Dr. Omary A Makau PhD

Dr. Omary A Makau PhD Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Dr. Omary A Makau PhD, Government Organization, Dar es Salaam.

UGOMVI WA ORHAN BEY NA ALAEDDIN BEY – NANI ALIKOSEA? (UCHAMBUZI WA SIASA YA VITA)Kwenye tamthilia ya Osman, ugomvi wa nd...
19/03/2026

UGOMVI WA ORHAN BEY NA ALAEDDIN BEY – NANI ALIKOSEA? (UCHAMBUZI WA SIASA YA VITA)

Kwenye tamthilia ya Osman, ugomvi wa ndugu wawili Orhan Bey na Alaeddin Bey unaonyesha mgongano wa mitazamo miwili ya uongozi wa vita: nguvu ya upanga dhidi ya nguvu ya akili ya kimkakati.

KOSA LA ORHAN BEY

• Aliongozwa zaidi na hasira kuliko busara.

• Kiongozi wa vita anatakiwa kudhibiti hisia zake hata k**a anaona amesalitiwa.

• Kumpiga kaka yake ngumi mbele ya askari kulidhoofisha heshima ya uongozi na nidhamu ya jeshi.

• Katika siasa ya vita, mgawanyiko wa viongozi ni zawadi kwa adui.

KOSA LA ALAEDDIN BEY

• Alitoa maamuzi ya kijeshi bila mawasiliano ya wazi na k**anda aliyekuwa vitani.

• Kuondoa askari bila kumjulisha Orhan kulionekana k**a kumwacha peke yake uwanjani.

• Hata k**a lengo lake lilikuwa kulinda jeshi, uamuzi wa kimkakati lazima uendane na mshik**ano wa uongozi.

Vita vinahitaji vitu viwili:

Ujasiri wa wapiganaji k**a Orhan.

Akili ya mipango k**a Alaeddin.

Endapo Orhan atakuwa sultan na akashirikiana vivuri na mdogo ake watakuwa na dola isiyopigika k**a ile ya Chagri bey mtaalamu wa vita na mapigano, na kaka ake Tugrul Bey mtaalamu wa siasa na sayansi ya vita

Lakini vikikosekana pamoja, hata jeshi lenye nguvu linaweza kushindwa kwa sababu ya mgawanyiko wa ndani.

HITIMISHO

Suluhisho la mgogoro k**a huu si nani ana nguvu zaidi au nani ana akili zaidi, bali ni umoja wa viongozi. Orhan anapaswa kujifunza kudhibiti hasira na kuheshimu maamuzi ya kimkakati, wakati Alaeddin anapaswa kuhakikisha mawasiliano na mshik**ano na wapiganaji walioko mstari wa mbele. Wakifanya kazi pamoja, nguvu ya upanga na nguvu ya akili vinaweza kuifanya dola iwe imara zaidi.

Mapenzi ya Osman Bey na Bala Hatun hayakuanzia kwenye maneno mengi, bali yalianza kwenye heshima, imani na moyo safi.Osm...
12/03/2026

Mapenzi ya Osman Bey na Bala Hatun hayakuanzia kwenye maneno mengi, bali yalianza kwenye heshima, imani na moyo safi.

OsmanBey alipokutana na Bala Hatun kwa mara ya kwanza, alivutiwa na tabia yake ya unyenyekevu, hekima na imani yake kubwa kwa Mwenyezi Mungu.
BalaHatun alikuwa binti wa SheikhEdebali, mtu mwenye heshima kubwa na elimu.

Osman Bey alipokua anakwenda kwa Sheikh Edebali mara nyingi kwa ajili ya ushauri, ndipo moyo wake ukaanza kuvutiwa zaidi na Bala Hatun. Lakini Bala Hatun hakuvutiwa na utajiri wala nguvu za Osman, bali alivutiwa na uadilifu wake, ujasiri wake na nia yake ya kulinda haki.

Licha ya vikwazo na maadui waliotaka kuwazuia, mapenzi yao yaliendelea kuwa imara. Osman Bey aliweka wazi nia yake ya kumuoa Bala Hatun mbele ya baba yake Sheikh .

Hatimaye baada ya majaribu mengi, ndoa yao ilifungwa. Bala Hatun akawa sio tu mke wa Osman Bey, bali pia mshauri wake, nguvu yake na mwanamke aliyesimama naye katika kila vita na kila changamoto ya kuijenga dola ya Ottoman empire:

Mapenzi yao yalikuwa mfano wa mapenzi ya kweli mapenzi ya heshima, imani na uaminifu. ❤️. Mimi binafsi k**a Muandishi navutiwa Sana na story Yao ya mapenzi na Uongozi kila naposoma Kuhusu wao na kuwatizama....🙌

K**a Una Imani nae mvumilie hakuna kitu kizuri kinachopatika kiurahisi labda uibe

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr. Omary A Makau PhD posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share