Latra ccc

Latra ccc Waweza kusoma sheria zaidi kwenye website yetu ambayo ni www.latraccc.go.tz

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA Consumer Consultative Council), lipo kwa mujibu wa Kifungu Namba 29 cha Sheria namba 3 ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, (LATRA) ya Mwaka 2019. Sheria hiyo inatoa wajibu kwa Baraza kwa:
(i) Kuwakilisha maslahi ya watumiaji wa huduma za usafiri Ardhini, kwa kuwasilisha, kupata maoni na taarifa na kwa kushauriana na Mamlaka, Waziri mwenye dhamana na wadau wa sekta mbalimbali zinazodhibitiwa;
(ii) Kupokea na kusambaza taarifa na maoni mbalimbali kuhusu masuala yanayowagusa watumiaji wa huduma zinazosimamiwa na LATRA;
(iii) Kuunda kamati za Watumiaji wa huduma za usafiri wa Sekta zinazodhibitiwa na LATRA katika Mikoa na Kushauriana nazo;
(iv) Kushauriana na wadau , Serikali na makundi ya watumiaji kuhusu huduma;
(v) Kufanya utafiti juu ya maslahi, haki, wajibu na masuala mengine yanayogusa watumiaji.

Address

Dar Es Salaam
VICTORIAHOUSE,BAGAMOYOROAD,9THFLOOR,ROOMNO:25

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Latra ccc posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Latra ccc:

Shortcuts

Share