18/09/2026
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya, Bw. Abdallah Mitawi, tarehe 17 Septemba 2026 amefanya ziara katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ikiwa na lengo la kufahamu kwa kina shughuli zinazotekelezwa na Mamlaka hiyo pamoja na mchango wa bandari katika kukuza biashara, usafirishaji na uchumi wa Taifa.
Katika ziara hiyo, Bw. Mitawi amepokelewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mha. Dkt. Baraka Mdima, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bw. Mitawi ameipongeza Menejimenti ya TPA kwa mafanikio yaliyopatikana katika kuhudumia shehena na kuongeza mapato kupitia bandari zinazosimamiwa na Mamlaka hiyo.
Amesema mafanikio hayo yanadhihirisha umuhimu wa kuendelea kuboresha ufanisi wa huduma za bandari, kuimarisha matumizi ya teknolojia na ubunifu, pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya usafirishaji.
Kwa upande wake, Mha. Dkt. Baraka Mdima amemshukuru Naibu Katibu Mkuu kwa kutembelea TPA na kueleza kuwa Mamlaka itaendelea kutekeleza kwa ufanisi maelekezo na mipango ya Serikali katika kuboresha huduma za bandari na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa.
Dkt. Mdima amesema TPA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya usafirishaji na biashara, wakiwemo wadau kutoka Sekta Binafsi, katika kuongeza ufanisi na tija katika sekta ya bandari, kuboresha huduma za kuhudumia na kushughulikia mizigo, pamoja na kuimarisha ushindani wa bandari za Tanzania.
Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Wizara ya Uchukuzi na TPA za kuimarisha ushirikiano na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mikakati ya Serikali katika kuendeleza sekta ya usafirishaji, kukuza biashara na kuimarisha nafasi ya Tanzania k**a kitovu cha biashara na usafirishaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
wizara_ya_uchukuzi Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News