01/06/2026
Leo ni siku ya kihistoria kwa taifa letu tunapoadhimisha Madaraka Day katika Kaunti ya Wajir.
Nimefarijika kuona uongozi wa Rais Dkt. William Samoei Ruto ukichukua hatua madhubuti za kurekebisha changamoto za muda mrefu zilizokwamisha maendeleo ya Kaskazini mwa Kenya.
Uwekezaji mkubwa katika elimu, afya, makazi nafuu, miundombinu na sekta ya mifugo ni ushahidi kuwa kila sehemu ya Kenya ina nafasi sawa katika safari ya maendeleo ya taifa letu.
K**a Mshauri wa Kisiasa wa Rais, ninaunga mkono dhamira hii ya kuhakikisha hakuna Mkenya wala eneo lolote linaloachwa nyuma kutokana na historia, jiografia au siasa.
Tuendelee kushirikiana kujenga Kenya yenye usawa, fursa na maendeleo kwa wote.
Hon. Karisa Nzai Munyika
Mshauri wa Kisiasa wa Rais, Ikulu 🇰🇪