15/09/2026
CCM SI CHAMA CHA KAWAIDA; NI CHAMA CHENYE HISTORIA KUBWA YA TAIFA-NDUGU STEPHEN WASIRA
Akizungumza Leo tarehe 15.09.2026 katika Mafunzo ya Itikadi, Ujenzi wa Chama na Kuongeza Wanachama Wapya, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Stephen Masato Wasira, amesisitiza umuhimu kwa kila mwanachama kuifahamu historia ya Chama chake, kuitambua na kujivunia kuwa sehemu ya Chama chenye historia kubwa katika Taifa.
Ameeleza kuwa tarehe 21 Januari 1977, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TANU na ASP walikutana Dar es Salaam chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa TANU, na Ndugu Aboud Jumbe, Rais wa ASP, na kwa pamoja wakafikia uamuzi wa kuvunja TANU na ASP kuanzia 5 Februari 1977, na kuunda Chama kipya-Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa msingi huo, amesisitiza kuwa mwanachama wa CCM anapaswa kuifahamu historia ya Chama chake, kuthamini misingi yake na kujivunia nafasi yake katika Chama kilichobeba sehemu muhimu ya historia ya Taifa la Tanzania.
“Ukiwa mwanachama wa CCM, lazima ujivunie kuwa mwanachama wa Chama hiki, kwa sababu si Chama cha kawaida.”