Pre Marriage Talk

Pre Marriage Talk Pre Marriage Talk is a ministry under the founder Rev. Isaac Challo (PhD) and his wife Betty Challo. They believe good marriage is prepared before the marriage.

They teach, counsel and pray for young people to prepare them to be good husbands and wives.

10/09/2026

Every Sunday after English service we offer Pre marriage counselling for free, karibu, Tuma ujumbe Pre marriage counselling kwenda 075205276.

πŸ’ PRE MARRIAGE TALKJE, UNA WITO WA KUMTUMIKIA MUNGU?Je, bado hujaoa au kuolewa?Kumbuka, mwenza sahihi anaweza kuwa nguzo...
24/07/2026

πŸ’ PRE MARRIAGE TALK
JE, UNA WITO WA KUMTUMIKIA MUNGU?
Je, bado hujaoa au kuolewa?
Kumbuka, mwenza sahihi anaweza kuwa nguzo ya kutimiza wito wako, huku asiye sahihi anaweza kuwa kikwazo kwa huduma na kusudi la Mungu maishani mwako.
Jiunge nasi kila wiki ujifunze jinsi ya kuchagua mwenzi ambaye: βœ… Atatambua wito wako. βœ… Ataheshimu vipawa ulivyopewa na Mungu. βœ… Atawezesha huduma yako kukua. βœ… Atakuwa mshirika wa kweli katika kutimiza kusudi la Mungu.
Na: Rev. Isaac Challo & Betty Challo
πŸ“± Tufuatilie kila wiki kupitia:
Facebook
TikTok
Instagram
YouTube
"Usichague mwenzi kwa hisia pekee; chagua kwa hekima na kusudi la Mungu."

24/07/2026

Uchaguzi wa mwenzi wa Maisha ni moja kati ya chaguzi muhimu sana katika maisha. Kosa katika kufanya uchaguzi huu huleta madhara ya kudumu. Usiruhusu hisia ziishinde akili katika mchakato huu. Muombe Mungu akupe neema ya kukutana na mtu sahihi atakayekusaidia kutimiza makusudi ya Mungu katika ndoa utakayoianza. USIKURUPUKE. KARIBU PRE MARRIAGE TALKπŸ‘‡
https://youtu.be/vxPfQUMtnN4?si=xtK7NHZqQzvSxdEZ

17/07/2026

Pre Marriage Talk- Wakati mwingine vijana wanaogopa kuingia kwenye ndoa kwa sababu ya jinsi waliopo kwenye ndoa wanaumizana na kukosa ushuhuda wa furaha, amani na utulivu k**a ilivyokusudiwa na Mungu katika mpango wa Mungu wa Ndoa.
https://youtu.be/IwjAjPx_rj8

Ni muhimu sana kijana au binti aliyeokoka kufanya maamuzi sahihi yanayohusu kuoa au kuolewa, kwa sababu uhusiano wa ndoa...
14/07/2026

Ni muhimu sana kijana au binti aliyeokoka kufanya maamuzi sahihi yanayohusu kuoa au kuolewa, kwa sababu uhusiano wa ndoa una athari kubwa kwa maisha yake ya kiroho, kihisia, na hata kimwili. Biblia inasisitiza hekima, uongozi wa Roho Mtakatifu, na ushauri wa kiroho katika maamuzi haya. Kufanya maamuzi sahihi kuhusu kuoa au kuolewa ni kuamua mustakabali wa maisha, ujuzi, huduma, furaha, na wokovu wako. Kijana au binti aliyeokoka anatakiwa kutafuta mwelekeo wa Mungu, ushauri wa kiroho, na uongozi wa Neno kabla ya kuchukua hatua. Kijana unapooa au binti anapolewa unaingia katika muungano na mtu au familia itakayokuwa ni chanzo za furaha au huzuni. Maamuzi ya unamwoa nani au unaolewa na nani ni maamuzi yatakayo athiri maisha yako yajayo. Maamuzi juu ya aina ya mtu unayeoa au kuolewa naye yataathiri aina ya familia utakayokuja kuwa nayo. Unafanya maamuzi ambayo yatakuinua au yatakudidimiza. Ni muhimu sana upate mwenzi sahihi kwa sababu:
1. Mwenzi atakuwa na mguso chanya au hasi katika maisha yako
Mnapooana kila mmoja atakwenda kumuathiri mwenzake kwa uzuri au kwa ubaya. Ushahidi wa mabadiliko ya kitabia, mabadiliko ya kiroho, mabadiliko ya kimandeleo na mabadiliko ya kiuchumi yako wazi kwa wanandoa wengi baada ya kuoana. Kuna mwanandoa ambaye atakufanya uwe bora katika maeneo kadhaa lakini kuna mwenzi ambaye anaweza kufanya mambo yako, maono na mipango yako ikaharibika. Kuna mwenzi ambaye anaweza kuwa dream killer (muua maono) au dream booster (muwezesha maono). Ni lazima uwaze aina ya mwenzi wa ndoto yako na umwombe sana Mungu akukutanishe na mtu ambaye ataboresha maisha, maono na mipango yako.

Enjoy the videos and music you love, upload original content, and share it all with friends, family, and the world on YouTube.

30/04/2026

TANGAZO MAALUM – SEMINA YA MAANDALIZI YA NDOA πŸ’

Takwimu zinaonesha wazi kwamba talaka zinaongezeka kwa kasi kubwa kati ya mwaka 2023–2025.
Cha kusikitisha zaidi, wanandoa wengi wanaotalikiana huwa wameishi pamoja kwa muda mfupi tu β€” kati ya mwaka 1 hadi 3.

Utafiti unaonesha kuwa takribani asilimia 80 ya wanaotalikiana hawakupata mafunzo ya awali kabla ya ndoa.

πŸ‘‰ Je, ungependa kuepuka changamoto hizi?
πŸ‘‰ Je, ungependa kuingia kwenye ndoa ukiwa umejiandaa kikamilifu?

Huduma ya Pre Marriage Talk chini ya
Pastor Isaac Challo na Betty Challo
imejikita katika kutoa elimu muhimu kwa vijana, kuwasaidia kujenga ndoa imara na kuepuka migogoro inayoweza kuzuilika.

🧠 β€œTo be pre-informed is to be forearmed”
(Kuwa na taarifa kabla ni kuwa na silaha ya ushindi)

πŸ“… TAREHE: 07.07.2026
⏰ MUDA: Saa 3:00 Asubuhi
πŸ“ MAHALI: Kanisa la Living Water – Kawe

πŸ‘₯ Waandaaji: CASFETA – Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam

🎯 Nani anakaribishwa?

Vijana wote
Wanaotarajia kuingia kwenye ndoa
Wazazi na walezi

🀝 Unaweza pia kusaidia na ku-support huduma hii kwa kuwasiliana na:
πŸ“ž Rev. Isaac Challo – 0752805276

06/12/2025

Kijana ambaye hujao na Binti ambaye hujaolewa unahitaji kusoma kitabu hiki. Kina madini yatakayokunusuru na MIGOGORO YA ndoa isiyo ya lazima. Mambo matano unayotakiwa kuyajua kuhusu mwenzi mtarajiwa yatakuandaa kisaikolojia na bad surprises za ndoa. Tuma ujumbe kwa simu 0655 383897.

Address

Mbweni

Telephone

0752805276

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pre Marriage Talk posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Pre Marriage Talk:

Shortcuts

Share