18/09/2026
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Modest Mkude, amewapongeza wajasiriamali hususan wanawake wa Arusha kwa ubunifu na juhudi wanazofanya katika kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi, huku akiwataka kutumia fursa zilizopo kurasimisha na kukuza biashara zao ili kuongeza mchango wao katika uchumi wa taifa.
Mhe. Mkude alitoa pongezi hizo leo tarehe 17 Septemba 2026 katika Viwanja vya Ngarenaro, Jijini Arusha, alipokiwa akizungumza na wajasiriamali na wadau walioshiriki katika Kliniki ya Biashara na Viwanda iliyoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikisha taasisi mbalimbali za Serikali zinazotoa huduma kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ikiwemo BRELA.
“Wajasiriamali wanapaswa kutumia fursa zinazopatikana, kuendelea kuwa wabunifu na kuhakikisha biashara zao zinarasimishwa ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali,” alisema Mhe. Mkude.
Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, taasisi zake na sekta binafsi katika kujenga mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wajasiriamali, akieleza kuwa upatikanaji wa elimu na huduma kwa wakati ni sehemu muhimu ya kuwawezesha wafanyabiashara kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Afisa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Rajab Chambega, alibainisha kuwa BRELA imeshiriki katika kliniki hiyo kwa lengo la kusogeza huduma na elimu ya urasimishaji wa biashara karibu zaidi na wafanyabiashara na wajasiriamali.
Aidha, alieleza kuwa kupitia kliniki hiyo, wafanyabiashara wamepata fursa ya kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na BRELA, ikiwemo usajili wa majina ya biashara, usajili wa kampuni, utoaji wa Leseni za Biashara Kundi A, leseni za viwanda pamoja na usajili wa alama za biashara na huduma.
“Lengo letu ni kuhakikisha mfanyabiashara anapata elimu sahihi kuhusu hatua anazopaswa kuchukua ili kurasimisha biashara yake, kuilinda na kuitengenezea mazingira ya kukua,” alisema Chambega.
Vile vile alisema kuwa urasimishaji wa biashara ni hatua muhimu katika kujenga biashara yenye msingi imara, kwa kuwa humwezesha mfanyabiashara kutambulika kisheria na kutumia fursa mbalimbali zinazohitaji biashara kuwa imesajiliwa na kuwa na