01/07/2026
KIKAO CHA KIKAZI KATI YA KATIBU WA CCM (W) TEMEKE NA UONGOZI WA WALIMU
Leo, ofisi ya Katibu wa CCM (W) Temeke imepata heshima na fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo ya kina na Uongozi wa Kitaifa wa Walimu Makada.
Katibu wa CCM (W) Temeke, Ndugu Daniel George Sayi, aliongoza kikao hiki kilicholenga kuimarisha ushirikiano, kusikiliza maoni na changamoto, na kujadili njia bora za kuboresha maslahi na mazingira ya kazi kwa walimu wetu nchini.
Mazungumzo haya ni sehemu ya utaratibu wa chama kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha tunajenga Taifa lenye elimu bora na walimu wenye motisha.
CCM Oyee! Kazi Iendelee! 🇹🇿🤝🍎