Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ngorongoro

Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ngorongoro Akaunti Rasmi ya Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ngorongoro

UJENZI WA DARAJA LA MTO POLOLETI UMEKAMILIKAWakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Ngorongoro wamek...
06/02/2026

UJENZI WA DARAJA LA MTO POLOLETI UMEKAMILIKA

Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Ngorongoro wamekamilisha ujenzi wa Daraja la Mto Pololeti lililopo katika Kata ya Oloipiri. Daraja hilo lina urefu wa mita 22 na limegharimu jumla ya shilingi 314,737,557.62, likiwa linaunganisha Kata ya Oloipiri na Soitsambu.

Ujenzi wa daraja hilo ulianza tarehe 6 Juni 2024 na kukamilika leo tarehe 6 Februari 2026. Kukamilika kwa daraja hili kunalenga kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi, hususan katika kipindi hiki cha msimu wa mvua, kwa kuhakikisha usalama na upatikanaji wa huduma kwa wakati.

TARURA inaendelea kutekeleza miradi ya miundombinu kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Wilaya ya Ngorongoro.

06/02/2026

MBUNGE KUWAUNGA MKONO WANANCHI WA KITONGOJI CHA HARARA

Wananchi wa Kata ya Samunge wameonyesha mshik**ano na uzalendo wa hali ya juu kwa kujenga daraja la Mto Rima lililopo kwenye barabara ya kwenda Mojenenane, Kitongoji cha Hahara, Kijiji cha Samunge. Daraja hilo limejengwa kwa nguvu zao wenyewe na kugharimu jumla ya shilingi milioni 11.
Mheshimiwa Mbunge amepongeza juhudi hizi na kuahidi kuwaunga mkono wananchi kwa hatua waliyochukua. Aidha, amewahimiza wananchi wengine kuiga mfano huu wa kujituma na kuibua miradi ya maendeleo kwa manufaa ya jamii nzima.

05/02/2026
Pongezi Kidato cha Nne
05/02/2026

Pongezi Kidato cha Nne

UTEUZI
29/01/2026

UTEUZI

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amemvisha cheo na kumuapisha Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ...
29/01/2026

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amemvisha cheo na kumuapisha Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-Razaq Ibrahim Badru.

Hafla hiyo iliyofanyika leo tarehe 29 Januari, 2026 Arusha ni baada ya uteuzi wa Kamishna huyo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 26 Mei, 2025 kisha Kamishna Badru kuhitimu mafunzo ya Jeshi la uhifadhi kwa mujibu wa sheria na hatimae kuvishwa cheo na kula kiapo kwa ajili wa utekelezaji wa Majukumu yake ya kuiongoza Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.

Ngorongoro Conservation Area Authority

28/01/2026

Swali :Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza maeneo ya malisho kutoka hekta 3 hadi 6 k**a Ilani ya CCM inavyosema?

Aliuliza Mhe Yannick Ndoinyo (MB) Jimbo la Ngorongoro

Taarifa
28/01/2026

Taarifa

Address

Loliondo
1

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ngorongoro posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ngorongoro:

Share