17/09/2026
📌UCSAF YAUNGANISHA VIJIJI 51 MWANZA, WANANCHI 322,820 WAMENUAFAIKA
Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imefikisha huduma za mawasiliano katika vijiji 51 vya Mkoa wa Mwanza, na kuwawezesha wananchi 322,820 kupata huduma za mawasiliano katika maeneo yao.
Vijiji hivyo vimefikishiwa huduma kupitia Mradi wa Kimkakati wa Ujenzi wa Minara 758 ya Mawasiliano, ambao umekamilika na tayari umezinduliwa rasmi. Mradi huo umewezesha kufikisha huduma za mawasiliano katika vijiji 1,400 nchini, hususan maeneo ya vijijini yaliyokuwa hayajafikiwa na huduma hizo.
Kupatikana kwa huduma za mawasiliano kumewawezesha wananchi kurahisisha mawasiliano ya kila siku, kupata taarifa na kutumia huduma mbalimbali zinazotegemea mawasiliano, ikiwemo huduma za kifedha, biashara na intaneti, hivyo kuchangia shughuli za kijamii na kiuchumi katika maeneo yao.