15/09/2026
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mha. Machibya Shiwa, amekuwa sehemu ya jopo kwenye Mkutano wa 10 wa Uhandisi Afrika unaoendelea katika Ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 15, 2026.
Mjadala kwenye jopo hilo umejikita katika maeneo mbalimbali ikiwemo umuhimu wa Ufadhili wa Miundombinu; Upatikanaji wa Nishati kupitia Mpango wa Mission 300, Uendelezaji wa Viwanda, Mabadiliko ya Kidijitali na Ushirikiano wa Kikanda.
Awali Mkurugenzi Mkuu, alipokea tuzo kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, kwa kutambua mchango wa TRC katika kufanikisha Wiki ya Uhandisi na Mkutano wa 10 wa Uhandisi barani Afrika.