Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar

Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Ukurasa rasmi wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ)

Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar tunashiriana na Watanzania wote kuadhimisha Miaka 62 ya Sikukuu ya Muungano wa Tanga...
26/04/2026

Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar tunashiriana na Watanzania wote kuadhimisha Miaka 62 ya Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

07/04/2026

15/02/2026

Mrajis wa Vyama vya Michezo Zanzibar Ndugu, Abubak Lunda amekipongeza Chama Cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) kwa kuendeleza Ushirikiano wao katika kutafuta viongozi kwa utaratibu ulioweka katika kanuni zao.

15/02/2026

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Ndugu Ali Bakar Ali (Cheupe) akitangaza Matokeo ya Uchaguzi wa Chama Cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA).

Katika Uchaguzi huo Uliofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Tumekuja Mjini Unguja Kamati imemtangaza Ndugu Said Suleiman Said kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho.

15/02/2026

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Ali Abdulghulam Hussein akitoa neno kwa Chama Cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) jinsi gani wanatakiwa kukiendesha Chama hicho ili kiweze kukuwa zaidi.

Naibu Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar Ali Abdallagulam Hussein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Za...
15/02/2026

Naibu Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar Ali Abdallagulam Hussein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikishirikiana na Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Zanzibar wataendelea kutoa ushirikiano ili kuweza kuimarisha Chama Cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA).

Aliyasema hayo wakati alipokuwa akifunguwa mkutano wa uchaguzi kwa wagombea Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Tumekuja Mjini Zanzibar.

Amesema lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya nane inayongozwa na Rais Hussein Ali Mwinyi imeamua kujenga Afisi ya Baraza la Taifa la Michezo zikiwemo Afisi za vilabu vya michezo ndani ya afisi hiyo.

Hata hiyo amesema serikali kwa kushirikiana na chama hicho (ZABESA) kuwa mstari wa mbele katika kuisaidia jamii kimazingira na kiafya na kuweza kutafuta mbinu ya kujipatia fedha za kujiendesha chama hicho.

Nae Katibu wa Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA) Khamis Akhui Khamis akiwasilisha risala kwa Naibu huyo alisema lengo la chama hicho ni kuhamisisha jamii katika kuvikusanya vilabu katika kuviunganisha Ili kujenga ushirikiano.

Hata hivyo alisema wanaendelea kushirikiana na taasisi za serikali pamoja na taasisi husika katika kuwahamasisha ili kuhakikiaha wananchi wote kufanya mazoezi na kuimarisha Afya iliyo bora.

Aidha alisema katika risala hiyo lengo kuu ni kuwapata viongozi watakaoendeleza Chama hicho na kuendeleza vilabu vilivyopo Unguja na Kisiwani Pemba na kutoa ushirikiano kati ya Wizara na Chama chao.

Hata hivyo Mwenyekiti wa chama Cha mchezo huo (ZABESA) Said Suleiman Said alisema chama Chao kina haki ya kuwakilisha na kuwashajihisha wananchi katika kujiunga chama Chao.


29/01/2026
Tunaungana na Watanzania wote kukutakia heri ya mfanano wa siku ya Kuzaliwa Mhe. Dr.
27/01/2026

Tunaungana na Watanzania wote kukutakia heri ya mfanano wa siku ya Kuzaliwa Mhe. Dr.

Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar BTMZ Ndugu Said Kassim ameshiriki Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la...
15/01/2026

Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar BTMZ Ndugu Said Kassim ameshiriki Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Muungano kwa upande wa Netball.

Mashindano hayo yamefunguliwa rasmi katika viwanja vya michezo (Indoor) vinavyopatikana ndani ya Uwanja wa New Amaan Complex, ambapo Bingwa mtetesi KVZ kutoka Zanzibar wamekutana na timu ya JKT kutoka Tanzania.

Mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Mashindano hayo alikua ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Ali Abdulghulam Hussein.

.riziki.pembe

Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), Ndugu Said Kassim Marine akiwa kwenye matukio ya picha katik...
14/01/2026

Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), Ndugu Said Kassim Marine akiwa kwenye matukio ya picha katika Fainali ya Kombe la Mapinduzi ambayo iliwakutanisha Azam FC dhidi ya Yanga SC katika Uwanja wa Gombani.

Haya ni miongoni mwa majukumu makubwa ambayo Katibu Marine amekua akiyafanya katika kumsaidia Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Ali Mwinyi katika kuboresha Michezo Zanzibar.

.riziki.pembe

Uongozi na wafanyazi wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) kwa pamoja tunaungana na Wananchi wote kuadhimisha sh...
12/01/2026

Uongozi na wafanyazi wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) kwa pamoja tunaungana na Wananchi wote kuadhimisha sherehe za 𝐌𝐢𝐚𝐤𝐚 𝟔𝟐 𝐲𝐚 𝐌𝐚𝐩𝐢𝐧𝐝𝐮𝐳𝐢 𝐲𝐚 𝐙𝐚𝐧𝐳𝐢𝐛𝐚𝐫

Address

Unguja

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share