15/05/2026
ULIMWENGU WA MAFANIKIO WA KIJANA: Ndoto, Mipango na Mikakati, Ushindi!🚀
Kijana mwenzangu!, fahamu kwamba mafanikio si tukio la bahati mbaya, bali ni matokeo ya maamuzi thabiti na nidhamu nzuri . Ulimwengu wa leo hauhitaji tu bidii, unahitaji *"MATUMIZI SAHIHI YA AKILI"* 🧠
Hizi hapa ni hatua 4 muhimu sana kwetu sisi vijana za kutuvusha katika bonde la ufukara:
✅ *1. Badili Mtazamo* "Mindset shift ":
Acha kulalamika lalamika kuhusu watu na mazingira. Badala ya kuona vikwazo, anza kuona fursa. Ukiamini unaweza, tayari umeshinda nusu ya vita. Kumbuka penye matatizo ndipo penye fursa!
✅ 2. *Wekeza kwenye Ujuzi*:
Dunia haikulipi kwa sababu unahitaji hela, inakulipa kwa sababu unatoa thamani. Jifunze kitu kipya kila leo...iwe ni teknolojia, au chochote chenye thamani kwa jamii.
Mh. JORAM NKUMBI aliwahi kusema
_"Toa Mchango kwa walimwengu na ulimwengu"_
Akimaanisha walimwengu na ulimwengu watakulipa kwa mchango wako! na si vinginevyo!
✅ 3. *Ishi katika dunia ya uhamasishwaji* "Circle of Influence":
Kamwe huwezi kuruka k**a tai ikiwa unashindana na kuku. Ambatana, suhubiana, changamana na vijana wenye njaa ya mafanikio k**a wewe. Status za marafiki zako ziwe katika kukutoa na kukuhamasisha kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine. Ukiona asilimia 90% ya status za rafiki zako wanapost ujinga, anza kuchukua hatua ya kutafuta marafiki wapya wenye malengo sawa na yako maana hutakuwa na hamasa ya kufika unapokusudia!
✅4. *Epuka hofu ya kushindwa* : Kijana mwenzangu usiogope makosa; kila kosa ni darasa la kukupeleka hatua inayofuata. Usiogope hasara katika biashara kwani hasara hukujenga kuwa imara zaidi, Usiogope kuchekwa kwani wanaocheka hawajui dhamira yako, Usiogope kusemwa vibaya kwani kamwe huwezi mridhisha binadamu!.
*_JIFUNZE HILI MAPEMA SANA!*
Ulimwengu hautoi tuzo kwa watu wenye nia njema, unatoa tuzo kwa watu wanaofanya kazi kwa *akili na bidii.* Kijana mwenzangu amka!, Tumia nguvu zako sasa ukiwa bado una damu changa ili uje kupumzika ukiwa mzee mwenye heshima na utulivu.
Ukweli mchungu unaoumiza ni kwamba kuwa mwema na mpole tu haitoshi duniani, dunia inataka mchango wako......Ni kweli pengine ni mstaarabu, mpole na watu wanakusifia lakini tambua hutokula sifa, tambua hutotoa sifa katika familia yako....kwa hiyo zinduka... Muombe mungu pia fanya kazi kwa akili na bidii *......Ianze akili kisha ndio bidii* " Zingatia sana hili my brothers and sisters!
Pia JUA KWAMBA....
_"Muda ndio mtaji pekee ambao maskini na tajiri wanapewa sawa. Tofauti ipo kwenye matumizi yake"
Sadath Mgenzi
This is the channel for your achievement 👆👆👆...make sure you have joined!
https://whatsapp.com/channel/0029VbBz6vE5kg726hEOIz0z
Africa Civic Dialogue Series ACDS
Shafii K Gongomeko