TCRA CCC - Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

TCRA CCC - Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano -
The Consumer Consultative Council of the Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA-CCC)

Tuwalinde watoto wetu dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao.
14/09/2026

Tuwalinde watoto wetu dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao.


KAMATI YA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO YAUNDWA MKOANI SHINYANGA.Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasi...
08/09/2026

KAMATI YA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO YAUNDWA MKOANI SHINYANGA.

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC) leo Septemba 8, 2026, limeunda Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Shinyanga, ikiwa na lengo la kuimarisha ulinzi wa haki na usalama wa watumiaji wa huduma za mawasiliano, pamoja na kuhakikisha changamoto zinazowakabili watumiaji zinafikishwa katika mamlaka husika kwa ajili ya hatua stahiki.

Kamati hiyo imeundwa na Wajumbe watano wakiwakilisha makundi ya Vijana, wanawake, wajasiriamali, makundi maalumu na wawakilishi wa viongozi wa dini na viongozi wa kata, mitaa na vijiji wakiwa na jukumu la kuelimisha, kuhamasisha na kukusanya maoni ya watumiaji katika ngazi ya mkoa na kuwasilisha kwenye baraza.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya awali kwa wawakilishi Katibu Mtendaji wa TCRA-CCC, Bi. Mary Msuya amesema uundwaji wa k**ati unatambulika kisheria lengo likiwa ni kutambua mahitaji ya makundi mbalimbali ya watumiaji wa mawasiliano kupata wawakilishi wa maeneo husika.

“Hadi sasa tumefanikiwa kuunda k**ati 22 katika mikoa mbalimbali nchini, ambazo zipo katika mikoa minne ya Zanzibar na mikoa 18 Tanzania Bara, na leo Shinyanga tunaunda k**ati nyingine moja ambayo itakuwa ya 23,” amesema Bi. Msuya.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Elimu na Uhamasishaji TCRA-CCC, Bw. Hilary Tesha amesema lengo la kuundwa kwa k**ati hiyo ni kuhakikisha wananchi wanafahamu haki na wajibu wao k**a watumiaji wa huduma za mawasiliano, pia inapaswa kuwa sikio kwa kukusanya changamoto za watumiaji na kuzifikisha katika mamlaka husika.

Salamu za Pole
08/09/2026

Salamu za Pole

KAMATI YA WATUMIAJI MKOA WA KUSINI UNGUJA YATOA ELIMU KWA VIONGOZI WA DINI KUHUSU USALAMA WA MTOTO MITANDAONI📍KUSINI UNG...
08/09/2026

KAMATI YA WATUMIAJI MKOA WA KUSINI UNGUJA YATOA ELIMU KWA VIONGOZI WA DINI KUHUSU USALAMA WA MTOTO MITANDAONI

📍KUSINI UNGUJA

Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Kusini Unguja imefanya mkutano wa elimu na uhamasishaji kwa viongozi wa dini wa Shehia ya Koani, Jimbo la Uzini, Wilaya ya Kati. Mkutano huo uliofanyika Septemba 7, 2026 katika Skuli ya Koani Msingi ulilenga kuwafikia viongozi wa dini k**a wadau muhimu katika kuwafikishia jamii ujumbe wa matumizi bora na salama ya huduma za mawasiliano.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwakilishi wa Kamati ya watumiaji Mkoa wa Kusini Unguja alisema kuwa lengo ni kuwajengea uwezo viongozi wa dini ili waweze kutoa elimu kwa wafuasi wao kuhusu athari za matumizi mabaya ya huduma za mawasiliano hususani mitandao ya kijamii.

Aliongeza kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuwaelimisha waumini wao na kuwalinda watoto ambao kwa kiasi kikubwa ndio wanaathirika zaidi na matumizi yasiyo sahihi ya mtandao.

Katika mafunzo hayo mada tatu muhimu zilitolewa. Mada hizo ni pamoja na ulinzi wa mtoto mitandaoni, matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano na athari zake katika jamii, pamoja na njia za kuwasilisha malalamiko endapo atakutana na changamoto.

Aidha; Kamati iliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuwa mabalozi wa kutoa elimu hiyo katika taasisi zao ili kulinda jamii hususan watoto, dhidi ya matumizi mabaya ya huduma za mawasiliano.

Kamati iliahidi kuendelea na zoezi k**a hilo katika shehia nyingine ili kuhakikisha kila mtumiaji anapata huduma bora, salama na anafahamu haki na wajibu wa matumizi ya ya huduma za mawasiliano.



📍KUSINI UNGUJAKamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa  Kusini Unguja imeendesha mkutano wa elimu na uhamasi...
02/09/2026

📍KUSINI UNGUJA

Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Kusini Unguja imeendesha mkutano wa elimu na uhamasishaji kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa watoto dhidi ya athari za matumizi mabaya ya huduma za mawasiliano.

Kamati imetoa elimu kwa wanafunzi wa Madrasa iliyopo katika Kijiji cha Bambi, Shehia ya Mitakawani, Jimbo la uzini, Wilaya ya Kati.

Mafunzo hayo yalihusu usalama wa mtoto mitandaoni, matumizi sahihi ya mtandao kwa watoto, pamoja na njia za kutoa taarifa pindi wanapobaini changamoto katika matumizi ya huduma za mawasiliano.

Katika hatua nyingine Kamati hiyo ilikutana na wajane katika Kijiji cha Mgeni Haji, Shehia ya Mgeni Haji, Jimbo la uzini, Wilaya ya Kati.

Akizungumza na wazazi hao, Mjumbe wa Kamati hiyo ndugu Mohamed Said alisema "watoto walioondokewa na wazazi wao ni wahanga zaidi wa matumizi mabaya ya mitandao, hivyo ni muhimu wazazi au walezi kuwa makini na kuwaelimisha mapema kabla ya athari kutokea".

Wazazi hao walielimishwa kuhusu matumizi sahihi ya mawasiliano na jinsi ya kuwalinda watoto wao dhidi ya athari zinazoweza kutokea kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya mawasiliano.

Kamati ya Watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Kusini Unguja inaendelea na jitihada za kuelimisha watumiaji ikiwa ni sehemu muhimu ya majukumu ya Kamati ya kuelimisha na kusambaza taarifa zenye maslahi ya watumiaji wa huduma za bidhaa za mawasiliano .

mtandaoni
wa mtoto mtandaoni
kwa uma

Tabora📍Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Tabora imefanya mkutano wa kuelimisha na kuhamasisha vijana ...
31/08/2026

Tabora📍

Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Tabora imefanya mkutano wa kuelimisha na kuhamasisha vijana wa Kanisa la FPCT-Ipuli mkoani Tabora tarehe 29 Agosti 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mafunzo hayo, mwakilishi wa Kamati hiyo alisema kuwa lengo kuu ni kuwaelimisha vijana kuhusu masuala muhimu yanayogusa maslahi ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano.

Masuala hayo ni pamoja na haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano, matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, pamoja na ulinzi wa taarifa binafsi ili kujikinga na utapeli na uhalifu wa kimtandao.

Katika mafunzo hayo jumla ya vijana 33 walishiriki, ambapo kati yao walikuwa wasichana 20 na wavulana 13. Vijana hao walionyesha kuridhishwa na elimu waliyoipata na kuahidi kuitumia katika maisha yao ya kila siku.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya watumiaji ya Mkoa wa Tabora amesema kuwa k**ati hiyo itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini, shule na makundi mbalimbali ya kijamii kuhakikisha elimu ya ulinzi wa mtumiaji inafika kwa wananchi wote. Alisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa kila mtumiaji anapata huduma bora na anafahamu haki zake

29/08/2026
MorogoroKamati ya Watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Morogoro imefanya ziara na kutoa elimu kwa wananchi wakati ...
28/08/2026

Morogoro

Kamati ya Watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Morogoro imefanya ziara na kutoa elimu kwa wananchi wakati wa Tamasha la Nne la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika Mkoani Morogoro.

Akizungumza na wananchi katika tamasha hilo, Mwenyekiti wa k**ati hiyo Ndug.Samweli Msuya amesema wamekuwa wakitoa elimu juu ya matumizi mazuri ya huduma za mawasiliano. Pia wametoa elimu kwa watumiaji kuhusu haki na wajibu wao pamoja na jinsi ya kutoa taarifa iwapo kuna viashiria vya utapeli mitandaoni.

Mbali na kutoa elimu, k**ati hiyo pia imetoa na kugawa vipeperushi mbalimbali kwa washiriki wa tamasha hilo ili kuwaongezea uelewa kuhusu masuala ya mawasiliano na ulinzi dhidi ya utapeli mtandaoni.

Tamasha la Kitaifa la Utamaduni linaloendelea Mkoani Morogoro limekuwa jukwaa la kuwafikia wananchi wengi na kuwapa uelewa juu ya masuala mbalimbali ikiwemo matumizi salama ya teknolojia na mawasiliano

Tunawatakia Waislamu na Watanzania Wote, Sikukuu Njema.
25/08/2026

Tunawatakia Waislamu na Watanzania Wote, Sikukuu Njema.

24/08/2026


Address

14 Jamhuri Street
Dar Es Salaam
11470DARESSALAAM,

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00

Telephone

+255652966633

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TCRA CCC - Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to TCRA CCC - Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano:

Shortcuts

Share