10/01/2014
Kwanini ni rahisi kushindwa kuliko kufanikiwa katika biashara ya magazeti Tanzania ?
UINGIAJI kaitka biashara ya uchapishaji na uuzaji magazeti Tanzania hivi leo ni kitu kigumu sana sio kutokana na ushindani mkubwa bali kutokana na changamoto zilizopo katika uanzishaji miradi ya kiuchapishaji hapa nchini.
Hapa chini ni baadhi ya changamoto ambazo mjasiriamali anayetaka kuthubutu kuingia kwenye biashara ya uchapishaji, usambazaji na uuzaji gazeti atapaswa kuzikabili penda asipende: Masharti na urasimu katika uanzishaji gazeti. Ili kuanzisha gazeti ni lazima utafute usajili wake na kuna masharti na urasimu yatakayokutoa jasho hadi ufanikishe kupata urajisi kamili. Kenya huwa unaanza gazeti na kulichapisha moja kwa moja na baada ya kuwa mitaani ndio unakwenda kulisajili ; Hata ukinunua gazeti toka kwa mtu mwingine. Inaweza ikawa ni rahisi zaidi kununua haki za umiliki gazeti toka kwa aliyeshindwa kulichapisha, lakini epuka matapeli waliojaa katika eneo hili. Aidha wanaokukodishia gazeti ukianza kufanikiwa ni rahisi kukugeuka au kukataa makubaliano ya awali na kutaka marejeo ya mkataba; Seng'eng'e ya genge la mawakala. Kizingiti kikubwa sana hivi sasa ni genge la mawakala ambao wana umoja katika kukusaidia kufanikisha azma yako au kuliua gazeti lako likingali changa bado. Hawa wana mbinu za kila aina kuhakikisha k**a hawakutaki, unashindwa na unashindwa vibaya. Ujanja na ajizi inayofanyika kwenye eneo hili inaweza ikwa inachangia mtu au shirika kukosa asiimia 25 ya mapato yake halali; Ukame wa watu wanaojua usimamizi na menejimenti ya magazeti. K**a inavyojulikana, mameneja na maofisa wengi kwenye magazeti Tanzania ni watu waliopata ujuzi na maarifa ya kazi zao kutokana na kuwepo kwenye gazeti jengine, lililopo au lililokufa. Aidha, ndivyo ilivyo kwa vyombo vingine vya habari k**a tivii na redio pia. Bado hatujawa na shule kuu inayowafunza watu kuwa mameneja wa vyombo vya habari. Tija katika utendaji kazi inaweza kushuka kwa asilimia 50 kutokana na kuajiriwa watu wasio na uwezo unaostahili kufanya kazi walizopewa; Changamoto katika upatikanaji matangazo ya kutosha. Ili kupata matangazo ya kutosha unahitaji kuwa na gazeti lililokuwepo kwenye mzunguko kwa miezi k**a sio miaka kadhaa. La sivyo, lazima uwe na fedha au mtaji wa kutosha kuweza kuwanunua watoa matangazo mbalimbali ili ufanikishe azma ya kujiendesha pia kwa kutumia pato linalotokana na matangazo. La sivyo, wewe mwenyewe uwe na biashara zako kadhaa ambazo zinahitaji kujitangaza na zitakuwa zikilipa gazeti bila kujali udugu uliopo; Ubia kati ya mawakala na wafanyakazi wa viwanda vya uchapishaji utakakokuwa ukichapisha gazeti lako. Upo uwezekano mkubwa wa kuwa na watu wako au Idara yako ya Usambazaji inayoshirikiana kwa heri au shari na mafundi wa kiwanda cha uchapishaji. Kinachofanyika hapa ni kwamba, mafundi kiwandani hawayaharibu kabisa magazeti machafu (reject) k**a wanavyopaswa, hadi yawe yasiyosomeka. Bali huyaacha mengi yakiwa bado yanaweza kuonekana k**a yaliyorudi baada ya magazeti safi kuuzwa. Wakala wanauziwa magazeti hayo machafu na kuyarudisha kwako mchapishaji k**a vile ni nakala zilizorudi bila kuuzwa (returns),lakini wao wameshauza pengine na kumaliza mgawo wao wa kila siku. Kwa namna hii, hasara unakula wewe, wakati mchapishaji na idara yako ya usambazaji inazidi kuvimbiana tu. Mtu au kampuni inaweza kupoteza kufikia asilimia 30 ya mapato halali kwa hujuma zinazofanywa katika eneo hili; Mtihani katika usambazaji. K**a nilivyosema awali ukitegemea usambazaji kupitia wakala waliopo hivi leo, lolote linaweza kutokea. Nimekwishaona mawakala waliosusia kuuza gazeti eti tu kwa sababu hawakualikwa kwenye hafla ya kulizindua gazeti husika. Hatari kubwa inakuwepo pale ambapo mkuu wa usambazaji anawez akafanya maamuzi ya kifedha au kibiashara bila kumshirikisha meneja mkuu; Mtihani katika viwanda vya uchapishaji. Bado uaminifu na udhibiti katika mashirika mengi ya uchapishaji ni mdogo na kwa kuwa kazi yenyewe inafanyika USIKU, ina mianya kadhaa inayotumika kupoteza lengo na mafundi uchapishaji kuhakikisha kwamba wanalichapisha gazeti wakati ambapo hamna udhibiti wa kutosha. Wafanyakazi wapowapo na wasiojitambua. Magazeti mengi bado yanaajiri wafanyakazi ambao hawajali kinacholisibu gazeti, bali wanafikiria tu mishahara na posho zao wakati wote. Hiyo ni haki yao. Lakini, je, katika nyakati hizi mkiachia gazeti kuwa na mianya mingi kiasi hicho huo mshahara kweli utapatikana kiurahisi au kazi itakuwa ni kulipana tarehe 32 k**a sio 45 ya kila mwezi? Tambua malipo ya mishahara yanapocheleweshwa, wafanyakazi wanavunjika moyo, wanakosa hamasa na wengi wao wanakuwa madeiwaka kwa magazeti au vyombo vingine vya habari. Ajizi toka kwa waajiriwa na wale wanaostahili kuiona mali ya kampuni k**a vile ni mali yao inachangia kupotea kwa zaidi ya asilimia 25 ya mapato ya mtu au kampuni; Maudhui zianzofanana na wengine. Ukiyaangalia magazeti mengi nchini huwa na habari zilezile k**a ni udaku, ni udaku au k**a ni habari za kwaida, habari ni zile zile na pengine zimeandikwa na mwandishi huyo huyo kwa majina tofauti. Kablal hujaingia kwenye biashara ya gazeti hakikisha kuwa una mawazo ya maudhui tofauti kabisa angalau kwa robo gazeti k**a sio thuluthi gazeti tofauti na ya yale yaliyomo kila leo kwenye magazeti yaliyopo. Kufa kwa soko la mazoea na kuzuka soko jipya la vijana wa smartphone. Hivi leo wasikilizaji wengi wa redio za kitaifa na watazamaji wa tivii za kitaifa na wasomaji wenye uwezo wa kununua magazeti ni wale wenye umri wa miaka 45 na kuendelea. Walio chini ya hapo wengi wao wanapendelea kufuatilia mambo kwenye tovuti au simu zao za mkononi. Mwelekeo huu inaelekea ndio tu umeanza kuchanua hivi sasa na utazidi kuendelea kadri simu za smartphone zinavyozidi kufirika na kuwa za bei nafuu zaidi nchini; Ukosefu wa ubunifu na uvumbuzi wa mambo mapya. Chombo cha habari cha kesho na keshokutwa kitakachofanikiwa, kwa maoni yangu, kittakuwa ni kile kitakachoweza kuivisha katika chungu kimoja biashara ya simu za mkononi ma maudhui hitajika; matangazo ya tivii na redo na matumizi yanayoendana na wakati ya tovuti kwa kuwa na wavuti zinazobeba yale yaliyomo kaika midia nyengine.
Baada ya muda sio mrefu pia, makampuni ya magazeti yatakayochangia kuwa na mashine za bei nafuu za kumuwezesha mtu kuchapisha nakala chache tu za gazeti (zima au sehemu yake ) nyumbani au ofisini kwake ndio yatakayoendelea kuvuna kutoka kwa wasomaji wake waaminifu.
Ieleweke kwamba hatusemi moja kwa moja kwamba yeyote anayetaka kuanzisha gazeti Tanzania atashindwa. La, hasha ! K**a una vyanzo vingine vya fedha vya kutegemea ma visivyokauka kiurahisi; k**a una njia za kupata matangazo kutoka serikalini na mashirika makubwa; k**a una wafanyakazi wachache na wanaoweza kufanya kazi sio chini ya masaa 14 kwa siku na k**a utaweza kufuatilia yote yanayofanywa na walio chini yako, bado uchapishaji gazeti sio kazi mbaya na hasa k**a utakuja na maudhui inayosadia kuwaamsha na kuwawezesha watu kimawazo, kiajira na kiuchumi kwa ujumla.
>
+255782808539
[email protected]