16/07/2026
SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Mhe. Ester Amos Bulaya, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Ndugu Benjamin Mataluma, aliyekuwa Katibu wa Vijana wa Kata ya Balili.
Mhe. Bulaya, anatoa pole za dhati kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, viongozi wa CCM Kata ya Balili, pamoja na vijana wote walioguswa na msiba huu mzito.
Ametambua mchango wa marehemu Benjamin Mataluma katika kuwatumikia vijana na kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na ujenzi wa chama katika Kata ya Balili.
Katika kipindi hiki kigumu, Mhe. Bulaya anawaombea familia na wote walioguswa na msiba huu Mwenyezi Mungu awape nguvu, faraja na uvumilivu wa kuhimili majonzi haya makubwa.
"Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe."
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Bunda Mjini