TBS Viwango

TBS Viwango TBS is mandated to undertake measures for quality control of products of all description and to promote standardization in Industry and Trade.

11/09/2026
Mkurugenzi Mkuu TBS, Dkt. Ashura Katunzi, akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TBS wakati wa ziara ya Naibu Wazi...
11/09/2026

Mkurugenzi Mkuu TBS, Dkt. Ashura Katunzi, akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TBS wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Mhe. Dennis Londo (Mb).

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb), ametembelea Ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) zili...
11/09/2026

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb), ametembelea Ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) zilizopo katika Kituo cha Mpaka wa Namanga, Wilaya ya Longido, Mkoani Arusha.

Mhe. Dennis Londo (Mb) ameipongeza TBS kwa kazi nzuri inayofanya na kuitaka kuendelea kuimarisha udhibiti wa ubora wa bidhaa zinazoingia nchini kupitia mipaka, kwa kuhakikisha taratibu za ukaguzi na upimaji wa bidhaa zinafuatwa kwa ufanisi bila kuathiri urahisi wa wafanyabiashara wanaofuata sheria.

Katika ziara hiyo, Mhe. Londo amepokea taarifa kuhusu shughuli zinazofanywa na TBS katika mpaka huo, hususan katika kuhakikisha bidhaa zinazoingia nchini zinakidhi viwango vya ubora na usalama kwa ajili ya kulinda afya, usalama na maslahi ya watumiaji.

Aidha, ziara hiyo imelenga kufahamu changamoto zinazokabili utekelezaji wa majukumu ya TBS mpakani Namanga pamoja na kuangalia maeneo ya kuimarisha ufanisi wa huduma za udhibiti wa bidhaa zinazoingia nchini.

TBS inaendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuhakikisha bidhaa zinazouzwa na kutumika nchini Tanzania zinakuwa bora, salama na zinakidhi viwango vinavyotakiwa.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb), ametembelea kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Viwango House e...
11/09/2026

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb), ametembelea kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Viwango House eneo la Mateves, Mkoani Arusha.

Ziara hiyo imelenga kujionea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hizo, pamoja na kufahamu hatua zinazofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo.

Ujenzi wa Ofisi za TBS Mateves unatarajiwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za viwango na uhakiki wa ubora kwa wananchi, wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa katika Mkoa wa Arusha na maeneo jirani.

Aidha, uwepo wa ofisi katika eneo hilo utasaidia kusogeza huduma za TBS karibu zaidi na wadau, kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma na kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Shirika katika kuhakikisha bidhaa na huduma zinazotumika nchini zinakidhi matakwa ya viwango.

Mkurugenzi Mkuu (TBS) Dkt. Ashura Katunzi (wa kwanza kulia) akiwa pamoja na viongozi wengine wakimfariji Rais wa Jamhuri...
11/09/2026

Mkurugenzi Mkuu (TBS) Dkt. Ashura Katunzi (wa kwanza kulia) akiwa pamoja na viongozi wengine wakimfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan nyumbani kwake Kizimkazi,Zanzibar kufuatiwa kufiwa na mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia tarehe 07 Septemba 2026.

09/09/2026

Address

9524
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 07:30 - 16:00
Tuesday 07:30 - 16:00
Wednesday 07:30 - 16:00
Thursday 07:30 - 16:00
Friday 07:30 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TBS Viwango posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share