WNB Maana halisi ya Ndagu
Ni aina ya nyasi kama magugu ambayo ukiing'oa chini huwa ina mbegu kama karanga

Ubuntu technology wanakualika K**a unapitia changamoto hizo katika matangazo yakulipia Instagram au Facebook Namba za ma...
30/03/2024

Ubuntu technology wanakualika
K**a unapitia changamoto hizo katika matangazo yakulipia Instagram au Facebook
Namba za mawasiliano zipo hapo
Pia k**a unahitaji followers FB,IG,Tiktok na YouTube (subscribers,view’s,watch hours na likes)
kwa gharama nafuu

29/11/2023

Kwa mahitaji ya
Vifaa vyote vya production
Tupigie simu au Whatsapp
0767647882 au 0623428213
Tupo kariakoo jirani na kanisa KKKT

Ukipata hata tatu ivi nidai zawadi
10/11/2017

Ukipata hata tatu ivi nidai zawadi

Yafahamu maisha ya nyukiNyuki ni mdudu mwenye mabawamanne angavu na mwiba nyuma yamwili wake anayekusanya mbelewele yama...
30/10/2017

Yafahamu maisha ya nyuki

Nyuki ni mdudu mwenye mabawa
manne angavu na mwiba nyuma ya
mwili wake anayekusanya mbelewele ya
maua k**a chakula chake. Aina
inayojulikana hasa ni nyuki wa asali wa
familia apis. Kuna spishi zaidi za 20,000
zinazojumlishwa na biolojia kati ya
nyuki lakini ni wale wa jenasi apis
wanaokusanya asali inayovunwa na
wanadamu.
Nyuki za asali mara nyingi wanafugwa
lakini wengine wanaishi porini na asali
yao inakusanywa kwa kuvunja mzinga
wao. Katika Afrika kwa jumla sehemu ya
asali bado inatokana na nyuki asali wa
porini lakini ufugaji nyuki unapanua.

Mwili wa nyuki
Mwili una pande tatu jinsi ilvyo kwa
wadudu wote: kichwa mbele, kidari
katikati na tumbo nyuma, halafu jozi
tatu za miguu na jozi mbili za mabawa.
Mwili huwa na nywele na ina rangi kali
za njano-nyeusi k**a onyo dhidi ya
maadui.
Nyuma ya tumbo wanabeba mwiba
wanaotumia kudunga wakijisikia
wameshambuliwa. Wakidunga mwiba
wanaingiza pia kiasi kidogo cha sumu
katika kidonda. Sumu hii inasababisha
maumivu na watu wengine
wanaathiriwa vikali lakini si kila mtu.
Kuna nyuki wanaokufa baada ya
kudunga kwa sababu mwiba unabaki
kwenye kidonda lakini wengine
wanaweza kutoa mwiba na kudunga
tena.
Wadudu wa kijamii
Nyuki asali ni wadudu wa kijamii maana
yake wanaishi katika kundi si peke yao
k**a aina nyingine za nyuki.
Wanajenga sega ya nta ndani ya mzinga
wa nyuki na humu wanatunza asali yao .
Kuna aina tatu za nyuki ndani ya kundi
na mzinga wao ambao ni
malkia wa nyuki ni mama wa nyuki
wote ndani ya kundi na kazi yake ni
kutega mayai pekee
nyuki wafanyakazi ni wakazi wengi wa
mzinga na wote ni wa k**e. Ni hao
wanaofanya kazi yote k**a kukusanya
mbelewele, kusafisha mzinga,
kutengeneza nta , kujenga sega,
kumlisha malkia na wadogo, kultetea
mzinga
nyuki dume ni wachache na kazi yao
ya pekee ni kuzaa na malkia; baadaye
wanafukuzwa kwenye mzinga na
hawapewi chakula tena

KWA MAHITAJI YA MIDOLI YA K**E, KIUME, WATOTO, ENGA AINA ZOTE,HOOK AINA ZOTE, SPEND ZA NGUO NA VIATU.  WASILIANA NA MIMI...
19/08/2017

KWA MAHITAJI YA MIDOLI YA K**E, KIUME, WATOTO, ENGA AINA ZOTE,HOOK AINA ZOTE, SPEND ZA NGUO NA VIATU.

WASILIANA NA MIMI

WhatsApp 0768503158
offline 0672812881

Turudi nyuma kidogo tukumbushane simuulizi hii fupi     CHOZI LA MAMAKILA mmoja alimpa jina alijualo yeye. Wengine wakim...
01/05/2017

Turudi nyuma kidogo tukumbushane simuulizi hii fupi

CHOZI LA MAMA
KILA mmoja alimpa jina alijualo yeye. Wengine wakimuita kichaa mgeni, wengine chizi freshi na mengineyo mengi kulingana na wakati. Hakuna aliyejua wapi anatoka, lakini alikuwa katika kundi la vichaa pale mjini. Aliokota makopo na kuzurura nayo, alikula majalalani akigombea chakula na mbwa koko, Mungu alimwepusha na magonjwa na kumfanya acheke peke yake kila mara. Alipokasirika aliponda watu mawe, lakini licha ya hasira hizo baada ya miezi kadhaa akagundulika kuwa ni mjamzito. Ikawa skendo mjini kumfahamu ni nani muhusika wa dhambi ile kwa mtu asiyekuwa na akili timamu. Hakupatikana!! Maisha yakendelea. Ilingojewa miezi tisa ifike aweze kujifungua ili atafutwe mchawi nani. Lakini hata miezi tisa haikufika ile mimba ikatoka, huku dhahiri shahiri yule kichaa akionekana kupitia maumivu makali. Wananchi wakanong’ona kimya kimya kuwa aliyemjaza mimba, amemvizia na kumlisha madawa makali hatimaye ile mimba imetoka. Hilo nalo likasahaulika. Ikapita miezi mingine miwili, akapata mimba tena yule mwanamama ambaye nyumba yake ilikuwa popote pale pasipofaa kukaliwa na mwanadamu wa kawaida. K**a ilivyokuwa awali watu walilaani kitendo hicho alichofanyiwa kichaa mgeni. Mimba ikaanza kukua, lakini hata hii haikufikisha miezi tisa, ikatoka k**a ile mimba ya awali. Lakini hii ilikuja katika mtindo wa aina yake. Kichaa mgeni alizungumza kitu kwa sauti isiyokuwa ya kwake. Alizungumza mambo ambayo kila mmoja alibaki na maswali lakini wengi wakipata majibu. MWAKA MMOJA NA NUSU ULIOPITA. MARIA akiwa amejipumzisha na mume wake asiyekuwa wa ndoa wala wa kutambulika popote bali waliishi uhawara na hatimaye kuzoeana. Wakaitana mume na mke lakini wakiwa hawana mtoto. Ugeni ukawajia siku hiyo, mwanamke mnene mfupi mweusi mwenye macho mekundu alikuwa akingoja nje baada ya mlinzi kumwambia subiri hapo. Maria alitoka akiwa ameongozana na mume wake wakiwa wameshikana viuno katika mtindo wa mahaba. “Nikusaidie nini?” aliuliza Christian ambaye ni mume wa Maria. Yule mama mwenye macho mekundu alijaribu kutabasamu na mdomo wake kufunguka, alikuwa na mapengo, meno ya mbele yote hayakuwa kinywani. Maria alimtazama kwa makini huku akiizuia hali ya kutaharuki iliyotaka kumtwaa. Mama yule mzee alikuwa na mtoto mgongoni. Bila shaka hakuwa mtoto wake labda mjukuu tu. “Wankuru haujambo..” alizungumza yule mama huku akimtazama usoni. “Wankuru nd’o nani tena..” Chris aliuliza huku akimtazama Maria. “Hata mimi nashangaa, ama amekosea nyumba.” Alijibu Maria kwa hofu!! “Wankuru umependeza wee mwanangu, yaani nilijiuliza k**a ningeweza kukupata. Tangu nipoteze namba yako basi nimeshindwa kabisa kukweleza lolote. Hivi ukimuona Gilbert utamkumbuka kweli Wankuru wangu.” Alizungumza kwa furaha na hakuona haya kuyaonyesha mapengo yake, wakati huo uso wake ulikuwa unavuja jasho. Miguu iliyopauka na nguo zake hazikuwa safi. “Maria unamjua…” Chris aliuliza. Maria akakana kwa maraq nyingine. Lakini mama yule aliendelea kuzungumza kwa furaha akisimulia mambo kadha wa kadha. “Mama samahani..kwani unamtaka nani?” aliuliza kwa ghadhabu kidogo Chris. Mama yule akamtazama kwa mshangao. “Mama nimekuuliza unataka tukusaidie nini?” alikazia sasa. “Nimekuja kwa mwanangu, nimemleta mjukuu wangu amwone mama yake. Kwani kuna ubaya…..” akamgeukia Maria, “Wankuru eeh kuna kosa nimefanya mwanangu eeh” aliuliza kwa kubembeleza huku akijitoa katika hatia. “Huyu ni nani Maria na huyo mtoto ni wa nani.” Alihoji Chriss. Maria akajitoa utimamu wake na sasa akawa mbogo. “Kwa hiyo Chris unadhani namjua huyu mwanamke ama. Hivi hujui unaweza kurogwa hivihivi, unamuona mtu wa kawaida huyu!! Chriss unamuona wa kawaida huyu, mtazame macho yake mekundu na hicho kitoto maskini sijui amekirogea wapi kakichukua…amet olewa kafara meno yake na bado watamtoa na huyu mtoo maskini weee!!” alifoka. Maneno yakamwingia Chriss. Yule mama akapigwa na butwaa macho yakamtoka na akazidi kutisha kumtazama. Chriss akaingiwa na maneno ya Maria akamwamuru mlinzi amwondoe yule mama nje. Mlinzi akatii, Maria na Chriss wakakokotana kurejea ndani. Nafsi ya Maria haikuwa katika utulivu hata chembe, alimtambua yule mama ipasavyo, alikuwa ni mama yake mlezi baada ya mama yake mzazi kufariki, mama huyu alimfanyia mengi sana yasiyostahili malipo yale. Maria alitambua kuwa kwa kukiri kuwa yule alikuwa ni mtoto wake wa kumzaa basi ule ulikuwa mwisho wa mahusiano na mwanaume yule ambaye anatamnbua kuwa Maria hajawahi kuzaa na hana ndugu wa karibu sana baada ya wazazi wake kufariki na yeye kukimbilia jijini Mwanza kutafuta maisha. Wakati akiwaza hayo Maria kwa mbali kabisa akakisikia kilio cha yule mama aliyekuwa anaomboleza. “Wankuru…Wankur u, unanikana mimi mbele ya hadhara, unanikana Wankuru, yaani umesahau nilivyokulea mimi, macho yangu mekundu haya si ni kwa sababu yako Wankuru yaani nimepika pombe za kienyeji ili usome Wankuru, nimechochea kuni na kujiharibu ngozi, kifua na macho yangu leo hii unasema mimi mchawi nataka kukuroga Wankuru, uuuuwi!!! Wankuru ukabeba mimba huko kila mtu akakukimbia nimekutunza kwa shida, mume wangu akanipiga hadi kunitoa meno Wankuru leo hii nimekuwa kituko, unasema nimetolewa meno yangu kafara kweli Wankuru. Wankuru ukazaa mtoto, ukanidanganya kuwa unaenda nje mara moja kumbe unamkimbia mwanao, nimekukuzia mtoto Wankuru, nimemtunza kwa mapenzi yote mimi. Si nilikwambia mama yako alitaka atoe mimba yako kutokana nna shida, nikamwambia nitamuhudumia asikutoe na akuzae ukue, nimekulindia uhai wako tangu upo tumboni mwa mama yako, nikakupenda kuliko mama yako mzazi leo hii nimekuwa ombaomba, unanikana mimi na damu yako unaikana Wankuru. Wankuru uuuwi!! Chozi langu la mwisho nilidondosaha siku ile yule mwarabu aliyekupa mimba alipokupiga na kusema hakujui, nilitoa chozi hilo kwa sababu ya kukupenda Wankuru, nikalia na kumlaani yule mwarabu k**a kweli anaikana damu yake Wankuru. Ulikuwa shahidi wankuru, tulipolala njaa ulinisikia nikikimbilia kwa Mganga, niliwahi kukufunga hirizi Wankuru!! Watu waliponiita mchawi nilikwambia Mungu atatulinda na malipo ni hapahapa. Yule mwarabu yupo wapi sasa! Wankuru muogope Mungu we mtoto, Wankuru majibu ya Mungu ni ya kweli hayaongopi. Nimemtumikia tangu usichana wangu hadi leo haongopi, hajanipoa mamilioni ya kung’ara ili unipokee katika nyumba yako nzuri lakini amenipa moyo wa huruma moyo wa mama. Wankuru sio kwamba nilikupenda kisa tu sijapata mtoto, nilikupenda kwa sababu ulikuwa umetengwa na kila mtu. Sasa umempata mtu wa kukupenda umesahau kila kitu na leo kwa mara nyingine nadondosha chozi. Namlilia Gilbert kwa uchungu kwa sababu atakutana na akina Wankuru wenye roho mbaya na akili nyepesi ya kusahau. Watamkana na kumnyanyasa, lakini hatakuwa k**a wewe Wankuru, hatakuwa mwepesi wa kusahau. Atamtegemea Mungu na utakuja kumkumbuka. Chozi hili halitatua chini na kumezwa na ardhi burebure, Mungu ninayemuamini si Mungu wa kisasi lakini atanisuuza moyo wangu na kunionyesha uwepo wake tena. Chozi hili na litue katika utosi wa kichwa chako!! Kichwa chenye nywele bandia zinazoogopa maji ya kijijini kwetu, maji ya chumvi. Chozi hili langu la mwisho hapa duniani liwe chozi lako kwa lolote utakalopitia. Yaani unamnkana mwanao uliyemzaa, Wankuru yaani mimi nilivyolilia mtoto miaka arobaini yote na nisimpate wewe umempata huyu mtoto mtiifu wa kiume unamkana, unamkataa katakata mbele yangu. Wankuru usipomkumbuka Gilbert, Mungu wangu hayupo hai!!!! Naondoka na Gilbert, k**a nilivyojikongoj a hadi kufika huku, nikitukanwa na wakati huohuo nikikutana na wachache wa kunifariji, nikiitwa mchawi na wapumbavu k**a wewe, lakini wapo wachache walioniita mkarimu. Narejea nikiamini wale wanaoutambua ukarimu wangu watanipokea, sitaishi miaka mingi lakini walau nimeishi umri wa kukukuza na kumkuza mwanao. Naenda Wankuru naenda ..” kilio kilikomea pale, Maria alijiwekea tabasamu bandia lakini moyo ukiteketea. Alitambua kuwa ni yeye aliyeitwa wankuru, Maria ni jina lake la mjini tu ambalo Chriss alilitambua. Chris pasi na hili wala lile akamliwaza mkewe huku akimwomba msamaha kwa yote yaliyotokea. Maria akapitiwa na usingizi. Siku iliyofuata akafunga safari kuelekea kijijini kwao, alitegemea kumkuta mama huyo kule, amwombne msamaha na kujirudi. Lakini mwangu wa kilio chake ukamvuruga, akapanda basi asifahamu linakwenda wapi, alijitahidi kuiweka akili yake sawa lakini hakujielewa hadi akajikuta mjini Dodoma. Alishuka k**a Maria, lakini baada ya masaa kadhaa akageuka kuwa KICHAA MGENI. Hakuna aliyemjua. Akajazwa mimba ya kwanza na haikudumu kuzaa kiumbe chochote, akajazwa ya pili na mtu asiyefahamika. Ni katika mimba hii alizungumza mambo mengi sana yaliyomfanya hadi afike hapo. Labda alipewa akili ndogo ya mwisho ya kusema ili watakaojifunza na wajifunze. Wasamaria wakahitaji kumsaidia, wakajipanga kwa ajili ya siku iliyofuata wamchukue Maria. Lakini hakuwa Maria tena…..alikuwa hayati Maria. Alikuwa mfu!! Na hakupatikana ndugu wa kumzika. Maiti yake yakazikwa na manispaa!! Aliishi maisha magumu, akampata mwenye upendo akamtunza, watuy wabaya wakamjaza mimba bado yule mtu mwenye upendo hakumtelekeza, akazaa na kutelekeza mtoto lakini mtu mwenye upendo akatunza kiumbe. Maria akageuka na kulikana jina lake alipokuwa mjini, akamkana hata yule mtu mwenye upendo akamkana na mtoto wake!!! CHOZI LA MAMA likaishi katika utosi wake, Mungu akamwadhibu Maria kadri ya kilio cha mama yule!! Mama mkarimu hakufa mapema aliishi!! Akakitunza kiumbe kinachoitwa Gilbert kwa hekima zote, kikakua wasamaria wakasaidia kikasoma. Na hata kilipofikisha umri wa kujitambua, kikiwa darasa la tano. Mama mkarimu akatokwa na uhai huku akitabasamu!!! UJUMBE: 1. MAMA ni kiumbe cha kipekee, hupaswi kumsaliti mama yako…..itunze ahadi k**a yeye aliyekutunza kwa miaka mingi bila kuvunjika moyo. 2. STAREHE ZA MUDA MFUPI zisikufanye uwasahau uliosota nao kwa miaka lukuki. 3. MUNGU hujibu!! Muamini yeye sasa. MWISHO!!!! **BOFYA LIKE, k**a umejifunza kitu siku ya leo, weka COMMENT yako…..SHARE KWA WENGINE!!!

Used flat screen inauzwa:Shs. 280000/=Ukubwa inch: 24Aina: Pinetech flat screen
15/02/2017

Used flat screen inauzwa:
Shs. 280000/=
Ukubwa inch: 24
Aina: Pinetech flat screen

Address

Cape Town
456787

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when WNB posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share