Takukuru.tz

Takukuru.tz Hii ni akaunti rasmi ya TAKUKURU TANZANIA.

ZIARA YA MHE: RIDHIWANI-TAKUKURU MOROGOROMhe. Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi...
21/08/2026

ZIARA YA MHE: RIDHIWANI-TAKUKURU MOROGORO

Mhe. Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ameipongeza TAKUKURU kwa kazi nzuri na inayoendelea kuzitekeleza na kuipa taasisi heshima inayostahili.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika jengo jipya la Ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Morogoro Agosti 20, 2026 ambapo pamoja na mambo mengine alizungumza na watumishi na kusisitiza yafuatayo:

📌Msingi mkubwa wa kazi zetu za kila siku ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo wanayostahili bila kuwepo kwa vitendo vya rushwa, hivyo tufanye kazi kwa wekedi mkubwa.
📌Endeleeni kusimamia fedha mnazopewa za majengo ili thamani ya fedha izidi kuonekana.
📌Jitahidini kuzingatia muda katika chunguzi zenu, ni vizuri chunguzi zisichukue muda mrefu kukamilika.
📌Endeleeni kufanya kazi vizuri kwani Mhe: Dkt. Samia Suluhu Hasan, Raisxwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anawategemea sana.

TAKUKURU - Morogoro Agosti 20, 2026

21/08/2026
MAHAFALI SHULE YA MSINGI BOMBO - TANGAMwanafunzi Shamsa Rashidi M***a ametaja madhara ya rushwa katika sekta ya afya kuw...
21/08/2026

MAHAFALI SHULE YA MSINGI BOMBO - TANGA

Mwanafunzi Shamsa Rashidi M***a ametaja madhara ya rushwa katika sekta ya afya kuwa ni huduma duni, vifo, ukosefu wa dawa na vifaa tiba pamoja na wananchi kupoteza imani kwa serikali yao.

Hayo ameyasema akijibu swali katika moja ya maswali ya chemsha bongo iliyofanyika k**a sehemu ya burudani katika mahafali hayo.

TAKUKURU Tanga, Agosti 16, 2026

MACHANO: TAKUKURU, ZAECA NI TAASISI MUHIMU KATIKA KUSIMAMIA HAKIMwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Waku...
21/08/2026

MACHANO: TAKUKURU, ZAECA NI TAASISI MUHIMU KATIKA KUSIMAMIA HAKI

Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Machano Othman Said, amesema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) ni taasisi muhimu katika kuimarisha usimamizi wa haki na mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Mhe. Machano alisema hayo Agosti 19, 2026, alipoongoza wajumbe wa k**ati hiyo katika ziara ya mafunzo kwenye ofisi za Makao Makuu ya TAKUKURU jijini Dodoma.

ZIARA YA MKURUGENZI MKUU - MKINGA TANGA Agosti 15, 2026 Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila aliwas...
17/08/2026

ZIARA YA MKURUGENZI MKUU - MKINGA TANGA

Agosti 15, 2026 Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila aliwasili Wilaya ya Mkinga ikiwa ni ziara ya kikazi wilayani humo.

Hapa ni Mkurugenzi Mkuu akipokelewa kwa kuvishwa Skafu na vijana wa Skauti wilayani Mkinga.

VIONGOZI WA SENETI ZA VYUO CCM WAAHIDI KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA"Ahadi Na. 4 ya mwanachama wa CCM inasema; _Ru...
17/08/2026

VIONGOZI WA SENETI ZA VYUO CCM WAAHIDI KUSHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

"Ahadi Na. 4 ya mwanachama wa CCM inasema; _Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa_. Hivyo sisi k**a wanachama wa CCM tuko tayari kushiriki kwenye mapambano dhidi ya rushwa ikiwa ni wajibu wa kutimiza ahadi zetu"

Haya yamesemwa na ALLY LINJE wa UVCCM Taifa baada ya Semina iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa katika mafunzo ya Viongozi wa Seneti za Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu - CCM, iliyofanyika Agosti 13, 2026 mkoani Iringa.

ZIARA YA MKURUGENZI MKUU - TANGAMkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila, akiwa mkoani Tanga, Agosti 15...
17/08/2026

ZIARA YA MKURUGENZI MKUU - TANGA

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bw. Crispin Francis Chalamila, akiwa mkoani Tanga, Agosti 15, 2026 alifika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kusalimiana kabla ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, kukabidhi mashine za kuwahudumia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati

Hapa ni wakati Mhe. Dadi Horace Kolimba - Mkuu wa Wilaya Tanga, aliyekuwa akikaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga akitoa maelezo ya ukaribisho.

TAKUKURU RAFIKI KATA YA MUGHANGA - SINGIDA“Ninaipongeza TAKUKURU kwa kubuni Programu ya TAKUKURU Rafiki, ambayo inawawez...
17/08/2026

TAKUKURU RAFIKI KATA YA MUGHANGA - SINGIDA

“Ninaipongeza TAKUKURU kwa kubuni Programu ya TAKUKURU Rafiki, ambayo inawawezesha wananchi kuibua kero na changamoto zilizopo katika maeneo yao ambazo zikiachwa bila kushughulikiwa zinaweza kusababisha vitendo vya rushwa.

Programu hii inatusaidia kutatua kero zinazowakabili wananchi na kutuwezesha sisi viongozi kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi,” amesema Bw. Thobias Erasto, Diwani wa Kata ya Mughanga.

TAKUKURU Singida, Agosti 12, 2026.

WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA WAAHIDI KUPINGA RUSHWA - MKALAMA Bw. Sadru Mvukie kutoka Idara ya Utumishi na Rasilimali Wat...
17/08/2026

WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA WAAHIDI KUPINGA RUSHWA - MKALAMA

Bw. Sadru Mvukie kutoka Idara ya Utumishi na Rasilimali Watu H/W Mkalama, ameishukuru TAKUKURU kwa kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Kata, na kuwasihi kuitumia katika maeneo yao ya kazi.

Amewataka watendaji hao kuwa mfano katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa, kutowashawishi wananchi kutoa rushwa na kutopokea rushwa.

TAKUKURU Mkalama - Singida, Agosti 12, 2026.

USHIRIKIANO WA UTATU NA MAHAKAMA WAIMARISHWA KAGERAViongozi wa taasisi zinazounda UTATU wakiwa katika picha ya pamoja na...
17/08/2026

USHIRIKIANO WA UTATU NA MAHAKAMA WAIMARISHWA KAGERA

Viongozi wa taasisi zinazounda UTATU wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mahak**a Kuu Kanda ya Bukoba baada ya kikao kilicholenga kuimarisha ushirikiano na uratibu katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo, mkoani Kagera, Agosti 12, 2026.

Aliyekaa katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahak**a Kuu Kanda ya Bukoba, Mh. Jaji David Ngunyale, akiwa pamoja na Mh. Jaji Lilian Itemba, Jaji wa Mahak**a Kuu Kanda ya Bukoba.

Viongozi wa UTATU kutoka Dodoma walioshiriki ni Bi. Pendo Makondo, Mkurugenzi - NPS; Bw. Gemin Mushi, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai; na Bw. George Barasa, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria TAKUKURU.

Pia walishiriki viongozi wa UTATU Mkoa wa Kagera ambao ni Bi. Magret Mwasebo (RPO), Bw. Ismail Bukuku (RBC) na ACP Boniphace Mayala Kibuga (RCO).

Kikao hiki ni sehemu ya kuendeleza ushirikiano baina ya taasisi za UTATU na Mahak**a katika kuimarisha utoaji wa haki na utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi.

Address

Jamhuri Street
Dodoma
255

Opening Hours

Monday 07:30 - 16:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Takukuru.tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Takukuru.tz:

Shortcuts

Share