Tanzania Dairy Board

Tanzania Dairy Board Ukurasa rasmi wa Bodi ya Maziwa Tanzania

Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Prof. George Msalya, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wadau wanaotek...
18/09/2026

Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Prof. George Msalya, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wadau wanaotekeleza Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), kilichofanyika jijini Dodoma, Septemba 17, 2026.

C-SDTP_Maziwa Tanzania Tanzania Dairy Board

17/09/2026


2026 Tumekuja Tena
16/09/2026

2026 Tumekuja Tena

Nyumbani Shuleni Maziwa kwa Lishe Bora
14/09/2026

Nyumbani Shuleni Maziwa kwa Lishe Bora

14/09/2026

Nyumbani, Shuleni Maziwa kwa Lishe Bora

Nyumbani, Shuleni Maziwa kwa Lishe Bora 2026 Tumekuja TenaRS Arusha
11/09/2026

Nyumbani, Shuleni Maziwa kwa Lishe Bora
2026 Tumekuja Tena

RS Arusha

KARATU: KIKUNDI CHA GONGALI CHAPEWA ELIMU YA UZALISHAJI BORA WA MAZIWAUhamasishaji wa kuelekea Siku ya Unywaji Maziwa Sh...
10/09/2026

KARATU: KIKUNDI CHA GONGALI CHAPEWA ELIMU YA UZALISHAJI BORA WA MAZIWA

Uhamasishaji wa kuelekea Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni 2026 umeendelea Wilayani Karatu, ambapo Kikundi cha Gongali kimepatiwa elimu kuhusu uzalishaji bora wa maziwa, ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuzalisha maziwa salama na yenye ubora kwa ajili ya matumizi ya familia na soko.

Kikundi hicho kimeeleza kuwa biashara ya maziwa imekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya wanachama wake, ambapo mafanikio yao yamewafikisha hatua ya kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha, kupitia mapato yatokanayo na shughuli za ufugaji na biashara ya maziwa.

Katika kuelekea maadhimisho hayo, uhamasishaji unaendelea kwa kushirikisha wadau mbalimbali, huku Kikundi cha Gongali kikitarajiwa kushiriki kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, ili kutoa uzoefu na kuhamasisha jamii kuhusu fursa na manufaa yanayopatikana kupitia uzalishaji na matumizi ya maziwa.

RS Arusha Manyara Rs

SIKU YA UNYWAJI MAZIWA SHULENI.... TUKUTANE ARUSHA , SHULENI MAZIWA KWA AFYA BORA
10/09/2026

SIKU YA UNYWAJI MAZIWA SHULENI.... TUKUTANE ARUSHA

, SHULENI MAZIWA KWA AFYA BORA

KIPYENGA CHAPULIZWA ARUSHA, KUELEKEA SIKU YA UNYWAJI MAZIWA SHULENIMaandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa S...
08/09/2026

KIPYENGA CHAPULIZWA ARUSHA, KUELEKEA SIKU YA UNYWAJI MAZIWA SHULENI

Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni 2026 yameanza rasmi mkoani Arusha baada ya Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) na wadau mbalimbali wa Tasnia ya Maziwa kukutana kwa ajili ya kujadili na kuweka mikakati ya pamoja kuelekea maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Septemba 30, 2026.

Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bi. Winfrida Joseph, ambaye ni Afisa Mifugo wa Mkoa, alisisitiza umuhimu wa maandalizi ya pamoja na ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kuhakikisha maadhimisho hayo yanafikia malengo yaliyokusudiwa.

Alieleza kuwa tukio hilo ni fursa muhimu ya kuhamasisha jamii, hususan wazazi, walimu na wanafunzi, kuhusu umuhimu wa unywaji wa maziwa katika lishe, afya na ukuaji wa watoto.

Akizungumza kwa niaba ya Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Kaimu Meneja Ufundi Maziwa, Bi. Deorinidei Mng’ong’o, alieleza kuwa TDB imejipanga kushirikiana na wadau katika kuimarisha uhamasishaji wa unywaji maziwa shuleni, huku akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha maadhimisho hayo yanakuwa chachu ya kujenga utamaduni endelevu wa unywaji wa maziwa miongoni mwa wanafunzi.

Katika kikao hicho, Meneja Masoko wa TDB, Bw. Joseph Semu, aliwasilisha Dhana ya Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni 2026, huku akielezea shughuli na mikakati mbalimbali itakayotekelezwa kabla, wakati na baada ya maadhimisho hayo ili kuongeza uelewa na ushiriki wa wanafunzi, wazazi, walimu na wadau wengine katika kuendeleza unywaji wa maziwa shuleni.

Aidha, washiriki wa kikao hicho walijadili kwa pamoja maeneo muhimu ya maandalizi, ikiwemo uhamasishaji kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, shule na majukwaa ya kijamii, pamoja na namna ya kushirikisha wadau mbalimbali ili kuongeza mwitikio na mwonekano wa maadhimisho hayo.

Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni 2026 inatarajiwa kufanyika Septemba 30, 2026 mkoani Arusha, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) na wadau wake katika kuhamasisha matumizi ya maziwa k**a sehemu ya lishe bora, kuimarisha afya na ukuaji wa watoto, pamoja na kuchochea utamaduni wa unywaji maziwa nchini huku ikienda sambamba na kaul

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Charles Mkombachepa ( wa Tatu katikati), a...
08/09/2026

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Charles Mkombachepa ( wa Tatu katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki kikao cha maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni 2026, mara baada ya kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Septemba 3, 2026.

Kikao hicho kililenga kuweka mikakati ya pamoja ya kuhakikisha maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Septemba 30, 2026 mkoani Arusha yanafanikiwa. 🥛




Address

Nyumba 300
Dodoma
P.O.BOX17029

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Dairy Board posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanzania Dairy Board:

Shortcuts

Share