30/05/2026
Mapinduzi ya Kidijitali: Mfumo Mpya wa Usimamizi wa Mashauri (CMS)
Wakati wa Mafunzo ya Mawakili wa Serikali 2026 yaliyofanyika na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ilionyeshwa video inayotambulisha Mfumo wa Usimamizi wa Mashauri wa Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT Case Management System).
Video hiyo ilionyesha muonekano, sifa na faida za mfumo huo wa kidijitali.
Lengo ni kurahisisha upatikanaji wa haki kwa njia ya kiteknolojia na kuongeza ufanisi katika usimamizi na utatuzi wa mashauri ya masoko ya mitaji, dhamana na bidhaa nchini.