12/11/2021
Mwanzo 35 (Maswali & Majibu)
[1] Nani wahusika wakuu katika sura hii? (Mwanzo 35) Yakobo, Debora, Rebeka, Raheli, Benyamini, Reubeni, Bila, Isaka, Esau.
[2] Yapi mawazo makuu katika sura hii? (Mwanzo 35)
(a) Mungu anamwamuru Yakobo akae Betheli, na kujenga madhabahu huko (1)
(b) Yakobo anaamuru familia yake iondoe sanamu: wajisafishe, na kubadili mavazi, katika maandalizi ya kwenda Betheli. Hili wanatii. (2-3)
(c) Kisha Yakobo anazika miungu yake migeni chini mti karibu na Shekemu, na kambi linasafiri kwenda Betheli (4)
(d) Wakanaani wanaogopa familia ya Yakobo, hivyo hakuna anayethubutu kuwafuatilia katika safari yao (4)
(e) Wanapofika Betheli, Yakobo anajenga madhabahu na kupaita mahali hapo El-Bethel (6–7). Debora, mjakazi wa Rebeka, anakufa, naye anazikwa chini ya Betheli chini ya Mwaloni. (8)
(f) Mungu anamtokea Yakobo, anathibitisha jina lake kuwa Israeli, na kurudia upya ahadi (9-13)
(g) Hivyo anajenga mnara, anamimina mafuta hapo, na kupaita mahali hapo Beth-eli (14-15)
(h) Wanaposafiri kutoka Beth-el kwenda Ephrathi; Raheli anakufa akiwa anamzaa Benyamini (16-18)
(i) Raheli anazikwa akiwa njia kuelekea Ephrathi (yaani, Bethlehemu). ~ (19)
(j) Naye Yakobo anajenga mnara kwenye kaburi lake, ambao ni mnara wa kaburi la Raheli hadi leo. (20)
(k) Reubeni analala na mkewe baba yake: analala na Bilha suria wa babaye (22)
(l) Sura hii hubainisha orodha ya wana kumi na mbili wa Yakobo (23-26)
(m) Yakobo anamtembelea Isaka, babaye, huko Mamre, au Kirjath Arba (yaani, Hebroni), alikokuwa ameishi Ibrahim una Isaka (27)
(n) Sura hii huhitimisha kwa taarifa ya mauti ya Isaka na tukio lililofuatia la maziko ya wanawe, Yakobo na Esau (28–29).
[3] Ni tukio gani la Biblia linalofanyika/lililotajwa katika sura hii? (Mwanzo 35)
MATUKIO YANAYOFANYIKA:
(a) Yakobo anahamia Betheli • Mwa 35:1–7
(b) Mlezi wa Rebeka anafia Betheli • Mwa 35:8
(c) Mungu anatokea Betheli • Mwa 35:9–15
(d) Raheli anamzaa Benyamini halafu anakufa • Mwa 35:16–20
(e) Reubeni analala na Bila • Mwa 35:21–22
(f) Isaka anafia Hebroni • Mwa 35:27–29
MATUKIO YALIYOTAJWA:
(a) Lea anawapata wana wanne • Mwa 29:31–35 (Mwa 35:23)
(b) Lea anawapata wana watatu wengine • Mwa 30:17–21 (Mwa 35:23)
(c) Raheli anamzaa Yusufu• Mwa 30:22–24 (Mwa 35:24)
(d) Bila anawapata wana wawili • Mwa 30:5–8 (Mwa 35:25)
(e) Zilpa anapata wana wawili • Mwa 30:10–13 (Mwa 35:26)
[4] Nini ambacho Mungu alitamani Yakobo afanye? Mungu alimwambia Yakobo arudi wapi? (1) Aende kuishi Betheli.
[5] Je umewahi kupata uzoefu wa “Kurudi Betheli”? Jadili.
• Mungu anamwita kila mmoja wetu “arudi Betheli" (v. 1), mahali pa njozi na nadhiri; mahali pa maombi na saumu. Mtu anapotanga mbali k**a ilivyokuwa kwa Yakobo, hana lolote la kufanya isipokuwa kurejea mahali pa wakfu na kufanya upya nadhiri zake.
• Najua hili kutokana na uzoefu wangu binafsi na Bwana. Kumbuka: “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” (Isaya 59:1–2)
[6] Yakobo alijiandaaje kwa ajili ya safari hii? Aliwahimiza watu wa nyumba yake wafanye nini? (2-4) Waweke mbali sanamu, na kujisafisha, na kubadili mavazi yao.
“Matarajio ya kukutana na Mungu huko Betheli ilisababisha kazi makini ya matengenezo. Kulikuwepo mambo mengi ya kufanywa kabla Yakobo na nyumba yake kuwa tayari kukutana uso kwa uso na Bwana (angalia Amosi 4:12; 1 Yohana 3:3). Nje ya mazingatio kwa ajili ya wakeze, Yakobo alikuwa amevumilia uwepo wa sanamu katika mahema yao. Miungu hii migeni pengine ilihusisha terafimu ambayo Raheli alikuwa ameiba kutoka kwa babaye (Mwa. 31:19), sanamu za watumishi wake, na zingine zilizomilikiwa na wanawe kupitia nyara za Shekemu.”
“Utakaso wa nje wa mwili na kubadilisha mavazi mengine kuliwakilisha utakaso wa kiroho na kimaadili wa akili na moyo (angalia Isa. 64:6; 61:10). Huduma ya Mungu haipaswi kuanzwa bila maandalizi husika (angalia Luka 14:28).” (The Seventh Day Adventist Bible Commentary, Vol. 1/ Genesis 35:1–2)
(kwa taarifa zaidi angalia sehemu ya 1-BSG-35T katika Mwongozo huu)
[7] Mungu alimwambia nini Yakobo alipomtokea tena? (10-12) Alimbariki na kurejesha upya agano.
[8] Ni vidokezo gani mahususi vilivyorudiwa katika agano hili lililofanywa upya katika 35:9-12?
(a) “Jina lako ni Yakobo; … lakini Israeli litakuwa jina lako.”
(b) “Mimi ni Mungu Mwenyezi.”
(c) “uzidi ukaongezeke”
(d) “Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako,” na
(e) “wafalme watatoka viunoni mwako.”
(f) “Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.”
Sasa, hebu tufanye marudio ya kile ambacho Mungu anamwahidi Yakobo hapa:
(a) Jina jipya,
(b) Uhakikisho,
(c) Kuzaa,
(d) Umati mkubwa,
(e) Mataifa & Wafalme kutoka kwa Ibrahimu >>>Isaka >>>Yakobo,
(f) Nchi/ Umiliki.
Linganisha maandiko yafuatayo:
(a) Mwa 26:23–24
(b) Mwa 28:14a
(c) Mwa 35:11b
(d) Mwa 46:3
(e) Mwa 48:3–4
(f) Law 26:9
[9] Nini kilitokea baada tukio hili la kukutana na Mungu? Yakobo aliitikiaje? (14-15)
Mwanzo 35:14–15 — 14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake. 15 Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.
[10] Nini kilimtokea Raheli wakati ule Benyamini alipozaliwa? (16-19) “akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito.”
[11] Ni upotevu gani mkuu uliompata Yakobo alipokaribia Bethlehemu? (19) Kifo cha Raheli.
[12] Raheli alifia wapi? Alizikwa wapi? (17–19) Familia hii inaposafiri kutoka Beth-eli hadi Ephrathi. Raheli alizikwa akiwa njiani kuelekea Ephrathi (yaani, Bethlehemu).
[13] Yakobo alikumbukaje kifo cha mkewe mpendwa? (20) Alisimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo.
[14] Ni jina gani lingine alilopewa Benyamini? (18) Ben-oni
“Kuzaliwa kwa Benyamini kuliashiria utimizwaji wa shauku ya Raheli katika kumpatia jina Yusufu, kwamba Mungu angempatia mwana mwingine (angalia katika sura ya 30:24). Anapokuwa katika hali ya kufa wakati wa kuzaa anamwita mwana huyu Ben-oni, “mwana wa uchungu wangu” au “mwana wa msiba wangu.” Katika mazingira haya, kwa mtazamo wake, lilikuwa jina sahihi.” (SDABC1/ Genesis 35:18)
[15] Ni dhambi gani aliyotenda Reubeni? (22) Alilala na suria wa Yakobo na mjakazi wa Raheli, Bila. Huu ulikuwa uhusiano mbaya sana; kwa vile Masuria walikuwa k**a wake halali.
“Hili liliongeza mateso yake (Yakobo), na kuifanya maradufu, kumpoteza Raheli kwa mauti, na mjakazi wake Raheli, suria wake, kunajisiwa na mwanawe, na ambaye inawezekana kabisa aliachana naye baada ya hapo. Hili, japo ni dhambi ovu sana ya mwanawe, lakini inaweza kuchukuliwa k**a marudi kwa Yakobo, kwa kuwachukua masuria.” (John Gill)
[16] Yakobo alikuwa na jumla ya wana wangapi? (22) Kumi na mbili
Wana wa Lea: Reubeni (mwana wa kwanza wa Yakobo), Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, na Zabuloni.
Wana wa Raheli: Yusufu na Benyamini.
Wana wa Bila ~ (mjakazi wa Raheli): Dani na Naftali.
Wana wa Zilpa ~ (mjakazi wa Lea): Gadi na Asheri.
Palikuwa na wana wa Yakobo waliozaliwa huko Padan Arani.
Zingatia: Dina hatajwi hapa, kwa sababu hakuwa kiongozi wa kabila.
[17] Je ni umbali gani kusini alikoenda Yakobo? (27) Mbali kadiri ya Mamre, au Kirjath Arba (yaani, Hebroni),
[18] Akina nani waliokaa huko? (27) Wazee wake zamani: Ibrahimu na Isaka. Pengine Yakobo alikufa miaka mitatu baadaye.
[19] Sura hii inahitimishaje? (28-29) Sura hii huhitimishwa kwa taarifa ya mauti ya Isaka na tukio lililofuata la maziko kutoka kwa wanawe, Yakobo na Esau.
Esau na Yakobo wakamzika. “Esau na Yakobo sasa walikuwa wamepatana kikamilifu kwa miaka 23. Hivyo si ajabu kumwona Esau akiungana na Yakobo katika desturi ya mwisho kwa ajili ya baba yao waliyemheshimu. Katika mazingira ya namna hiyo Isaka na Ishmaeli alikuwa ameshiriki katika maziko ya Ibrahimu (sura ya 25:9). Isaka alikuwa mtauwa na mwenye kujisalimisha kwa unyenyekevu mbele ya Mungu, mchangamfu na mkarimu kwa wanadamu wenzake. Ikilinganishwa na ile ya Yakobo mwanawe, tabia yake mwenyewe ilikuwa bora zaidi.” (SDABC1/ Genesis 35:29)
Less
MORE FROM MWANZO
Mwanzo 41 (Maswali & Majibu)
November 22, 2018 • Mwongozo wa Biblia.
Mwanzo 38 (Maswali & Majibu)
November 19, 2018 • Mwongozo wa Biblia.
Mwanzo 37 (Maswali & Majibu)
November 18, 2018 • Mwongozo wa Biblia.