07/07/2022
Nuru Ya Muthwani ni Dr Jacob Haji Ali Samdamte , ambaye ni mwekezaji, mfanyibiashara na mkazi wa Joska kupitia shirika lake la Samdamte Waters Company wameweza kusambaza maji kwa wakazi wa Joska na Muthwani kwa ujumla. Huyu ndiye kiongozi ambaye ana ari ya kuwatumikia wana Muthwani.
K**a mwekezaji wa Wadi Ya Muthwani anatambua umuhimu wa kuboresha miundo msingi k**a barabara ambazo zimetelekezwa na uongozi tangulizi, ujenzi wa soko ya kisasa katika kila kata, ujenzi wa shule za umma (chekechea), kuleta vituo vya afya karibu, kuimarisha usalama, kushinikiza usambazaji wa bursaries kwa usawa bila ubaguzi, kushinikiza kutengwa viwanja vya umma vya michezo kwa minajili ya kukuza talanta ya vijana.
Huyu ni mgombea ambaye si kazi anatafuta k**a wapinzani wake, la msingi kwake ni kuboresha miundo msingi ya Wadi Ya Muthwani iliotelekezwa na viongozi wabinafsi wasiosera za maendeleo ila porojo.* Maendeleo yatakayo boresha hali za maisha za wakazi wote kwa ujumla.
Mpe Kura zake Dr. Jacob Haji Ali, mgombea asiye chuki au tamaa. Amekomaa kiimani, kibusara na kihekima.
Joska yote imekubali kuwa Mwakilishi Wadi wa Muthwani ni Jacob Haji Ali Samdamte ambaye ndiye Taa ya Wadi Ya Muthwani.
Kutoka Katani, Githunguri, Kamulu, Joska, Kware, Ivovoani, Ndovoini, Muthwani mpaka Kwa Kalusya, mpaka Ng'alaya amekubalika. Samdamte ndiye chaguo letu.
Mnamo Agosti Tisa, ukichukua ballot paper yako usijisumbue kutafutilia weka Tick โ๏ธ katika kisanduku cha kulia cha mgombea wa kwanza ambaye ndiye Taa ya Wadi Ya Muthwani, ambaye ana:
Taa ya mageuzi,
Taa ya barabara bora,
Taa ya shule bora,
Taa ya maji kwa wote,
Taa ya usawa katika usambazaji wa burasies,
Taa ya ujenzi wa soko,
Taa ya kuotesha ajira kwa vijana, Taa ya kuondoa unyanyapaa,
Taa ya Maendeleo,
Taa ya haki na usawa kwa wote.
Usishawishike na siasa duni za porojo, shawishika na siasa za kuimarisha miundo msingi ya Wadi yetu Ya Muthwani ambayo imetelekezwa.