24/08/2022
MASOMO YA MISA
ALHAMISI, AGOSTI 25, 2022
JUMA LA 21 LA MWAKA
SOMO 1
1 Kor. 1:1 – 9
Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu. Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo yesu; kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote; k**a ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu; hata hamkupungukiwa na karama yoyote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingine katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 145:2 – 7 K (1)
(K) Ee Bwana, nitalihimidi jina lako milele na milele.
Kila siku nitakuhimidi,
Nitalisifu jina lako milele na milele.
Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,
Wala ukuu wake hautambulikani. (K)
Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako,
Kitayatangaza matendo yako makuu.
Nitakufikiri fahari ya utukufu wa adhama yako,
Na matendo yako yote ajabu (K)
Watu watayajua matendo yako ya kutisha,
Nami nitausimulia ukuu wako.
Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu.
Wataiimba haki yako. (K)
SHANGILIO
Yn. 14:23
Aleluya, aleluya,
Mtu akinipenda, atalishika neno langu,
na Baba yangu atampenda,
na sisi tutakuja kwake.
Aleluya.
INJILI
Mt. 24:42 – 51
Yesu aliwambia wanafunzi wake: Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni neno hili; k**a mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa kat