NemcTanzania

NemcTanzania Karibu katika ukurasa rasmi wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC). Pamoja tulinde na kutunza mazingira kwa maendeleo endelevu.

17/09/2026
NEMC YASHIRIKI MKUTANO WA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM-MIKAKATI YA USAFI WA JIJIBaraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi...
17/09/2026

NEMC YASHIRIKI MKUTANO WA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM-MIKAKATI YA USAFI WA JIJI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila uliowakutanisha wahariri wa vyombo vya habari na Viongozi wa Jiji la Dar es Salaam kujadili hatua na mikakati ya pamoja kuimarisha usafi wa Mazingira katika Jiji la Dar es Salaam.

Hatua hiyo ni Utekelezaji wa wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia kauli yake kuhusu hali ya uchafuzi wa Mazingira katika Jiji la Dar es Salaam.

Amesema watanzania wote kwa kila kaya wanapaswa kuwa na vifaa vya kutunzia taka (Dustins) angalau viwili au zaidi ili kurahisisha utenganishaji taka, pia magari kuwa na kifaa kimoja, pamoja na kuwepo kwa mapipa katika stendi na maeneo mbalimbali ya huduma huku akieleza umuhimu wa kutumia vifaa vya kisasa vya usafi na vya kuwekea taka katika maeneo mbalimbali ili kurahisisha shughuli za usafi kufanyika kwa ufanisi.

Aidha Mhe. Chalamila amesema tayari Serikali imeanza mashirikiano na Taasisi za kifedha zikiwemo Benki na Kampuni za kuzalisha vifaa vya kutunzia taka ili kuhakikisha vifaa hivyo vinapatikana kwa wingi huku akisisitiza kuwa mkakati wa kusafisha Jiji la Dar es Salaam hautegemei tu kuondoa taka bali kuchakata taka na kuzibadili kuwa bidhaa ikiwemo Gesi.

Pamoja na mikakati iliyojadiliwa, Mhe. Albert Chalamila ametoa wito kwa watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya Mvua za El ñino zinazotarajiwa kunyesha ikiwa ni pamoja na kuzingatia ushauri na taarifa zinazotolewa na Mamlaka husika.

Naye Meneja wa Kanda ya Mashariki Kaskazini, Bi. Glory Kombe akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, amesema kila mwananchi ana haki ya kuishi katika mazingira safi na salama kwa mujibu wa Sheria hivyo ni wajibu kwa kila mmoja kutunza na kuhifadhi mazingira huku akisisitiza kuwa usafi wa Jiji la Dar es Salaam unahitaji ushiriki na hatua za pamoja kutoka kwa viongozi, vyombo vya habari na jamii ili kurejesha usafi wa jiji.

Madereva wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanashiriki Kongamano la Chama cha Madereva Tanz...
17/09/2026

Madereva wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanashiriki Kongamano la Chama cha Madereva Tanzania( CMST) lililoanza tarehe 12 Septemba na kutarajiwa kuhitimishwa Septemba 19, 2026 Jijini Dodoma.

Pamoja na kuwajengea uwezo, Kongamano hilo pia limejumuisha kuwakumbusha madereva wa serikali mambo mbalimbali ya msingi kuhusiana na maadili ya Utumishi wa Umma, matumizi na utunzaji wa magari na kuzingatia Sheria za barabarani.

Aidha, waajiri, wamesisitizwa kuwatengenezea Madereva mazingira mazuri ya kazi ikiwa ni pamoja na kuzingatia maslahi yao, na pia kuwapa mafunzo yatakayowawezesha madereva kutumia magari ya kisasa na yenye teknolojia mpya.

Wajiolojia wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamehudhuria Kongamano la Mwaka la Wajiolojia ...
16/09/2026

Wajiolojia wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wamehudhuria Kongamano la Mwaka la Wajiolojia Nchini (TGS 2026) lililofanyika Mkoani Mwanza katika ukumbi wa Kwatunza Beach Arena.

Kongamano hili lilifunguliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. CPA Subira Mgalu na kuhitimishwa na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Stephen Kiruswa.

NEMC YATOA WITO WA KUGEZA UBUNIFU WA MAZINGIRA KUWA FURSA ZA UWEKEZAJI NA AJIRAWito juu ya mambo makubwa mawili watolewa...
16/09/2026

NEMC YATOA WITO WA KUGEZA UBUNIFU WA MAZINGIRA KUWA FURSA ZA UWEKEZAJI NA AJIRA

Wito juu ya mambo makubwa mawili watolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Careen Kahangwa kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi aliyekuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya kufunga Mkutano wa Tanzania Green Summit 2026 ukiofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Dkt. Careen amesema jambo la kwanza ni kujenga mfumo wa kugeuza ubunifu na fursa za mazingira kuwa miradi inayotekelezeka, inayoweza kufadhiliwa na inayoweza kukua. Akisisitiza kuwa hii inamaanisha kuunganisha wabunifu, wajasiriamali na jamii na ujuzi, teknolojia, masoko, taasisi za fedha na washirika wa maendeleo.

Amesema, "hatupaswi kuridhika kuona mawazo mazuri yakibaki kwenye mashindano, maonesho au miradi ya majaribio. Tunahitaji kuyaona yakibadilika kuwa biashara endelevu, ajira, uwekezaji na suluhisho kwa changamoto za mazingira na tabianchi."

Amesema jambo la pili ni kujenga ushirikiano wa kudumu unaotafsiri maazimio ya kongamano hili kuwa hatua na matokeo yanayopimika. Akisisitiza kuwa Tanzania Green Summit isiwe tukio la siku mbili pekee, bali iwe sehemu ya mchakato unaoendelea wa kuunganisha sera, ubunifu, fedha, teknolojia na utekelezaji.

Ameongeza, "Tunahitaji kufuatilia fursa zilizojadiliwa, kuendeleza ushirikiano ulioanzishwa na kupima matokeo ya hatua zitakazochukuliwa baada ya kongamano hili."

Tanzania Green Summit 2026 imefanyika kwa siku mbili kuanzia trh 15 hadi 16 Septemba, 2026 ikiwa na kaulimbiu isemayo "Turning Climate Action into Opportunity" ikiwa na maana ya Kugeuza Hatua za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kuwa Fursa.

NAIBU WAZIRI KWAGILWA ATOA MAAGIZO KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑONaibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazing...
16/09/2026

NAIBU WAZIRI KWAGILWA ATOA MAAGIZO KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Reuben Nhamanilo Kwagilwa, ametoa maagizo kwa wakuu wa mikoa nchi nzima kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na athari za kimazingira zinazoweza kusababishwa na mvua za el niño zinazotarajiwa kunyesha nchini ikiwemo kusitisha shughuli za kilimo na Biashara katika maeneo hatarishi pembezoni mwa mito na kuandaa mpango wa kuhamisha wananchi wanaoishi katikati maeneo yanayoweza kuathiriwa na mafuriko.

Mhe. Kwagilwa ametoa agizo hilo wakati akiendelea na ziara katika mikoa ya Arusha na Manyara iliyoanza Septemba 14, 2026, kwa lengo la kukagua maeneo hatarishi kwa mafuriko na kuweka mikakati ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua ambapo ameelekeza shughuli zote zinazofanyika pembezoni mwa mito katika ziwa Manyara kusitishwa mara moja na kuandaliwe mpango wa kuwanusuru wananchi wanaoishi safu za Bonde la ufa Kata ya Mangara.

Naibu Waziri ametoa maagizo hayo baada ya kutembelea Ziwa Manyara na maeneo ya mashamba ya Mangara mkoani Manyara, Migungani B na Jangwani, ambako amekagua hali ya mazingira pamoja na shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika maeneo hayo.

Naye Mkurugenzi wa Utekelezaji na Uzingatiaji wa Sheria wa NEMC, Bw. Elibariki Bajuta, akizungumza wakati wa ziara hiyo, amesema wananchi wanapaswa kuzingatia Sheria na Kanuni za Mazingira na kuepuka kufanya shughuli katika maeneo hatarishi ili kupunguza uwezekano wa kutokea kwa mafuriko na madhara yake.

Ziara hiyo imewashirikisha viongozi na wataalamu mbalimbali, wakiwemo Wakuu wa Wilaya, viongozi wa Serikali za Mitaa, viongozi wa Ulinzi na Usalama, Madiwani, pamoja na wadau wa mazingira na miundombinu, kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na athari za mvua na mafuriko.

WAZIRI MASAUNI AITAMBUA NEMC K**A MLEZI WA GREEN SUMMITWaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), ...
15/09/2026

WAZIRI MASAUNI AITAMBUA NEMC K**A MLEZI WA GREEN SUMMIT

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Yusuf Masauni, amelitambua na kulipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa nafasi yake muhimu k**a Mlezi na mdau wa kitaasisi wa Tanzania Green Summit.

Akizungumza Septemba 15, 2026 wakati wa ufunguzi wa Tanzania Green Summit 2026, Waziri Masauni amesema nafasi hiyo inaakisi dhamana ya NEMC katika usimamizi bora wa mazingira kupitia utekelezaji wa Sheria za Mazingira, Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ukaguzi, tafiti, uhamasishaji wa umma na uratibu wa masuala ya mazingira.

Waziri Masauni amesema Tanzania ina fursa kubwa katika nishati jadidifu, kilimo endelevu, nishati safi ya kupikia, uchumi wa mzunguko, uhifadhi wa mazingira, usimamizi wa taka na uchumi wa buluu, ambazo zinapaswa kugeuzwa kuwa thamani ya kiuchumi, ajira na maendeleo kwa wananchi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushiriki wa vijana katika agenda ya mazingira na tabianchi, akiwataka kutambuliwa k**a wabunifu, wajasiriamali, watafiti na viongozi wa baadaye wa uchumi wa kijani. Amehimiza kuwaunganisha vijana na ujuzi, teknolojia, mitaji, ushauri wa kitaalamu na masoko ili kuwawezesha kupata ajira na kukuza biashara.

Waziri Masauni amewataka wadau wote kutumia jukwaa la Tanzania Green Summit kuhamisha majadiliano kuwa vitendo, vitendo kuwa matokeo yanayopimika na matokeo kuwa mafanikio endelevu yenye manufaa kwa Taifa.

14/09/2026

TUSIFUNGULIE CHEMBA ZA MAJI MACHAFU NA VINYESI WAKATI WA MVUA, NI HATARI KWA AFYA

Address

Regent Street
Dar Es Salaam
00000

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 09:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NemcTanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share