National Housing Corporation

National Housing Corporation Government organisation, Real Estate Developer NHC is under the Ministry of Lands, Housing and Settlements Development.

The current National Housing Corporation is the outcome of the decision of the Government to dissolve the Register of building (RoB) through Act of Parliament No.2 of 1990, which vested its responsibilities with the NHC. The former NHC was established by Act of Parliament No.45 of 1962, while RoB was established by Act No.13 of 1971. The Ministry is represented by the Board of Directors which is responsible for the corporate policies and strategies. The day to day management of NHC's business is overseen by the Director General who is responsible to the Board of Directors. Effective from July, 1994, the Corporation's portfolios have been divided into profit centers which are income generating and self-sustaining directorates and cost centers which play a supportive role. This role mandates the NHC to undertake an array of business.
- Construction of houses for sale.
- Construction of buildings as part of approved scheme.
- Provision of facilitating the provision of building materials, components, concrete article and other related articles.
- Business of building contractors, planners or consultants.
- Renting out and managing houses or properties built by the corporation and those acquired by the government.
- Carrying out other activities related to construction of houses or other building built or acquired by the corporation.

🏗️ UBORA KWANZA | UHAKIKISHO WA UBORA NHCKwa NHC, uhakikisho wa ubora ni sehemu muhimu ya kila hatua ya ujenzi.Katika mi...
14/09/2026

🏗️ UBORA KWANZA | UHAKIKISHO WA UBORA NHC

Kwa NHC, uhakikisho wa ubora ni sehemu muhimu ya kila hatua ya ujenzi.

Katika miradi ya Mkwakwani Plaza – Tanga na Samia Housing Scheme Kijichi – Dar es Salaam, wataalamu wa NHC wanaendelea kufanya ukaguzi wa kitaalamu kuhakikisha kila kazi inatekelezwa kwa kuzingatia michoro na vipimo vya mradi, viwango vya ujenzi, usalama na uimara unaotakiwa.

Ukaguzi huu unasaidia kuhakikisha usahihi wa kazi katika kila hatua, kubaini kasoro mapema na kuhakikisha hatua inayofuata ya ujenzi inaanza baada ya viwango vinavyotakiwa kuthibitishwa.

Tunajenga. Tunakagua. Tunahakikisha ubora. ✅

📍 Mkwakwani Plaza – Tanga
📍 Samia Housing Scheme Kijichi – Dar es Salaam

NHC | Tunajenga Taifa Letu

SamiaHousingScheme TunajengaTaifaLetu

🏗️ UBORA KWANZA | MKWAKWANI PLAZAKwa NHC, Quality Assurance (QA) ni sehemu ya kila hatua ya ujenzi.Shuhudia wataalamu wa...
14/09/2026

🏗️ UBORA KWANZA | MKWAKWANI PLAZA

Kwa NHC, Quality Assurance (QA) ni sehemu ya kila hatua ya ujenzi.

Shuhudia wataalamu wa NHC wakifanya ukaguzi katika mradi wa Mkwakwani Plaza, Tanga, kuhakikisha kila kazi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango, ubora, usalama na uimara unaotarajiwa.

Tunajenga, tunakagua na tunahakikisha ubora. ✅

📍 Mkwakwani Plaza – Tanga
NHC | Tunajenga Taifa Letu

Karibu ujipatie nyumba yako sasa
14/09/2026

Karibu ujipatie nyumba yako sasa

ULIKOSA SAMIA HOUSING KAWE? USIVUE MIWANI BADO 😎🏠Uliwahi kutamani kumiliki nyumba Samia Housing Scheme Kawe, lakini furs...
14/09/2026

ULIKOSA SAMIA HOUSING KAWE? USIVUE MIWANI BADO 😎🏠

Uliwahi kutamani kumiliki nyumba Samia Housing Scheme Kawe, lakini fursa ikakupita? Usihuzunike sana… NHC bado ina jambo kwa ajili yako.

Safari ya kumiliki nyumba haijaishia hapo. Kawe 711 inakupa fursa nyingine ya kuwa na nyumba yako katika eneo la Kawe, Dar es Salaam.

Kwa hiyo, ukisikia “Samia Housing Kawe ziliisha”…
😎 vaa miwani vizuri, tazama fursa inayofuata. Samia zingine zinafuata...

🏙️ Kawe 711 – nafasi nyingine ya kusema: HII NI NYUMBA YANGU.

📞 Wasiliana nasi: 0736 114 433

NHC – Tunajenga Taifa Letu.

Uwekezaji DarEsSalaam

KAWE 711: NYUMBA ZIPO, WEWE UKO WAPI? 🏙️🔑Fikiria kuamka asubuhi ukiwa kwenye nyumba yako ya kisasa, katika eneo la Kawe,...
14/09/2026

KAWE 711: NYUMBA ZIPO, WEWE UKO WAPI? 🏙️🔑

Fikiria kuamka asubuhi ukiwa kwenye nyumba yako ya kisasa, katika eneo la Kawe, Dar es Salaam—ukiwa na mazingira yaliyopangwa kwa ajili ya maisha ya kisasa, familia na uwekezaji.

Hiyo ndiyo Kawe 711, mradi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) unaokupa fursa ya kumiliki nyumba katika moja ya maeneo yanayokua kwa kasi jijini Dar es Salaam.

Hapa si suala la kununua nyumba pekee; ni kuchagua mahali pa kuishi, kuwekeza na kujenga thamani ya maisha yako ya baadaye.

🏠 Nyumba zipo. Fursa ipo. Uamuzi ni wako.

Usisubiri mpaka useme “ningejua…”
Tembelea NHC na ujue hatua za kumiliki nyumba yako Kawe 711.

📞 0736 114 433 | 022 210 5002

NHC – Tunajenga Taifa Letu.

RealEstateTanzania

13/09/2026

MEYA TANGA AIPONGEZA NHC KWA MKWAKWANI PLAZA, ATAKA UWEKEZAJI MKUBWA ZAIDI

Meya wa Jiji la Tanga, Mustafa Selebos, ameipongeza NHC kwa jitihada na kasi ya ujenzi wa Mkwakwani Plaza, akisema mradi huo umekuja wakati muafaka kutokana na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na ongezeko la mahitaji ya majengo ya kisasa ya makazi na biashara jijini Tanga.

“Kwanza niwashukuru sana watu wa NHC kwa jitihada zao na kasi yao. Kwa kweli kasi hii imeendana na uhitaji uliopo. Ukiangalia Mkwakwani Plaza sasa, jengo limefikia hatua za mwisho kabisa, jambo ambalo linatia moyo,” amesema Selebos.

Amesema kukua kwa shughuli za Bandari ya Tanga na kuongezeka kwa wageni wanaoingia jijini humo kwa shughuli za biashara na uwekezaji kunazidi kuongeza mahitaji ya nyumba za kisasa pamoja na maeneo bora ya kufanyia biashara.

Kwa mujibu wa Meya huyo, hali hiyo inatoa sababu zaidi kwa NHC kuendelea kutafuta maeneo mengine yenye fursa na kufanya uwekezaji mkubwa zaidi ili kwenda sambamba na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea Tanga.

“Hivyo, kwa NHC naona ipo haja ya kufanya uwekezaji mkubwa zaidi ya huu wa Mkwakwani Plaza. Tanga inafunguka, shughuli za kiuchumi zinaongezeka na watu wanaingia kwa ajili ya fursa mbalimbali. Hii maana yake ni kwamba mahitaji ya nyumba za kisasa na maeneo ya biashara yataendelea kuongezeka,” amesema.

Ameongeza kuwa Mkwakwani Plaza yenyewe imewekwa katika eneo la kimkakati katikati ya Jiji la Tanga, lenye muunganiko mzuri wa barabara zinazoelekea maeneo mbalimbali. Upande wa kaskazini kuna njia inayoelekea Mombasa, huku upande wa kusini kukiwa na njia ya Pangani inayounganisha maeneo yanayoelekea Dar es Salaam.

Kwa mtazamo wake, uchaguzi wa eneo hilo unaonesha namna wataalamu, wahandisi na Menejimenti ya NHC walivyotambua mapema uwezo wa eneo hilo katika biashara na uwekezaji.

“Hii inaonesha kwamba wenzetu wa NHC wamepeleka kitega uchumi katika eneo lenye potential kubwa. Wataalamu, wahandisi na Menejimenti yao wamefikiria vizuri eneo hili, na ninaamini uwekezaji huu utakuwa na ushindani mkubwa. Tunachotamani sasa ni kuona NHC ikiendelea kuwekeza zaidi Tanga,” amesema Selebos.

Mkwakwani Plaza ni mradi wa NHC wa matumizi mchanganyiko unaolenga kutoa

MAGHALA YA NHC MTWARA YAZIDI KUPENDEZA, YAKARIBIA HATUA ZA MWISHOMuonekano mpya wa Maghala ya NHC Mtwara unazidi kujitok...
13/09/2026

MAGHALA YA NHC MTWARA YAZIDI KUPENDEZA, YAKARIBIA HATUA ZA MWISHO

Muonekano mpya wa Maghala ya NHC Mtwara unazidi kujitokeza kadri kazi za umaliziaji zinavyoendelea, huku mradi ukielekea kuwa eneo la kisasa na lenye mazingira rafiki kwa shughuli za biashara na uhifadhi wa bidhaa.

Kwa sasa, kazi mbalimbali zinaendelea ikiwemo ufungaji wa fremu za madirisha ya aluminium, taa za ukutani (wall-mounted lights), ukamilishaji wa plaster za ndani na nje, pamoja na upakaji wa rangi yenye texture katika kuta za nje.

Kazi nyingine zinazohusisha mifumo ya umeme na maji, roller shutters, tiling pamoja na maandalizi ya landscape nazo ni sehemu ya hatua za umaliziaji wa mradi.

Muonekano wa mbele na pembeni wa maghala unaanza kuonesha taswira kamili ya mradi, huku eneo kubwa la nje likitoa nafasi nzuri kwa mzunguko wa magari na shughuli mbalimbali za kuhudumia maghala.

Mradi huu wa NHC Mtwara unajumuisha maghala yenye ukubwa wa takribani mita za mraba 1,000 kila moja, ukiwa uwekezaji wa takribani Shilingi bilioni 4.146.

Kadri kazi zinavyokamilika, NHC inaendelea kuweka mazingira bora ya miundombinu yatakayosaidia biashara, uhifadhi na usafirishaji wa bidhaa, na hivyo kuchangia ukuaji wa shughuli za kiuchumi Mtwara.

NHC – Tunajenga Taifa Letu.

SAMIA HOUSING KIJICHI: NYUMBA ZA 1, 2 NA 3 BEDROOM ZAZIDI KUCHUKUA SURA 🏗️🏠Ujenzi wa Samia Housing Kijichi unaendelea ku...
12/09/2026

SAMIA HOUSING KIJICHI: NYUMBA ZA 1, 2 NA 3 BEDROOM ZAZIDI KUCHUKUA SURA 🏗️🏠

Ujenzi wa Samia Housing Kijichi unaendelea kushika kasi, huku majengo mbalimbali yakifikia hatua tofauti za utekelezaji.

Block A imefikia asilimia 90 ya ujenzi wa kuta za ghorofa ya pili, huku maandalizi ya ghorofa ya tatu yakikamilika. Block D nayo imefikia asilimia 90 ya kuta za ghorofa ya pili, wakati kazi za plastering na maandalizi ya paa zikiendelea.

Block E, yenye nyumba za chumba kimoja, ujenzi wa kuta za ghorofa ya tatu umefikia asilimia 55, huku Block B na C zikielekea hatua ya kumwaga zege la ghorofa ya nne.

Hatua kwa hatua, Samia Housing Kijichi inabadilika kutoka michoro kuwa makazi halisi ya kisasa.

NHC – Tunajenga Taifa Letu. 🇹🇿

MEDELI III: GHOROFA ZINAPANDA, TASWIRA MPYA YA MAKAZI DODOMA YAZIDI KUJITOKEZA 🏗️Ukiangalia maendeleo ya SHS Medeli Phas...
12/09/2026

MEDELI III: GHOROFA ZINAPANDA, TASWIRA MPYA YA MAKAZI DODOMA YAZIDI KUJITOKEZA 🏗️

Ukiangalia maendeleo ya SHS Medeli Phase III, kuna simulizi mbili zinazoendelea kwa wakati mmoja: majengo yanapanda juu, huku kazi za chini zikifanyiwa umakini kuhakikisha ubora unaenda sambamba na kasi.

Leo, Block K na M zimeanza kugusa hatua za ghorofa ya saba, huku Block N ikiwa tayari kwa hatua ya kumwaga zege la beams na slab ya ghorofa ya sita. Block L nayo inaendelea na formwork ya ghorofa ya tano, iliyofikia asilimia 60.

Lakini ujenzi si kwenda juu pekee. Block J, plastering ya ghorofa ya kwanza imefikia asilimia 70, huku Block L na N zikikamilisha kwa asilimia 100 marekebisho ya nafasi za milango na madirisha pamoja na alignment ya kuta na corners.

Jambo la kuvutia zaidi? Kazi zote zilizopangwa kwa siku zimefikia malengo yake, huku curing na usafi wa eneo la mradi pia vikikamilishwa.

Hivyo ndivyo Medeli III inavyoendelea kujengwa—ghorofa kwa ghorofa, hatua kwa hatua, huku kila hatua ikipeleka mradi karibu zaidi na kuwa makazi mapya ya Dodoma.

NHC – Tunajenga Taifa Letu. 🇹🇿

ULUGURU PLAZA YAZIDI KUPAMBA MJI WA MOROGORO, FURSA MPYA ZA BIASHARA ZIKICHOMOZAMOROGORO, 11 Septemba 2026Katikati ya ma...
11/09/2026

ULUGURU PLAZA YAZIDI KUPAMBA MJI WA MOROGORO, FURSA MPYA ZA BIASHARA ZIKICHOMOZA
MOROGORO, 11 Septemba 2026
Katikati ya mandhari ya kuvutia ya Morogoro, Uluguru Plaza ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) inaendelea kuchukua sura mpya, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji unaolenga kuongeza maeneo bora ya biashara na kuchangia mabadiliko ya taswira ya mji huo.
Hadi leo, Septemba 11, 2026, shughuli mbalimbali za ujenzi zimeendelea kwa kasi. Skimming katika ghorofa ya tatu imefikia asilimia 75, huku brandering katika ghorofa ya chini ikiwa imefikia asilimia 85. Plastering ya coplo katika ghorofa ya nne imekamilika kwa asilimia 100, wakati kazi za umeme katika eneo la paa la juu zikiendelea.
Kadri kazi zinavyosonga mbele, Uluguru Plaza inaanza kuonesha taswira ya jengo la kisasa litakaloongeza nafasi na fursa za kufanya biashara katika eneo muhimu la Morogoro.
Kwa wafanyabiashara na wawekezaji wanaotazama ukuaji wa Morogoro kwa jicho la kesho, Uluguru Plaza ni jina la kuanza kulifuatilia sasa.
Uluguru Plaza — nafasi mpya, biashara mpya, Morogoro mpya.

Address

P. O Box 2977
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:30 - 16:00
Tuesday 08:30 - 16:00
Wednesday 08:30 - 16:00
Thursday 08:30 - 16:00
Friday 08:30 - 16:00

Telephone

+255222105002

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when National Housing Corporation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share