Serengeti Yetu

Serengeti Yetu Serengeti District is located on the Eastern part of Mara region. The District is one of the six District Councils constitute Mara region. Karibuni

KATA 30 WILAYANI SERENGETI ZANUFAIKA NA MILIONI 88 ZA MFUKO WA JIMBO.Mbunge Jimbo la Serengeti Mhe. Mary Daniel Surati  ...
20/05/2026

KATA 30 WILAYANI SERENGETI ZANUFAIKA NA MILIONI 88 ZA MFUKO WA JIMBO.

Mbunge Jimbo la Serengeti Mhe. Mary Daniel Surati leo Mei 20, 2026 amefanya hafla ya mgawanyo wa fedha za mfuko wa Jimbo Shilingi Milioni 88 kwa Kata 30 za Wilaya ya Serengeti.

Hafla hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kushuhudiwa na Madiwani wa kata zote pamoja wananchi, imehusisha ugawaji wa mifuko 2597 ya saruji ikiwa ni fedha za mfuko wa j
Jimbo na mchango wa mifuko 500 ya saruji kutoka Taasisi ya Nyansaho (Nyansaho Foundation), Hundi ya Shilingi Milioni 25 kwa ajili ya ukamikishaji wa Zahanati ya Kisaka sambamba na madawati yenye thamani ya Shilingi Milioni 2 kwa Shule ya Msingi Kambarage.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mhe. Mary amesisitiza kuwa, lengo la mgawanyo wa fedha hizo ni kuhakikisha kuwa miradi yote ya elimu na afya katika Kata zote za Wilaya ya Serengeti inakamilika ili wananchi waweze kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kupata huduma za elimu na afya.

Sambamba na hayo ameongeza kuwa kipaumbele cha Serikali ya awamu ya sita ni kuwajali wananchi wake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora za muhimu katika maeneo yao huku akiwasisitiza Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha wanasimamia matumizi sahihi ya saruji hiyo na fedha.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Wakili Angelina Marco Lubella amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Serengeti kwa uwazi wake katika mgawanyo wa fedha za mfuko wa jimbo huku akimhakikishia usimamizi mzuri wa fedha hizo ili ziweze kutimiza lengo lililokusudiwa.

Nao Waheshimiwa madiwani wamepongeza hatua ya Mbunge huyo kwa uamuzi wa kutoa mifuko hiyo ya saruji na fedha kwani inaenda kukamilisha miradi mbalimbali iliyokuwa imekwama katika kata zao.

BARAZA LA MADIWANI LAIPONGEZA SERIKALI KWA KUFIKIA HATUA MUHIMU KUELEKEA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SEREN...
20/05/2026

BARAZA LA MADIWANI LAIPONGEZA SERIKALI KWA KUFIKIA HATUA MUHIMU KUELEKEA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SERENGETI.

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, limeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuweka mkazo thabiti katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Serengeti (Serengeti International Airport).

Pongezi hizo zimetolewa Leo Mei 20, 2026 wakati wa Kikao cha Baraza hilo, ambapo madiwani hao wamebainisha kuwa hatua ya Serikali kuungiza mradi huo katika bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka (2026/2027) sambamba na  kusimamia kwa ukaribu na kuharakisha taratibu za mradi huo kuanzia kutekekezwa, ni ishara tosha ya dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Serengeti na Mkoa wa Mara kwa Ujumla huku wakieleza kuwa ujenzi wa uwanja huo umekuwa kilio cha muda mrefu cha wana-Serengeti.

Akizungumza kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani hao, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Ayub Mwita Makuruma amesisitiza kuwa kukamilika kwa uwanja huo kutafungua fursa kubwa za kiuchumi, hususan katika sekta ya utalii, 

"Ujenzi wa Uwanja wa ndege ndani ya Wilaya ya Serengeti kimekiwa kilio chetu cha muda mrefu, hivyo hatua hii haitasaidia tu kuongeza idadi ya watalii na mapato ya halmashauri, bali pia itachochea biashara na kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wa eneo hilo". Amesema Mhe. Makuruma 

Aidha, Baraza la Madiwani limeahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mamlaka zote zinazohusika na ujenzi huo ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa na kuiomba serikali kuendelea kutenga na kutoa fedha za utekelezaji bila kukwama, ili ndoto hiyo ya kihistoria kwa wakazi wa Serengeti itimie kikamilifu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Ayub Mwita Makuruma akiongoza Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiw...
19/05/2026

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Ayub Mwita Makuruma akiongoza Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani mapema leo Mei 19, 2026 uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.

RAS MARA AZITAKA SACCOS KUSAIDIA VYAMA VYA MSINGI Katibu Tawala Mkoa wa Mara Ndg. Gelard Kusaya amevitaka vyama vya Akib...
19/05/2026

RAS MARA AZITAKA SACCOS KUSAIDIA VYAMA VYA MSINGI

Katibu Tawala Mkoa wa Mara Ndg. Gelard Kusaya amevitaka vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) kuwa msingi na chachu kwa vyama vya msingi ilikusaidia kukuza mitaji itakayosaidia kutoa huduma za kifedha kwa riba na nafuu  kwa maendeleo ya wanaushirika.

Kusaya, ametoa kauli hiyo leo Mei 19, 2026 Wilayani Serengeti, Mkoani Mara wakati akifungua wiki ya jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoani Mara ambapo, amesema k**a vyama vya akiba na  kukopa vitasaidia vyama vya msingi vitaleta tija katika kukuza kuendeleza maendeleo ya ushirika.

Aidha, ameitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika kushirikiana na wadau katika kutoa elimu ili watu wenye mahitaji maalum nao kunufaika kupitia ushirika k**a wanavyonufaika watu wengine.

Nae Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Mara (WAMACU) Ndg. Samweli Gisiboye amesema kuwa bei ndogo ya soko lisilotabirika kutokana na ushindani mdogo unaosababishwa na uwepo wa wananunuzi wachache wa mazao ya kimkakati ni chanzo cha kufifisha shughuli za uzarishaji sambamba na kupelekea madeni ya pembejeo za kilimo katika vyama hivyo, na kuiomba Serikali kuzingatia suala hilo.

Aidha naye Mrajisi Msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Mara Ndg. Lucas Kihondere amesema kwa sasa sitakabadhi za ghala ndani ya Mkoa wa Mara, zimeanza kutumika miongoni mwa vyama, jambo lililofanikisha baadhi yao kununua trekta kwa ajili ya kujiinua katika sekta ya kilimo cha Pamba na Dengu.

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Je...
15/05/2026

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imetembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Utawala ambao unatazamiwa kukamilika kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mradi huo ulioanza kutekelezwa Aprili 2025, utagharimu jumla ya Shilingi Bilioni 4.5 ikiwa ni fedha kutoka serikali kuu ambapo mpaka sasa utekelezaji wa  mradi huo umefikia asilimia 39.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Elias Merengo Mwita, apongeza hatua iliofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo na kukusisitiza nguvu kazi kuongezeka ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

Sambamba na hayo Mhe. Merengo amesisitiza wakazi wa Serengeti kupewa kipaumbele hususani vibarua katika ujuenzi wa mradi huo ili waweze kunufaika na uwepo wa mradi huo ndani ya Wilaya yao.

HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI YATOA MKOPO WA PIKIPIKI 13 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 39 KWA VIJANA.Halmashaur...
06/05/2026

HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI YATOA MKOPO WA PIKIPIKI 13 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 39 KWA VIJANA.

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imetoa mkopo wa Pikipiki 13 zenye thamani ya shilingi milioni 39 kwa vikundi vinne vya vijana, kupitia mikopo ya asilimia 10 ya makusanyo ya Halmashauri.

Akikabidhi pikipiki hizo leo Mei 06, 2026 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Ndg. Jabir Athuman amewataka wanufaika wa pikipiki hizo kuzitunza na kuzitumia vyema ili ziweze kuwa tija katika kuwainua kiuchumi huku akiwasisitiza kurejesha kwa wakati mkopo huo.

Kwa upande wake Afisa Vijana Wilaya ya Serengeti Ndg. Isack Mwakyuse amesema vikundi vilivyonufaika na mkopo huo ni pamoja na kikundi cha vijana Nyamihuru pikipiki 3, vijana Nyabihore pikipiki
3, kikundi cha Smart Bodaboda pikipiki 4 na kikubdi cha umoja wa wasafirishaji NMB pikipiki 3, hivyo kuleta jumla pikipiki 13 zenye thamani ya Tsh. 39,000,000.

DC ANGELINA AMALIZA UTATA WA ENEO LA MALISHO ULIODUMU KWA MUDA MREFU KATIKA MBUGA YA KEMGESI.Mkuu wa Wilaya ya Serengeti...
06/05/2026

DC ANGELINA AMALIZA UTATA WA ENEO LA MALISHO ULIODUMU KWA MUDA MREFU KATIKA MBUGA YA KEMGESI.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Wakili Angelina Marco Lubela, amemaliza mgogoro wa muda mrefu katika Mbuga ya Kemgesi,Tarafa ya Ikorongo,mgogoro uliohusisha uvamizi wa eneo lililotengwa na kijiji hicho kwa ajili ya malisho.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza kusikiliza utatuzi wa mgogoro huo katika mkutano uliofanyika mei 04, 2026 Mhe. Angelina akiongozana na k**ati ya Usalama pamoja na Wataalam wa Halmashauri, amesema Serikali haitafumbia macho uvamizi wowote wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kichumi na kijamii.

Katika Mkutano huo, ametoa siku 14 kwa watu waliovamia eneo hilo ambalo limekuwa likitumika na vijiji vya Kemgesi, Ring’wani na Masinki toka kipindi cha Ujamaa kwa takribani miaka 52 sasa kupisha mara moja huku akiagiza kuchukuliwa hatua kali kwa wote waliohusika kwenye mauzo ya ardhi katika eneo hilo.

Amesisitiza kuwa uvamizi wa maeneo ya malisho unahatarisha usalama wa mifugo na kuchochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji, jambo ambalo Serikali haitovumilia, hivyo akawataka wafugaji wote kutumia eneo hilo bila kizuizi chochote.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi katika tarafa hiyo, wamepongeza hatua ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti kurejesha eneo hilo mikononi mwa wanakijiji wote ili kutumika kwa ajili ya malisho k**a lilivyokuwa limetengwa hapo awali huku wakiaidi kuendelea kulinda eneo hilo dhidi ya wavamizi.

ZOEZI LA UTOAJI WA CHANJO YA POLIO AWAMU YA PILI WILAYANI SERENGETI KUANZA MEI 7, 2026.Kamati ya Afya ya Msingi Ngazi ya...
05/05/2026

ZOEZI LA UTOAJI WA CHANJO YA POLIO AWAMU YA PILI WILAYANI SERENGETI KUANZA MEI 7, 2026.

Kamati ya Afya ya Msingi Ngazi ya Jamii (PHC) Wilaya ya Serengeti imefanya kikao na wahamasishaji ngazi ya jamii kuhusu chanjo ya polio, kikao kilicholenga kuongeza uelewa juu ya ugonjwa wa polio sambamba na chanjo hiyo ya matone itakayoanza kutolewa kwa awamu ya pili kuanzia Mei 07, 2026 hadi Mei 10, 2026.

Akizungumza katika Kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Wakili Angelina Marco Lubela amewataka washiriki wa kikao hicho kuhakikisha wanasambaza elimu juu ya umuhimu wa chanjo hiyo ili kuongeza uelewa wa jamii sambamba na kuondoa fikra potofu zinazoweza kujitokeza juu ya chanjo hiyo.

Aidha, Mhe. Angelina ameongeza kuwa chanjo hii ni salama hivyo akawataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo hiyo kwa mara ya pili kwani ni kinga ya mtoto dhidi ya ugonjwa wa polio ambao huweza kusababisha ulemavu kwa watoto.

Zoezi la kampeni ya utoaji chanjo ya Polio awamu ya pili katika Wilaya ya Serengeti litakaloanza Mei 07, hadi 10, 2026 litahusisha vijiji vyote 78 na Miata 23 katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambapo watoto wenye umri chini ya Miaka 10 watapata chanjo hiyo katika zoezi litakaloendeshwa mashuleni na nyumba kwa nyumba.

DC SERENGETI AWATAKA WANUFAIKA WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KUTOTUMIA MIKOPO HIYO KUFANYA ANASA.Mkuu wa Wilaya ya Serengeti ...
04/05/2026

DC SERENGETI AWATAKA WANUFAIKA WA MIKOPO YA ASILIMIA 10 KUTOTUMIA MIKOPO HIYO KUFANYA ANASA.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Wakili Angelina Marco Lubela amewataka wanufaika wa mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri kuacha kutumia mikopo hiyo kufanyia starehe na badala yake watumia kuendeleza miradi ambayo waliiombea.

Mhe. Angelina ameyasema hayo leo Mei 4, 2026 katika hafla ya kukabidhi hundi kwa wanufaika wa mikopo hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ambapo amesema ili mikopo hiyo iweze kurejeshwa kwa wakati na kwa uaminifu, wanufaika wanatakiwa kutumia mikopo hiyo kuendeleza miradi waliyoombea ili kusaidia wengine kunufaika na fedha hizo.

Aidha, Mhe. Angelina amesema Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imetenga Shilingi Milioni 383 inayotokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani huku akimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Maulid Madeni (PhD) kwa kutenga milioni 83 kutoka mapato ya ndani na fedha zilizorejeshwa kutoka kwenye mikopo shilingi Milioni 300 na kuongeza kuwa Serikali inamatumaini kuwa fedha hizo zitabadilisha maisha ya wananchi hao.

“Matarajio ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan nikurejesha furaha kwa wananchi hivyo ninyi Halmashauri yetu ya Serengeti kupitia kaka yangu Madeni mmelifanya kweli hongereni sana niwaombe sana wanufaika nendeni mkarejeshe fedha hizo kikamilifu ili na wengine wapate” amesema Mhe. Angelina

Aidha kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Ndg. Victor Rutonesha amesema kwa sasa urejeshaji wa mikopo hiyo unafanyika vizuri ambapo umesaidia kufanikisha utaoji wa mikopo kwa vikundi 52 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

04/05/2026

Address

P. O BOX 176
Musoma
MARA

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Serengeti Yetu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Serengeti Yetu:

Share