWA WAKATINa. Antonia Mbwambo na  Lusungu Helela N...
15/09/2026

NAIBU WAZIRI MHE.QWARAYAWAAGIZA WAAJIRI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAAJIRI KWA WAKATI

Na. Antonia Mbwambo na Lusungu Helela

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray, amewaagiza waajiri kuhakikisha changamoto na stahiki za watumishi wa umma zinashughulikiwa kwa wakati, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Qwaray ametoa agizo hilo leo Juni 16, 2026 wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza kwa lengo la kusikiliza changamoto za watumishi na kujadili namna ya kuboresha utendaji katika Utumishi wa Umma.

Amesema masuala yanayohusu kupandishwa vyeo, uhamisho, malimbikizo ya mishahara na mafao yanapaswa kushughulikiwa kwa wakati na mamlaka husika, badala ya kuendelea kucheleweshwa.

"Nawaagiza waajiri wote kuhakikisha changamoto na stahiki za watumishi, ikiwemo kupandishwa vyeo, uhamisho, malimbikizo ya mishahara na mafao, zinashughulikiwa kwa wakati,” amesema Mhe Qwaray.

Aidha, amesisitiza kuwa madai ya watumishi yanapaswa kuhakikiwa ipasavyo na kuwasilishwa yakiwa na nyaraka zote muhimu ili kuwezesha malipo kufanyika kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Mhe. Qwaray amezitaka Mamlaka za Ajira na Nidhamu kusimamia haki na wajibu wa watumishi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma, huku akiwataka kuachana na utendaji wa mazoea.

Amesema mambo yaliyo ndani ya mamlaka za waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu yanapaswa kushughulikiwa katika ngazi husika badala ya kuendelea kuwasilishwa Ofisini kwake.

Aidha, Mhe. Qwaray amesisitiza umuhimu wa watumishi kutumia mifumo ya kidijitali iliyobuniwa na Serikali katika kusimamia utendaji na kupata huduma za kiutumishi.

Mifumo hiyo ni pamoja na e-Watumishi, Watumishi Portal, e-Utendaji (PEPMIS) na e-Mrejesho, ambayo imeimarishwa kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma, kuongeza uwajibikaji na kutoa fursa kwa wananchi na watumishi kuwasilisha maoni, pongezi, malalamiko na mapendekezo.

Amesema matumizi sahihi ya mifumo hiyo ni sehemu ya jitihada za kujenga Utumishi wa Umma unaozingatia haki, wajibu, uwajibikaji, ufanisi na matumizi ya teknolojia.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buchosa, Bw. Benson Mihayo amesema changamoto za watumishi zitaendelea kushughulikiwa kutokana na bajeti iliyopo huku akibainisha kuwa mwitikio wa watumishi katika suala ujazaji PEPMIS limekuwa na mwitikio mkubwa ukilinganisha na hapo awali hali inayopelekea malalamiko ya watumishi kupungua wakati wa upandaji wa madaraja.

Naye Mbunge wa Buchosa, Mhe. Erick Shigongo ametumia fursa hiyo kuwashukuru Watumishi wa Halmashauri ya Buchosa kwa huduma bora wanazoendelea kutoa kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.

" Hatua ya maendeleo unayoyaona leo hapa Buchosa ni kutokana na uwepo wa watumishi wazalendo waliojitoa kwa lengo la kuwahudumia wananchi" amesisitiza Mhe. Shigongo

MRADI WA TANZANIA YA KIDIJITALI UMELETA MAPINDUZI MAKUBWA YA MAWASILIANO YA KIMTANDAO YALIYORAHISISHA UTOAJI WA HUDUMA K...
15/09/2026

MRADI WA TANZANIA YA KIDIJITALI UMELETA MAPINDUZI MAKUBWA YA MAWASILIANO YA KIMTANDAO YALIYORAHISISHA UTOAJI WA HUDUMA KWA UMMA

Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam

Mradi wa Tanzania ya Kidijitali (DTP) umeleta mapinduzi makubwa ya mawasiliano ya kimtandao yaliyorahisisha utoaji wa huduma za serikali kwa wananchi.

Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Priscus Kiwango ameyasema hayo alipokuwa akimwakilisha Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakati wa kikao kilicholenga kujadili utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Bw. Kiwango amesema kupitia DTP, miradi mingi imetekelezwa na kuleta mafanikio makubwa ikiwemo minara ya simu iliyopelekwa kwenye maeneo mengi ya vijijini ambayo mawasiliano yalikuwa hayapatikani na kwa sasa yanapatikana kwa ubora wa 3G na 4G.

Vilevile amesema, mradi huo umeweka Mawasiliano ya kimtandao kwenye Taasisi za Serikali ikiwemo kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa ajili ya kutumia mifumo mbalimbali ya serikali kidijitali.

Bw. Kiwango ameongeza kuwa, mradi huo umeleta mafanikio makubwa ya kuunganishwa kwa mifumo mingi ya Serikali ambayo ilikuwa ni maelekezo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kubadilishana taarifa kwa taasisi za umma.

Aidha Bw. Kiwango amesema, kupitia mradi huo, Mfumo unaotumika na Taasisi za Umma Kupima Utendaji Kazi wa Watumishi wa Umma (PEPMIS) umetekelezeka.

Bw. Kiwango ametaja mafanikio mengine ya mradi huo wa DTP kuwa ni kupatikana kwa Mfumo wa Daftari la Huduma za Serikali (GSD) unaowawezesha wananchi, wafanyabiashara na wageni kupata taarifa mbalimbali za huduma za serikali katika Wizara, Idara, Wakala, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo, kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma kwa njia ya kidijiti.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Bakari Mwamgugu, amesema lengo kuu la mradi huo ni kupeleka mawasiliano sehemu ambazo hazikuwa na mawasiliano na kuboresha huduma bora kwa mwananchi kidijitali.

Ameongeza kuwa, Minara 304 imeboreshwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia kutoka kwenye 2G Kwenda kuwa na 3G na 4G.

Mradi wa Tanzania ya Kidijitali ulianza mwaka 2021 na unatarajia kukamilika mwaka huu 2026.

TAARIFA KWA UMMA
12/09/2026

TAARIFA KWA UMMA

Address

670
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi ya Rais-UTUMISHI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ofisi ya Rais-UTUMISHI:

Shortcuts

Share

Category