Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco Karibu kwenye ukurasa rasmi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

ZIMEBAKI SIKU 6 TU! Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linawakaribisha Viongozi na Watendaji...
16/09/2026

ZIMEBAKI SIKU 6 TU!

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linawakaribisha Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika kushiriki mafunzo ya Uongozi, Kodi, Uhasibu na TEHAMA yatakayofanyika tarehe 23 hadi 25 september 2026 katika Ukumbi wa Mabeyo Dodoma. Mafunzo hayo ni ya nadharia na vitendo. Gharama za mafunzo ni TSH 350,000 tu kwa kila mshiriki.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi 0658732050.

CPA MURO: MAGEUZI YA KIUTENDAJI NGUZO YA KUIMARISHA HUDUMA BORA ZA COASCOWatumishi wa Ofisi ya Shirika la Ukaguzi na Usi...
14/09/2026

CPA MURO: MAGEUZI YA KIUTENDAJI NGUZO YA KUIMARISHA HUDUMA BORA ZA COASCO

Watumishi wa Ofisi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) Mkoa wa Morogoro, wameaswa kufanya mageuzi ya kiutendaji na kimtazamo, huku wakizingatia uwajibikaji na uadilifu ili kuimarisha zaidi ubora wa huduma za Shirika.

Rai hiyo imetolewa leo, Septemba 14, 2026, na Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Alphonce Muro, wakati wa mwendelezo wa ziara yake katika Ofisi za Mikoa za Shirika, ambapo ametembelea Ofisi ya COASCO Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusikiliza changamoto na maoni ya watumishi hao ili kuboresha utendaji na ubora wa huduma za Shirika.

CPA Muro amesema kila mtumishi anapaswa kubadili utamaduni wa kiutendaji na kuufanya kuwa chachu ya kuongeza ubora wa huduma za ukaguzi, ushauri wa kitaalam, tafiti, uchunguzi na usimamizi wa vyama vya ushirika na taasisi nyingine.

Aidha, amesisitiza watumishi kufanya kazi kwa uadilifu, kushirikiana na kuwajibika kikamilifu katika majukumu yao ili kuchochea utawala bora katika vyama vya ushirika.

Katika ziara hiyo, CPA Muro amehimiza Ofisi hiyo kuhakikisha Vyama vyote vya Ushirika vilivyopo Mkoa wa Morogoro vinakaguliwa.

Kwa upande wake, Jerad Lwitiko, aliyemwakilisha Mkaguzi wa Mkoa, kwa niaba ya watumishi wenzake, ameahidi ushirikiano wa dhati, uwajibikaji na kujituma katika kutekeleza majukumu yao.

ZIARA YA MKURUGENZI MKUU WA COASCO CPA ALPHONCE MURO KATIKA OFISI YA SHIRIKA MKOA WA DAR ES SALAAM
12/09/2026

ZIARA YA MKURUGENZI MKUU WA COASCO CPA ALPHONCE MURO KATIKA OFISI YA SHIRIKA MKOA WA DAR ES SALAAM

CPA MURO AANZA ZIARA ZA OFISI ZA MIKOA YA COASCO, ASISITIZA UKAGUZI WA VYAMA VYA USHIRIKA KWA ASILIMIA 100Mkurugenzi Mku...
12/09/2026

CPA MURO AANZA ZIARA ZA OFISI ZA MIKOA YA COASCO, ASISITIZA UKAGUZI WA VYAMA VYA USHIRIKA KWA ASILIMIA 100

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), CPA Alphonce Muro, amefanya ziara ya kikazi ya kwanza katika Ofisi ya Mkoa ya Shirika jijini Dar es Salaam na kusisitiza Vyama vya Ushirika vilivyopo Dar es Salaam na Pwani kukaguliwa kwa asilimia 100 ili kuongeza uwajibikaji katika vyama hivyo.

CPA Muro ameyasema hayo leo, Septemba 12, 2026, wakati wa ziara yake katika Ofisi ya Mkoa ya COASCO Dar es Salaam, ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika ofisi za mikoa za Shirika tangu kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu. Katika ziara hiyo, pia ametembelea nyumba za makazi zinazomilikiwa na Shirika zilizopo Chang’ombe na Mtaa wa Mazengo, Upanga, jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, CPA Muro amekutana na watumishi wa ofisi hiyo na kusikiliza changamoto, maoni na mapendekezi yao kwa lengo la kuboresha utendaji na ubora wa huduma za Shirika.

“Tuhakikishe tunakagua Vyama vya Ushirika vya Kifedha na vya mazao kwa asilimia 100 vilivyopo katika maeneo ya Dar es Salaam na Pwani ili kuzidi kuimarisha uwajibikaji katika vyama hivyo,” amesema CPA Muro.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kufanya ukaguzi wenye ubora na unaoleta matokeo, pamoja na kuhakikisha taarifa za ukaguzi zinakuwa na mapendekezo bora na yanayotekelezeka.

Kwa upande wake, Mkaguzi wa Ofisi hiyo, CPA Michael Makundi, kwa niaba ya watumishi, amemshukuru Mkurugenzi Mkuu kwa kufanya kikao hicho kilichowapa nafasi ya kueleza kero, changamoto na maoni yao kwa ajili ya kuboresha utendaji wa Shirika.

ZIMEBAKI SIKU 11 TU! Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linawakaribisha Viongozi na Watendaj...
11/09/2026

ZIMEBAKI SIKU 11 TU!

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linawakaribisha Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika kushiriki mafunzo ya Uongozi, Kodi, Uhasibu na TEHAMA yatakayofanyika tarehe 23 hadi 25 september 2026 katika Ukumbi wa Mabeyo Dodoma. Mafunzo hayo ni ya nadharia na vitendo. Gharama za mafunzo ni TSH 350,000 tu kwa kila mshiriki.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi 0658732050.

ZIMEBAKI SIKU 12 TU! Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linawakaribisha Viongozi na Watendaj...
10/09/2026

ZIMEBAKI SIKU 12 TU!

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linawakaribisha Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika kushiriki mafunzo ya Uongozi, Kodi, Uhasibu na TEHAMA yatakayofanyika tarehe 23 hadi 25 september 2026 katika Ukumbi wa Mabeyo Dodoma. Mafunzo hayo ni ya nadharia na vitendo. Gharama za mafunzo ni TSH 350,000 tu kwa kila mshiriki.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi 0658732050.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Umwagiliaji na Zana za Kilimo, Mhandisi Athumani Kilundumya; na Naibu...
08/09/2026

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Umwagiliaji na Zana za Kilimo, Mhandisi Athumani Kilundumya; na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Prof. Peter L. M. Msoffe wamekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), CPA Alphonce Muro kufuatia uteuzi wake wa hivi karibuni ili kujadili mipango na mikakati ya Shirika hilo katika shughuli za kukagua na kuimarisha utendaji kazi wa Vyama vya Ushirika nchini.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 8 Septemba 2026, katika Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Salamu za pole
08/09/2026

Salamu za pole

Vipaumbele 7 vya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), CPA Alphonce Muro
05/09/2026

Vipaumbele 7 vya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), CPA Alphonce Muro

ZIMEBAKI SIKU 17 TU! Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linawakaribisha Viongozi na Watendaj...
05/09/2026

ZIMEBAKI SIKU 17 TU!

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linawakaribisha Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika kushiriki mafunzo ya Uongozi, Kodi, Uhasibu na TEHAMA yatakayofanyika tarehe 23 hadi 25 september 2026 katika Ukumbi wa Mabeyo Dodoma. Mafunzo hayo ni ya nadharia na vitendo. Gharama za mafunzo ni TSH 350,000 tu kwa kila mshiriki.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi 0658732050.

Address

2 Barabara Ya Hatibu,3 Madukani, S. L. P 761, Dodoma4110
Dodoma
4110

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share